serikali yawatuliza waliomaliza ualimu

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
Send to a friend SERIKALI hatimaye imetangaza kuwaajiri walimu wapya 16,000 waliokuwa wakihaha mitaani kwa kuhoifia kutoajiriwa baada ya kumaliza masomo yao tangu Mei mwaka jana.

Kwa hatua hiyo, serikali imewatoa hofu walimu hao wenye stashahada na shahada waliomaliza vyuo mwaka jana kati ya Mei na Juni ambao walikuwa washangaa kutopata ajira ya moja kwa moja kama ilivyo kawaida kwa taaluma hiyo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti,Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia alisema kwa sasa tayari serikali imejiridhisha baada ya uhakiki wa majina kumalizika na kwamba wameishatoa ruhusa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Tamisemi kuwapangia vituo vya kazi walimu hao.

Awali ilidaiwa kuwa sababu ya kucheleweshwa kwa walimu hao kupata ajira ilitokana na ongezeko la walimu waliokuwa kazini na kwenda kujiendeleza hali ambayo serikali ilitakiwa kufanya uchambuzi wa majina hayo kati ya walimu wapya na wale waliopo kazini ili kuepuka kumpangia mwalimu kituo zaidi ya kimoja cha kazi.

“Kwa sasa tayari tumejiridhisha mara baada ya kufanya kazi hiyo kwa wale walio na sifa tumeiagiza Wizara ya Elimu na Tamisemi kuwapangia vituo vya kazi kuanzia sasa, kwahiyo walimu hao wasiwe na wasiwasi, ajira zao zitatoka muda wowote kuanzia sasa,”alisema Ghasia.

Alisema kazi iliyobaki ni ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) kuwapangia vituo walimu hao ili waanze kufanya kazi na kuepusha lawama zilizokuwa zimetawala kwa wananchi na walimu wenyewe.

Alisema serikali haikuwa na nia mbaya ila kwa kawaida ni lazima ijiridhishe ili kuepuka malumbano ambayo yanaweza kujitokeza hapo baadaye.

“Sio kwamba serikali ilikuwa imewatelekeza walimu hao, bali kama tulivyosema awali kwamba ni lazima tufanye uchambuzi wa majina ya walimu waliotoka moja kwa moja vyuoni na kuna waliokwenda kujiendeleza”, alifafanua.

Aidha kwa upande wa walimu hao waliozungumza na Mwananchi jana walisema wana hofu ya kupangiwa vituo hivyo na kukuta hakuna mazingira yoyote yalioandaliwa na kuiomba serikali kuwapatia mahitaji muhimu ambayo yanahitajika kwa mfanyakazi ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

“Inasikitisha kuona mfanyakazi anapangiwa kituo chake cha kazi halafu hakuti hata sehemu ya kulala, mshahara wenyewe unamaliza zaidi ya miezi mitano , tunaiomba serikali ituangalie kutupatia haki zetu mapema kama kweli wanasema ukweli juu ya ajira zetu,”alisema mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Alizitaka wizara zilizoagizwa kutoa nafasi za kazi zifanye haraka ili kuona kama walimu watarudisha imani juu ya ajira zao na kwamba baadhi yao tayari wameishakata tamaa kutokana na kutoelewa hatima ya ajira zao.
Ata hivyo baadhi ya walimu hao tayari walikuwa wameishaomba kazi katika kampuni binafsi na sasa wanafanya kazi kwenye kampuni husika zikiwemo kampuni za simu.

SOSI: MWANANCHI

WAZO: WANAFANYA HIVYO MUDA HUU ILI WAWALIPE DOWANS SI MNASEMA HELA HAKUNA?
 
Back
Top Bottom