Serikali yatangaza Mkoa, Wilaya na Tarafa mpya za Tanzania

Habari wanajf:
Ni jambo la kushangaza na kusikitisha juu ya walichokisema bungune jana waziri mkuu na rais hasa juu ya uamuzi wa serikali kuongeza idadi ya mikoa na wilaya.
Wakati wa mchakato wa kuandika katiba mpya, tume ya rais ilikuja na wazo la kuwa na serikali tatu, lakini serikali ya ccm kupitia "tume ya Samwel Sitta" walipinga kwa nguvu zote mapendekezo ya wananchi kwa tume ya rais ya katiba ya kutaka serikali tatu kwa madai kuwa itakuwa gharama kubwa.

Sasa ongezeko la mikoa wilaya na halmashauri zinazidi kuongeza gharama za uendeshaji wa serikali (government administrative costs).

Sijui wa wachumi wa serikali hii wana mtazamo gani, ama walikuwa na lao jambo juu ya kukataa serikali tatu, ila walitumia kigezo cha gharama kubwa za uendeshaji wa serikali.

Katika ongezeko hilo tunahitaji mkuu wa mkoa, mkurugenzi wa mkoa, RPC, RCO, RAS na wengine wengi.
Wilayani tutahitaji DC, DAS, OCD, na wengine wengi.

Duuh! Wachumi wetu mmechemka katika hili.
 
Naeza sema hapo kuna gharama ila usilinganishe kabisa na serekali kuzifanya 3. Unajua nini serikali utakua na viongozi wakuu namtaja mmoja tu RAIS huyu gharama zake za kuishi ni mara 10 ya hizo gharama zilizopo si unamuona mstaafu mtarajiwa (Yeye + familia yake)
 
Masikini John Mnyika atabakia tu Ufipa ubunge ndiyo basi tena ndiyo maana alikuwa mkali kweli bungeni anafanya fujo si alikuwa anasema JK dhaifu tuone sasa.

Daah jamani Mimi nipo nyuma kidogo,, naomba kujua Jonh mnyika anaathirika vipii
 
Last edited by a moderator:
Kuanzisha mikoa mipya ni kuhalalisha matumizi mabaya ya pesa, Serikali yetu ni masikini lkn inapenda kutumia zaidi kuliko mapato iliyonayo na kuliko hata wafadhili wake.

Vv
 
mtoa mada hapo kwenye manispaa ni halmashauri za miji, huwezi kutoka hatua ya mamlaka ya mji mdogo kwenda hatua ya halmashauri ya manispaa, lazima upitie hatua ya halamshauri ya mji kwanza.
 
Naomba anayejua hii wilaya iko mkoa gani atueleze naamini watu wengi hawajui iliko.
 
Kwani pia Chama cha Mapinduzi maana yake ni nini? Kinapindua nini?. Sikikebei na ninakipenda ila maana yake bado sijajua. Na pia Tanganyika sijui kama bado lipo ili neno. Ila naona wanalitumia Tanzania Bara???????
 
katavi upande wa ziwa tanganyikaa

Mbona maeneo hayo ya upande Wa Tanganyika kama yalibaki mkoa Wa rukwa,kama sikosei
Kilando,ikola na kalema ndo maeneo yanapakana na ziwa Tanganyika kwa upande huo Wa kusini magharibi na yako rukwa
 
Back
Top Bottom