Shabiby line tuoneeni huruma abiria....!!!

Mnatuleta kwenye migahawa ya ghali sana kwa huduma za chakula, au mnataka turudi kwenye Zama za kusafiri huku tumebeba mikate na soda?
kuna mgahawa mmoja wa ajabu upo pale morogoro msamvu aisee, chakula kichafu, wanauza chakula cha 1500 kwa shs.8000, hata chakula cha mamantilie ni kuzuri afu wana customer care mbovu, ajabu sana. bora hata pale pa zamani.
 
Dom-Dar mkuu
Sawa, nikujuze tu, vyakula vya njiani huwa wengi wanawalisha viporo na ndio maana abiria wengi hukamatwa na matumbo ya kuhara.
Vyakula vinabaki, wanaweka kwenye freezer kesho yake unapashiwa.
vyakula vya njiani vyafaa mtu ambaye hajiwezi kabisa lakini ili kuondoa huo ukiritimba ni kuhama kabisa kwenye hayo mabasi maana hasikilizi kilio chenu.
 
Bora wangesimama pale Cates Hotel, Kwa ile complex sijui inaitwa Dakawa au Msolwa, ina vitu vizuri hata kama bei kubwa.
kuna mgahawa mmoja wa ajabu upo pale morogoro msamvu aisee, chakula kichafu, wanauza chakula cha 1500 kwa shs.8000, hata chakula cha mamantilie ni kuzuri afu wana customer care mbovu, ajabu sana. bora hata pale pa zamani.
 
Thread 'Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo' Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†...
wao kama ni madereva, wanakuwa na kamisheni kwanza ya chakula bure na pili ya pesa. sasa mwenye mabasi sijui kama analijua hilo. kiukweli inakera mno mno. unaweza kusafiri na mtoto mimi naweza nisile ila mtoto unatamani umnunulie kitu cha kutafuna hata kama kidogo, shida sasa unaogopa mtoto asije kuugua tumbo. watu wamejazana kama mtaa wa congo, choo haipo mbali, watu wote wanaotoka chooni na mimaji waliyokanyaga kule chooni wanapita na kukanyaga karibu na vyakula, watu wenyewe wa morogoro wanatawadhaga bila kunawa na sabuni hao.
 
kuna mgahawa mmoja wa ajabu upo pale morogoro msamvu aisee, chakula kichafu, wanauza chakula cha 1500 kwa shs.8000, hata chakula cha mamantilie ni kuzuri afu wana customer care mbovu, ajabu sana. bora hata pale pa zamani.
I think ndio wametuleta hapa Leo. Kwa nje si kuna kina mama kibao wanauza ndizi na machungwa? Imebidi ninunue tu ndizi kisukari za buku mbili na maji ya kunywa. Imagine ka robo kuku elfu sita, kuku mwenyewe si kuku sijui njiwa
 
mimi wale huwa nawafananisha na wachinja kuku wa sokoni, anakulipisha 1000 anakuchinjia na kunyonyoa manyoya, ila kichwa na miguu hakupi, ukifanya mchezo hata filigisi anaweza kuchukua, jioni vimejaa vindoo anauza kwa mamantilie kwa pesa ndefu tu, vya kukaangia na pilipili then wanauza kwa wanywa chibuku na mnazi huko uswahilini.
 
Back
Top Bottom