BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Serikali yasikia kilio cha wanafunzi wa vyuo
Veronica Mheta
Daily News; Friday,November 21, 2008 @20:21
Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya migomo katika vyuo vya elimu ya juu hasa vya umma, Serikali imeamua kuunda kamati kupitia na kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha utekelezaji wa Sera ya Uchangiaji wa Elimu ya Juu.
Kamati hiyo inajumuisha wajumbe saba ambao wanatoka katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mwanafunzi mmoja kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), mwanafunzi mmoja kutoka Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na wataalamu kutoka Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).
Hayo yalisema jana Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Gaudentia Kabaka wakati alipokuwa akitoa tamko la serikali kuhusu kufungwa kwa vyuo vikuu vya umma. Kabaka alisema si rahisi kurekebisha sera ya uchangiaji wa elimu kwa mara moja, ni lazima mchakato ufanyike kisha ujadiliwe na wataalamu mbalimbali na kupelekwa bungeni kujadiliwa tena na hatimaye sera iweze kubadilishwa.
Lakini huu ni mchakato na hatua hii inachukua muda, alisema Kabaka. Aliongeza kuwa sera ya uchangiaji inalenga kutumia rasilimali na fedha kidogo za serikali ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kupata elimu ya juu. Alisema hivyo si busara kwa serikali kwa sasa kuwalipia wanafunzi asilimia 100 kama wanavyotaka hata kwa wale wanafunzi wanaotoka kwenye familia zenye uwezo.
Wanafunzi wa vyuo wamelazimika kugoma kuingia madarasani kutokana na kugomea sera ya uchangiaji wanayodai kuwa ina upungufu mwingi na kwamba haiwatendei haki wanafunzi hasa wanaotoka katika familia za watu ambao hawana uwezo wa kifedha. Wanafunzi hao wanadai baadhi ya wanafunzi wanaotoka familia moja wanapewa madaraja tofauti ya mikopo, hali inayoonyesha kuwa bodi ya mikopo haiko makini wakati wa kuchambua vigezo vya kutoa mikopo hiyo.
Sababu hizo ndizo zimesababisha wanafunzi hao kugoma kwani wengi wao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kulipa ada wanayotakiwa kuchangia baada ya kupewa mkopo. Kwa upande wake, Kabaka alisema bajeti ya mwaka 2008/2009 ni Sh bilioni 117, ambazo zinatosheleza wanafunzi 42,000 tu ambao wangeweza kukopeshwa kama serikali ingekuwa inatoa asilimia 100.
Lakini alisema kwa sasa wanafunzi 60,000 wapo vyuoni. Kuwapatia wanafunzi 60,000 mkopo wa asilimia 100 kungehitaji kiasi cha Sh bilioni 163.7 ambazo serikali haina uwezo wa kuzipata fedha. Kabaka alisema hivi sasa kila chuo kipo kwenye mchakato wa kuwabaini wanafunzi wanaokubaliana na sera ya uchangiaji wa elimu ili waweze kurudi vyuoni kwa kutumia sheria na taratibu zilizowekwa na vyuo.
Alisisitiza kuwa wanafunzi watakaokubaliana na sera ya uchangiaji wa elimu ndio wataoweza kuingia madarasani kusoma; lakini wanafunzi ambao hawatakubaliana na sera hiyo wataendelea kukaa nyumbani hadi hapo watakapokubali wenyewe.
Kubadilisha sera ya uchangiaji si kwa haraka kama wanavyodai wanafunzi, kunahitaji muda na Bunge kupitia marekebisho hayo hivyo wanafunzi watakaokubaliana na sera ya uchangiaji wa elimu ndio wataweza kurudi vyuoni endapo wasipokubaliana nayo wataendelea kukaa nyumbani kwao hadi hapo watakapoamua kuikubaliana nayo.
Pia Kabaka alisema gharama inayotozwa na vyuo vikuu vya umma siyo halisi na serikali inachangia gharama kwa kiasi kikubwa na kueleza kuwa gharama halisi ya kozi ya udaktari wa binadamu kwa Chuo Kikuu cha Muhimbili ni Sh milioni 4.3 lakini mwanafunzi hulipa Sh milioni 1.0 kwa mwaka.
Pia ada halisi kwa kozi ya udaktari wa Tiba ya Wanyama, Chuo Kikuu cha Sokoine ni Sh milioni 32 kwa mwaka; lakini mwanafunzi hulipa Sh milioni 1.2 na kwa upande wa Shahada ya Biashara, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam gharama halisi ni Sh milioni tatu ila mwanafunzi analipa Sh milioni 1.25.
Hadi sasa wanafunzi wa vyuo vikuu saba wamerudishwa nyumbani kwa muda usiojulikana kwa madai ya kutaka sera ya uchangiaji wa gharama za elimu ya juu ifutwe au kufanyiwa marekebisho ili wanafunzi wote wapewe mikopo kwa asilimia 100 ambapo chanzo chake ni wanafunzi hao kuendelea na migomo hata baada ya uongozi wa vyuo kuasihi wasitishe migomo hiyo ilishindikana.
Akizungumzia hasara inayoipata serikali kutokana na migomo hiyo, Kabaka alisema wanasubiri takwimu sahihi toka vyuo mbalimbali vilivyogoma ili kujua hasara inayoendelea kuipata serikali juu ya migomo hiyo na kusisitiza kuwa migomo hiyo imesababisha wanafunzi wanaohitaji elimu kuikosa kwa wakati unaotakiwa.