BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,032
- Thread starter
- #41
Mkuu Nguruvi3 hawa watu ni wahuni sana sijui kwanini wanataka kulidanganya Taifa mchana kweupe kuhusu kiasi halisi kilichokusanywa na uongo huo wanaousema ni kwa faida ya nani. UK imetoa 6.3 billion na kwingine inaonekana ni 6.7 billion (conversion rate inahusu hapa) India wametoa shilingi 545 million, Uganda shilingi 437 million, Majaliwa alikusanya bilioni 1.4 hii ni baadhi tu ya michango ambayo ni zaidi ya bilioni 8 sasa iweje leo tuambiwe zilikusanywa 5 billion tu!?
Na kama unavyosema hawa wana Kagera waliopata maafa haya nao ni walipa kodi nchini miaka nenda miaka rudi kwanini Serikali ishindwe kutoka bilioni 20 au hata zaidi kuwasaidia kwenye haya maafa!? Kwanini Serikali itegemee tu pesa za michango toka ndani na nje ya nchi? Nina wasiwasi hata hizo milioni 800 zilizotumika hazikuwafikia wahanga wa tetemeko kama ziliwafikia basi ni sehemu ndogo sana zilizowafikia.
Iweje wiki ya saba sasa Serikali inashindwa kusambaza pesa hizo kwa wahanga na huku wakiendelea kuishi nje, hawana maji, hawana chakula!? tatizo ni nini hasa Serikali inaendelea kuzikumbatia pesa hizi?

Hili la tetemeko linatatiza sana
Kwanza, tetemeko limeathiri watu na mali zao. Kwa hesabu zao zilihitajika Bilioni kadhaa kurudisha hali
Kwa minajili ya mjadala tuseme ni Bilioni 20. Hivi kweli serikali inayokusanya 1.2T imeshindwa kutoa bilioni 20 hadi tuite mabalozi kwa misaada?
Mh Makamba alitueleza, katika kero za muungano JMT ilitoa bilioni 29 kwa budget support ya Zanzibar
Serikali hiyo hiyo imeshindwa kutenga kiasi cha bilioni 20 kwa Walipa kodi wa Kagera!
Pili, tulisikia Kenya na Uganda wamechangia yakiwemo mataifa mengine na watu binafsi
Leo namba zinapishana, mara bilioni hizi mara zile
Ni wakati sasa kila kitu kiwekwe wazi wananchi wajue nini kilichangwa na kimeelekezwa wapi
Tatu, leo waziri mkuu bado anatembelea magofu ya shule. Ina maana hakuna kilichofanyika hadi wakati huu
Hivi hatuna wataalamu wanaoweza kuchora, na contractors wanaoweza kujenga shle katika muda mfupi?
Ile dhana ya hapa kazi ipo wapi?