Shahidi aliyehongwa milioni 5 awakaanga ccm singida-chadema hawanunuliki

hivi nayo hii ni kesi ? maana tangu mwanzo ashahidi wote hawana cha maana cha kusema

Ni suala la ajabu mkuu kwani hata kesi ya kupinga ubunge wa CDM ARUSHA mashahidi walionekana kutokuwa makini lakini umeyasikia matokeo ya hukumu? Kama ulikuwa ukifuatilia sana post za watu ttofuati humu ndani ya forum utagundua kuwa zilikuwepo threads ambazo zilikuwa zikituupdate kuhusu kesi ya Arusha. Mungu na atuepushie mbali kwani wasipoangalia CCM wataliingiza Taifa katika gharama nyingine kubwa huku wakijua fika kwamba mashahidi ni wa kupikwa
 
Hizo kesi zimefunguliwa makusudi ili kuwapotezea wabunge wa chadema muda wa kufanya kazi katika majimbo yao. Wanawachosha kwa kesi ili wasi concentrate kwenye mambo ya maana.
 
Haki ina simama batili inajitenga,kutengua ubunge wa wapinzani ni silaha duni inayotumiwa na watawala wabovu waliochokwa na watawaliwa.Na kama lengo ni kufifisha juhudi za ukombozi wa katiba mpya na mfumo mpya wa kujiamulia mambo yetu wenyewe,basi wajue wameula wa chuya,kwani kila mchuma janga hula na wa kwao.Watahangaika sana ila mwisho wa siku kidedea atajulikana ni nani.Tukiamua hata bila katiba mpya tunaweza kujikomboa bila hata kuwategemea wanasiasa,CCM angalieni mchezo huo mchafu mnao ucheza hauna tija bali kutuingiza kwenye janga ambalo itakuwa historia kwa nchi zetu za Afrika.
 
:shock:by Ndalahwa
Mimi naona baada ya kuona sanduku la kura litawaumbua kwenye chaguzi zijazo, ccm kwa kusaidiwa na dola watatumia mabavu kushinda, kwa njia yoyote haramu. na hapo ndipo watakapoitumbukiza nchi yetu kwenye matatizo kwani kizazi cha sasa hakitakubali. Zanzibar raia wasio hatia walitwangwa rirasi.hali ya ccm sasa hivi mbaya na itaanza kuogopwa na kila mtu,sasa hivi kuvaa rangi za chama hicho ni fedheha hata wao wameanza kuzionea aibu.
 
Back
Top Bottom