shabiki siku zote si mchezaji

bamwaiche

Member
Aug 30, 2011
50
8
Mwigulu ndugai na makinda wao ni mashabiki wa chama na si wanchama, mwanachama huwa hongozwi na hulka za hisia bali hekima, busala na utashi wa kubaini ukweli na kusimamia haki. Shabiki siku zote haijui haki wala hatambui ukweli ni upi, isipokuwa anakurupushwa na hisia juu ya kile anachokishabikia. Mfano Mh. Serukamba anatamka hayo hadharani huku akisisitiza wananchi tusikilize kwamba yeye ni bingwa wa kutukana tena kwa lugha ya kigeni, ambayo amesomeshwa na fedha za sisi watanzania.

Ama kwa hakika naibu spika JN hajatutendea haki sisi raia wa Nchi hii. Cha kushangaza zaidi pale aliporuhusu Bwana serukamba kuendelea kuongea hata alipotukana, nasema hii si bahati mbaya hata kidogo, Bali ni namna ambavyo chombo hiki mhimu kilivoamua kupoka haki zetu za kujadili masuala ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Umbuka ni makinda aliyekemea vikali kuhusu matusi hayo kiasi kwamba alisema hawezi hata kutamka, leo anamfumbia macho serukamba, anataka wananchi tumweleweje?

Ikumbukwe kuwa hawa watu wanatumia rasilimali nyingi za taifa hili. Je hawa wana tofauti na wnyang'anyi wa mali za watu? Je ukitenda haki hutaonekana mwadilifu katika chama chako?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom