TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

#Swali la kujiuliza, je alinunua gari lini!
Je ameanza kuendesha lini?
Je ana uzoefu wa kuendesha gari toka dar mpaka tanga? Kwa sababu kuna watu wengi sana wanajifunza kuendesha gari hapa dar, mara anataka kwenda safari ndefu!! Bila kujua safari ndefu inahitaji uzoefu,
si kila anaekufa ni mungu!
 
jamani hakuna mtu ambae hata onja mauti... sote tuta pita njia hiyo hiyo ila kWa namna tofauti,, Mungu alilaze roho ya shario Millionea mahal pema peponi AMEN
 
duh!! amebugi meeeeenn!!!!
siajabu akifika anakoenda atawaambia dunia hapasomeki meeenn!!!
 
TAARIFA KAMILI YA KIFO CHA SHARO
MILIONEA HII HAPA Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo
Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi
Tanga akisema “leo majira ya saa mbili
usiku kwenye barabara ya Segera Muheza
mtu mmoja alietambulika kwa jina la
Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR
Toyota Harrier akitokea Dar es salaam
kwenda Muheza alipofika eneo la
Maguzonizonga
wilayani Muheza hilo gari lake liliacha
njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa
marehemu umehifadhiwa kwenye
hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona kali
sana wala ubovu wa barabara kwenye
sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo
gari imehifadhiwa mahali salama kwa
sababu haitembei.
Kwenye gari alikua mwenyewe.
 
RIP Sharo Millionea nimeskitika sana kwa msiba huu,kuna siku nakumbuka alipata ajali ya Basi maeneo ya Morogoro. Pole familia,Pole Marafiki,Pole Mzee Majuto na Wasanii wooote "Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe!
 
Omama!!! kamata mwizi men!!
Sajuki (bongo movie)wametoka kwenye show iringa wamemkuta amepata ajali tanga muheza wakamuokota na kumpeleka hospital akafia hospital
hizi nyepesi nyepesi iringa na tanga wapi wapi???sijaelewa
hapa
bongo movie wanamzika john kesho kisha wanaenda tanga busses are ready
rest in peace my brother from another mother!!! Omama
 
kama kumbu kumbu zangu ziko vizuri sharo anakuwa msanii wa tatu kufariki akiwa anafanya kazi karibu na mzee majuto........anyway RIP sharo!
 
kiukwel inasikitisha sana,braza ndyo kwnza alikuwa anaanza k uenjoy jasho lake.Pole sana mzee majuto kijana wako huyo.
 
"Gone Too Soon Man"
Like A Comet
Blazing 'Cross The Evening Sky
Gone Too Soon

Like A Rainbow
Fading In The Twinkling Of An Eye
Gone Too Soon

Shiny And Sparkly
And Splendidly Bright
Here One Day
Gone One Night

Like The Loss Of Sunlight
On A Cloudy Afternoon
Gone Too Soon

Like A Castle
Built Upon A Sandy Beach
Gone Too Soon

Like A Perfect Flower
That Is Just Beyond Your Reach
Gone Too Soon

Born To Amuse, To Inspire, To Delight
Here One Day
Gone One Night

Like A Sunset
Dying With The Rising Of The Moon
Gone Too Soon

Gone Too Soon
 
Lala Salama Sharo,,,mungu wa majeshi atakufufua siku ya mwisho..ila ningepata faraja sana kama ningejua kama ulipata muda wa kutubu dhambi zako!

Hili la kutubu ndio kuu kuliko yote mkuu, tukiwa wazima tunamsahau Muumba nakujiona sisi ndio sisi, leo kaondoka sharo kesho haijulikani ni nani lakini bado binadamu tunawekeana vinyongo, dharau, tunadhulumu as if tunajua kesho itakuwaje......RIP SHARO...... tuliobaki tukeshe tukiomba, tusameheane, tupendane na kuchukuliana kama ndugu maana hatujui muda wala saa tutakayozimika.
 
Back
Top Bottom