Shambulio la Lissu, sawa na mtu kutafuta kichwa chake

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,866
41,929
Yamesemwa mengi, yamependekezwa mengi. Mengine ni halisia, mengine ya kuwapumbaza watu, mengine ya kuwadharau watu kuwa hawana akili. Yafuatayo ni ukweli ambao unatuambia kuwa waovu wote waliohusika na shambulio dhidi ya uhai wa Tundu Lisu, wanafahamika.

1) Jiwe anatawala kwa mkono wa chuma, mwenyewe anajiita ni Jiwe, atamka wazi kuwa eti yupo kwenye vita ya uchumi. Anatamka kuwa ameshikilia containers za za Accia zenye dhahabu.

Adai kuwa kuna mtu amempigia Dio wa Accia anaomba nakala ya mkataba kati ya Accia na Sirikali, na kusema kuwa sijui anautaka wa nini. Anaendelea kudai kuwa hii ni vita, anayeenda kinyume (ikiwa na maana ya kinyume cha matendo na fikra zake), ni msaliti. Adai kuwa msaliti hatakiwi kuishi.

2) Siku chache kabla, Lisu alimtafuta Dio kwa simu. Dio hakupokea. Lisu alimtumia meseji Dio kumwomba nakala ya mkataba kati ya Accia na Sirikali, Dio hakumjibu.

3) Bashite, Jiwe anafanya mkutano mkoani mwake, yeye hayupo. Aonekana Dodoma hotel busy na simu yake akitoa maelekezo.

4) Gari la washambuliaji linaingia kwenye compound ya makazi ya viongozi ambako Lisu anaishi. Tofauti na siku nyingine zote, getini hakuna askari hata mmoja. Washambuliaji wanafanya shambulio, gari la washambuliaji linatoka kwenye compound, barabarani magari na pikipiki zinasimamishwa ili gari la washambuliaji lipite.

5) Baada ya shambulio, Lisu anafikishwa hospitalini, Jiwe kupitia simu ya Mahga, anaongea na Mwglu kumwagiza aitishe vyombo vya habari na kuwaambia kuwa Sirikali haihusiki kwenye shambulio dhidi ya Lisu. Mwglu anashauriana na Mahga, anaamua kukaa kimya.

6) Kwenye mawasiliano ya siri Bashite anamjulisha Jiwe kuwa kazi amemaliza, Jiwe anang'aka na kusema kuwa mbona amejeruhiwa tu, na yupo hospitali. Bashite anamwambia kuwa amehakikishiwa ni suala la muda tu, kwa idadi ile ya risasi, kazi imekwisha.

7) Jiwe anaagiza kuwa Lisu akishakufa mwili wake usipelekwe Dar, usafirishwe kwenda Singida, na Dodoma kusiwepo na heshima za Mwisho.

8) Kalmni anampigia simu mkewe kuwa kuna watu wanakuja kuondoa CCTV cameras, awaruhusu. Camera zinaondolewa.

9) Mambo ya sasa anasema wamewatambua washambuliaji. CCTV camera wamezipata (baadaye alikuja kukana kuwa hawakupata CCTV cameras).

10) kesho yake Bashite aonekana Morogoro. Gari inayoaminika kutumika kwenye shambulio yaonekana ikiwa imeteketezwa kwa moto Morogoro.

11) Lissu anaendelea na matibabu Nairobi, Jiwe anaagiza kuwa hapendi kuona watu wanaenda kumwona Lisu hospitali.

12) Mwglu afutwa uwaziri kwa sababu ya kukaidi agizo la Jiwe la kuwaita waandishi wa habari kuwaambia kuwa Serikali haihusiki.

Wale wanaosema eti polisi wafanye uchunguzi wa waliohusika kwenye shambulio dhidi ya Lisu, hivi kuna mtu aliwahi kufanya uchunguzi kutambua kilipo kichwa chake?

Siku nuru itakapoliangazia Taifa hili, siyo kwamba kutafanyika uchunguzi wa wahusika wa shambulio dhidi ya Lisu, bali watakamatwa na kupelekwa mahakamani.
 
Inatosha Sasa mjadala wa Lissu ufungwe aliyempiga Lissu lisasi kashakufa so bora huu mjadala tuufunge inatosha!!!

Lissu agombee Urais by 2025 ili tutengeneze strong political kupitia upinzani tupate Katiba na kuweka sheria za kuwanyoosha viongozi wajinga wajinga wakiingia madarakani!!
 
Lini huyu Lisu atazungumzia sera za maendeleo kwa nchi?

Sabaya jambazi ukiambiwa upeleke ushahidi wa alichokuibia utapeleka?
 
Hili Suala Tundu Lissu kila mtu ana ongea lake, mengi ni uongo tu.

Kwahiyo ushahidi wa Chadema ni hotuba ra Rais kuwa tuko vitani yeyote anaepinga lazima apoteze maisha? Wekeni hapa Audio au video ya Rais akiamuru Lissu apigwe risasi, mbona mna shindwa kupata mawa siliano ya siku lissu ana pigwa risasi na resources na pesa zote mlizonazo upinzani?

Tuna taka evidence sio maneno , kila mtu anaweza ongea lolote analofikiri kutoka kichwani, lakini not guilty until proven guilty.
 
Jambo lipo wazi kabisa kwamba mwendazake alitaka kummua Lissu, afe na azikwe kama raia wa kawaida kabisa pale kwao Ikungi bila serikali kuchangia chochote; mishe inakwama, Jiwe kwa hasira kali anaamua mengi kuwahusu wale wote waliokaidi amri yake.
  • Lissu anayimwa fedha za matibabu na Serikali ya jiwe.
  • Jiwe anatoa amri ni marufuku kiongozi wa Serikali ama wa Chama kumtembelea Hosp ama hata kumpigia simu
  • Mama Samia anaibukia Hosp Nairobi, baada ya hapo yanaibuka mengi chini ya kapeti.
  • Hujuma za kutaka kummalizia Lissu pale Hosp Nairobi zinagonga mwamba
  • Lissu anahamishiwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi
  • Serikali kupitia Bunge linamtangaza ni mzururaji na hajulikani alipo
  • Spika wa Bunge anapitisha hoja kwamba avuliwe Ubunge
  • Tume inatangaza Jimbo lipo wazi, ubunge wa Lissu unapotea
  • Lissu ananyimwa mafao yake yote, msaada unaendelea kwa wasamalia wema kumtibia
  • Lissu anapigiwa simu kwamba Daktari wake pale NBI hopital kwamba "Rafiki yako kaletwa NBI hosp hapa ila hatoboi", jiwe anarudishwa Bongo land
  • Lissu anauliza "Rais wetu yupo wapi wiki ya 2 sasa hatoki hadharani" anajibiwa kwa mzaha kwamba anamtaka wa nini kwani ni mumewe?
  • Mama anakwenda Tanga kwa Ziara ya kikazi, anatangaza kwamba tusiwe na wasi Rais yupo salama ni mambo ya homa homa tu.
  • Waziri Mkuu pia anatutangazia kwamba tuachana na mambo ya mitandaoni - Rais yupo gado.

endeleeni wengine nishachoka....
 
Back
Top Bottom