Shahidi kesi ya bilionea Msuya: Niliteswa mpaka nikahasiwa na Polisi na kuamua kumfukuza mke wangu

Inawezekana wanahusika, kila mifumo yetu ya upelelezi bado, yaani uwezo wa kumpiga mtu maswali ajikanyage mpaka aonekane kweli kahusika bado ni shida.
Uko sahihi kabisa Mtanzania mwenzangu. Kwenye suala la upelelezi Jeshi letu la Polisi bado lipo nyuma kabisa. Nimekuwa mfuatiliaji na muangaliaji wa kipindi cha TV Crime Investigation kwa muda mrefu. Ukiona vile wenzetu wanavyo tumia ujuzi na maarifa kupata ushahidi kabla ya kufanya ukamataji utasema kweli hawa ni wapelelezi. Sisi tukio linafanyika usiku ikifika asubuhi tayari wanafanya arrest , unapatwa na wasiwasi hivi washiriki wa matukio ni wajinga kiasi hicho?

Hata kama mahakama haikubali lakini ni ukweli usio pingika vituoni watuhumiwa hiteswa kukiri kosa wanasahau kuwa wakienda mahakama na mtuhumiwa aka kana maelezo yaliyo andikwa na Polisi basi Jamhuri huwa haina njia mbadala ya kuithibitishia mahakama kuwa flani ndo musika wa tukio hilo.

Kwa wataalam wa sheria wanakuambia hakuna kesi rahisi Dunia kama kesi ya mauaji kwani shahidi namba moja ni marehemu, mashahidi wangine huwa ni wakuunga unga tu....kwani ni lazima mahakama ijiridhishe X ndo aliyetoa uhai wa Y bila mashaka yoyote.....
 
Tatizo ni kwamba Waliopataga Division Four hata Zero wakiwa form four ndo Mapolisi Akili ni ndogo sana.. Yan kutumia akili kuweza pata ushahidi hawawezi ni kutumia nguvu. Hawa hata wakifanya tukio wao njia ya kudanganya bado kwao ni tabu Wanabaki kusema hakuna Ushahidi wakutosha,,
 
Inawezekana wanahusika, kila mifumo yetu ya upelelezi bado, yaani uwezo wa kumpiga mtu maswali ajikanyage mpaka aonekane kweli kahusika bado ni shida.

Nimelipenda swali la " kama ulikuwa umefungwa kitambaa na umelala chali ulijuaje kuwa hapo ni nje ya kituo cha polisi flani"
Na hapo ndo uongo wa jamaa utakapomcost.. All in all torcharing is inevitable during interrogation process.. Hakuna mtuhumiwa anaekubali kosa Kirahisi
 
Hawa watu wanatia shaka kidogo nahisi wanaweza kuusika ilikuwaje wote wanaotuhumiwa wawe nje ya arusha sikui hiyo kama sio mipango rejea filamu ya kihindi hamza kanuni utajua ni picha ikichexwa
Kabisa mkuu, wanatia shaka kweli
 
Na hapo ndo uongo wa jamaa utakapomcost.. All in all torcharing is inevitable during interrogation process.. Hakuna mtuhumiwa anaekubali kosa Kirahisi
Wewe ndio unafahamu vizuri kazi ya upelelezi ikoje; wengine wanabwabwaja tu nyuma ya keyboard. Hivi kupata ticket ya basi bongo na kuiandika ikaonekana genuine ni rocket science?? Documents za bongo kuzipata ni easy kama kumsukuma mlevi tu.
 
Tatizo ni kwamba Waliopataga Division Four hata Zero wakiwa form four ndo Mapolisi Akili ni ndogo sana.. Yan kutumia akili kuweza pata ushahidi hawawezi ni kutumia nguvu. Hawa hata wakifanya tukio wao njia ya kudanganya bado kwao ni tabu Wanabaki kusema hakuna Ushahidi wakutosha,,
Msilaumu polisi kunaambao wako vizuri sana kwenye hii kazi kuna siku mimi binafsi nilishawahi kukamatwa kwa kesi fulani ila ilikuwa ni kuchukiana kitaa jamaa akapanda polisi akaongea uongo wake ili nikamatwe kweli nilikamatwa nikaulizwa maswali mengi nikapelekwa polisi kwa mahojiano zaidi kufika nikahojiwa nikaachiwa siku hiyohiyo kumbe baada ya kupeleka umbea. wake polisi walinifuatilia wakagundua ni uongo ila hawakuniambia chochote zaidi tu we nenda tutakuita mpaka leo mungu ni mwema polisi wako vizuri sana ila sio wote
 
Bora ukubali afu ukatae mahakamani

umewaza kama mimi, nikiona spoku tu nakubali nikifka mahakaman nasema wazi kua m nilikubali mana najua ambacho ningepata(hata historia inaeleza) na kweli kama lengo lao ni kuniuzia kesi najua hawataniacha watanitesa mpk nisain. Uteswe, uhasiwe halaf ndo usain huo n ukunguni. Unless otherwise uwe unajiamin hata wakufanyeje husemi
 
Unachosoma kwenye magazeti ni sehemu ndogo mno ya mwenendo wa kesi. Hata kama ana hizo tiketi kuna mambo mengine mengi yanazingatiwa. Kwa mfano unaweza kusafiri asubuhi na basi ukaenda mpaka Singida jioni ukarudi na gari binafsi na ukafanya uhalifu Arusha halafu tena ukarudi na hilo hilo gari la binafsi mpaka Singida na kesho yake ukakata tiketi ya kurudi Arusha na ukarudi kwa basi. Hiyo yote ni katika kutengeza kitu kinachoitwa alibi (soma alay-bai) ya kuwa hukuwepo wakati wa uhalifu

Pia unaweza kumtuma mtu akate Kwa jina lako maana ticket zinakatwa kiholela tu
 
Hivi kwa mini polisi au mawakili wao wasiwasiliane na makampuni ya simu zao na kujua siku hio,mda huo wa mauaji walikua wapi?Very simple.Record zipo mbona. Bongo bana.
Kesi bado inaendelea na hatujui kuna ushahidi gani uko mbele ya mahakama. Nadhani kutakuwa na ushahidi wa aina nyingi. Kuhusu rekodi za simu kwa mhalifu mzoefu anaweza asitembee na simu yake ya siku zote wakati wa mauaji. Anajua watakuja ku-track wajue ni nani alikuwa eneo la tukio.
 
watuhumiwa watakuwa wanahusika hivi kwanza wanajitetea kwa hoja zinazofanana kuonekana wamepangana kutoa hoja

kingine huyo aliyesema alitolewa chuga mpaka kia huku amefungwa kitambaa usoni na amelazwa kifudifudi na akawa amezungukwa na polisi alijuaje kuwa anapelekwa kia wakati hapo umefungwa na kitambaa na kuzungukwa na huwezi sema hata mwanga wa jua umekupiga usoni kitambaa kikawa transparent ukaona mandhari ya nje hapa niseme kuna ukakasi hata kama unaexperience na barabara sio hivi

angefungwa kitambaa na kulazwa hivyohivyo then azungushwe moshi town baadae safari ya kwenda chuga ianze akifika kia atamke mwenyewe hapa ni kia ili aidhibitishie mahakama kuwa ana uzoefu na hiyo road
 
Mamaeee "" police wa Tanzania ...kama kweli kwa Mungu patakuwa na hukumu kwa watenda dhambi"" basi nikija kumuona askari .police . mahakimu na mawakili wanaingia peponi "" nitakata rufaa""
kama hapo wakili wa serikali alikuwa Anataka kupindisha ushahidi uliowazi kabisa kwa mshitakiwa "" walikuwa na mantiki ipi yakutotka kuzitambua hizo ticket"" yaani wanatetea matumbo yao tu"" period ""
 
iala wahusika wajanja sana " kila muhusika anadai alisafiri " aliporudi ndio akakamatwa duuhh"" haiwezekani watu wanaokana kuto fahamiana wao wote watoe maelezo yakusafiri tu "" halafu baada ya kurudi safarini ndio wakaja kukamatwa ....iko namna """
 
Back
Top Bottom