Serikali ya Tanzania yaridhia utoaji mimba

sithani kama utoaji wa mimba kihalali utapunguza watoto wa mitaani,kuna nchi nyingi tu waruhusu kutoa mimba lakini bado kuna watoto wa mitaani wengi tu .nikupatie mfano Marekani kuna watoto wengi tu wa mitaani lakini wale watoto wanatunzwa kwenye mashiriaka ya dini,kwa hivyo hawaonekani mtaani,hata hivyo bado kuna mitaa ambayo ukienda bado watoto wa mitaani wapo .Angalia Afrika kusini wameruhusu lakini bado watoto wa mitaani wanazidi kuongezeka,bado kuruhusu kutoa mimba hakutaondoa tatizo la watoto wa mitaani ,NAOMBA NIKUPE KAZI MOJA YA KUFANYA UCHUNGUZI KWAMBA WATOTO WA MITAANI WANATOKA WAPI?Kwamfano niliwahi kuwauliza wato fulani mtaani huku bongo ,lakini wengi wao walisema walikua kwenye famillia lakini mmoja alisema baada ya baba yake kufukuzwa kazi hela ya kwenda shuleni illikosekana na akaacha kwenda shule hadi akamua kuanza kuzurura mtaani .wengine walisema baada ya baba na mama kugombana na kkuachana nipo walipoaanza kuzurura mtaa,,wngine walisema babazao walikufa na vitu kama hivyo ,NAWE JARIBU KUTAFUTA MUDA UFANYE UTFITI KIDOGO HALAFU UANGALIE,Maisha yanakua magumu ndio mana unaona watoto wanaongezeka mtaani,kuruhusu kutoa mimba sio jawabu la kupunguza watoto wa mitaani ,PILI KUTOA MIMBA NI KUFANYA MAUAJI KUBALI USIKUBALI UKWELI UNABAKIA PALEPALE ,Ni sawa tu nakusema mtu huyu simtaki kwahivyo unaamua kumuua ,kuna maendeleo lakini sio kuruhusu kutoa mimba ,NASEMA TENA KUTOA MIMBA NI KUFANYA MAUAJI ,UNAMNYIMA MTOTO HAKI YAKE YA KUZALIWA NA KULISHI KAMA WEWE ,TUSIZUNGUMZE TU TUANGALIE UKWELI UKO WAPI?
 
Kama kweli tunafuta mifumo ya demokrasi ya kweli basi na mtu ana uhuru kwa kufanya mambo yake kwa huru. Leo katika Kampus nyingi za vyuo America wana ruhusu kutoa mimba na pia kama tunakubali yalio yao basi na haya inatupaswa kufanya hivyo. Tunaweza kufanya utoaji mimba ukawa legalize kwa wakati pale mjamzito anakuwa na matatizo lakini kuua watoto kinyume na sheria za Mungu na Neno Lake na siyo vingine, Lakini kama mtu anaona kuwa ana uhuru wa kutoa mimba apewe elimu hiyo itapunguza sana watu kupata matatizo kama haya bwana
 
Abortions in the first stage of pregnancy should be completely by choice, though consultation and adequate education should be provided, and a formal recommendation to carry the pregnancy should be issued.

Abortions in the second stage of pregnancy should only be done by the prescription from a qualified doctor and for medical reasons. Abortion in this stage should also be allowed if the pregnancy was the result of a rape.

In the third stage, an abortion should be strictly allowed for medical resons ONLY, the most prominent of which are the threat of death for the mother or baby.

Yes, i know that many Tanzanian will disagree with what i have said, but to the few that do agree, please comment on this thread and voice your support. To those that disagree i urge the same, although i can't promise that i will give your retorts any attention as i do not fancy debating with a person who has an empty head.

Don't dump your religion, change it. Fight for what is right.

It is OK IF and only IF it is done for the medical reason(s). Kwamba maisha ya mama yanahatarishwa na uwepo wa hiyo mimba. Lakini siyo jitu limefanya ngono halafu linaogopa kunyonyesha likatoe mimba...Nooooooooooo... Au mmekwaruzana unaamua/mnaamua mkatoe..........Noooooooo.
 
Nyie mnaopinga abortion sasa sisi tuliooa na hatuna huwezo wa kuwatunza watoto wote ambao tunauwezo wa kuwazaa, Kumbuka mayai kwa wastani yanafika mpaka 400 yaani mama anaweza kupata hedhi mara 400. watoto mpaka 20. Condoms na mipango mingine ya uzazi dini wanakataza tufanyeje?tusishiriki tendo la ndoa?. Au tuzae tu hata tusipowatunza?
kama mimba yangu ingetolewa ningekwepo? je hii ni hoja kweli kwa sasa?je nisingekwepo Tanzania isingekwepo?.Ni mpaka baada ya wk 24 ndipo mtoto anaanza kuwa na viungo. kabla ya hapo ni Damu tu hata siyo mtoto.kwaiyo msiseme mtu anaua.
 
Nyie mnaopinga abortion sasa sisi tuliooa na hatuna huwezo wa kuwatunza watoto wote ambao tunauwezo wa kuwazaa, Kumbuka mayai kwa wastani yanafika mpaka 400 yaani mama anaweza kupata hedhi mara 400. watoto mpaka 20. Condoms na mipango mingine ya uzazi dini wanakataza tufanyeje?tusishiriki tendo la ndoa?. Au tuzae tu hata tusipowatunza?
kama mimba yangu ingetolewa ningekwepo? je hii ni hoja kweli kwa sasa?je nisingekwepo Tanzania isingekwepo?.Ni mpaka baada ya wk 24 ndipo mtoto anaanza kuwa na viungo. kabla ya hapo ni Damu tu hata siyo mtoto.kwaiyo msiseme mtu anaua.

Uhai wa mtu siyo umri. Hata dakika ya kwanza baada ya mimba kutunga ni mtu huyo..!!! Hizo zote ni stage tu........ Zaigoti (mimba), mtoto mchanga, kijana, mtu wa makamo, mzee......... zote hizo ni stage za mtu. Ukimuuwa akiwa kwenye hatua yoyote ile katika hizo, wewe ni muuwaji tu.
 
Tumekubali kununuliwa kwa kila kitu sasa mambo kama haya wakati yanakuja Tanzania lazima tujuhoji, Lakini Dini ndio zenye maamuzi ya kufanya hata ndio zenye wajibu kwa kukemia na kuhubiri makanisani na kuona mambo haya hayaendelei hata siku moja, Kama Dini zikinyamaza basi wao watafanya watakavyo. Tunapokea Misaada toka kwa kwa hiyo hata masuala ya ajabu watatupelekea kufanya hivyo
 
Serikali yaridhia utoaji mimba
* PRO-LIFE yapinga, yamwandikia Kikwete

na Joseph Sabinus

Tanzania Daima~Sauti ya watu

SERIKALI imetia saini kuridhia itifaki za haki za wanawake, ikiwemo ya kuruhusu utoaji mimba nchini.

Tanzania imeridhia mkataba huo, huku madhehebu mbalimbali ya dini yakipiga marufuku utoaji mimba, kwani ni kinyume cha mafundisho ya dini.


Itifaki hiyo ambayo inasubiri kutungiwa sheria bungeni ili ianze kutekelezwa, imo katika Mkataba wa Haki za Binadamu na Haki za Wanawake barani Afrika na Itifaki ya Maputo.

Itifaki ya Maputo inazipa wajibu nchi wanachama kuhakikisha kuwa, zinalinda na kuboresha afya za wanawake, hususan afya ya uzazi.

Itifaki hiyo kwa mujibu wa uchunguzi, inaainisha haki mbalimbali za mwanamke, ikiwa pamoja na haki ya kuamua kuzaa au kutozaa, haki ya kuamua kupata watoto na nafasi ya mtoto mmoja hadi mwingine, pamoja na haki ya kuchagua njia ya uzazi wa mpango, ikiwemo kutoa mimba.

Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, Philip Marmo, alithibitisha kuridhia kwa itifaki hiyo katika barua yake yenye Kumb. Na. I/CFC.188/444/01 ya Januari 30 mwaka huu, kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Uhai (PRO-LIFE), Tanzania, Emil Hagamu, aliyeiandikia barua serikali kuhoji uhalali wa Tanzania kuridhia itifaki hiyo.

Katika barua hiyo, Hagamu alimwomba Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuingilia kati na kuzuia haraka mauaji ya watoto yanayoweza kutokea endapo Bunge litapitisha sheria ya utoaji mimba.

Akifafanua kuhusu kuridhia kwa itifaki hiyo, Waziri Marmo katika barua yake ya majibu kwa PRO-LIFE ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, alisema Itifaki ya Haki za watu na Haki za Wanawake Barani Afrika, Ibara ya 14, kipengele cha (2) C, kinasema:

“Kwa kuangalia maudhui ya vipengele hivi kwa ujumla ni kweli inatoa tafsiri sahihi ya kuridhia utoaji mimba ili kukidhi vigezo kama inavyojieleza, ambavyo ni kwa mimba iliyosababishwa na shambulio la aibu kama vile kubakwa au kwa mimba inayohatarisha afya ya mwili na akili ya mama au uhai wa mtoto.”

Akirejea barua ya PRO-LIFE, Tanzania yenye kumbukumbu namba PLT/C-A/2009 ya Januari 5, mwaka huu, Waziri Marmo alikiri kuwa kweli Tanzania imeridhia itifaki hizo, lakini bado hazijatungiwa sheria.

“Ni kweli Tanzania iliziwekea sahihi na kuridhia itifaki za Haki za Wanawake katika Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Haki za Wanawake barani Afrika na Itifaki ya Maputo,” alisema.

Waziri Marmo katika barua hiyo kwa Mkurugenzi wa PRO-LIFE, ambaye pia ni Mratibu wa Human Life International (HLI) Kanda ya Tanzania, alisema japo Tanzania imeridhia itifaki hizo mbili, bado hakuna sheria iliyotungwa kusimamia au kuruhusu utoaji mimba.

“Taratibu nchini Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine ni kwamba, itifaki na mikataba ya kimataifa, haiwezi kuwa sheria ya nchi hadi zitakapotungiwa sheria za Bunge.

“Isitoshe, lugha zinazotumika katika itifaki mbalimbali zinakuwa za jumla sana na tafsiri yake inaweza kupotoshwa kwa urahisi ikifanywa bila kufuata tafsiri ya vyombo husika vilivyopewa mamlaka ya kutoa tafsiri ya maana ya miandiko katika sheria ambayo hapa kwetu ni Mahakama,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Waziri Marmo alifafanua kuwa Tanzania imeridhia itifaki hiyo kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Hata hivyo alisema mchakato wa kutungia sheria bado unafanyiwa kazi ili kujua kama sheria hiyo ni muhimu kwa sasa nchini.

“Kuridhia ni suala jingine, lakini tujiulize tuna mahitaji hayo kwa sasa? Ni sawa na kuwa na msitu wa miti mingi, halafu unajiuliza, je, nahitaji kupanda miti mipya kwa sasa?

“Kwa hiyo niseme tu kwamba ni kweli serikali imeridhia kuingia na imesaini mkataba huo, lakini mchakato wa kupitisha sheria bado unafanyiwa kazi,” alisema Waziri Marmo.


Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kupata barua ya ufafanuzi kutoka kwa Waziri Marmo, Hagamu alisema PRO-LIFE, Tanzania iliwaomba Waziri Mkuu na Spika wa Bunge, kumshauri Rais na wabunge kuwa makini ili wasiruhusu kupitishwa kwa sheria hiyo inayolenga kutekeleza maamuzi ya Itifaki ya Maputo (Maputo Protocol) yaliyopitishwa miaka miwili iliyopita.

Akifurahia tamko hilo la serikali kuhusu kutoruhusu au kutunga sheria ya kuhalalisha utoaji mimba, Hagamu alisema utekelezaji wa Makubaliano ya Maputo yanayozilazimisha nchi zilizosaini kuridhia kuwapo kwa sheria hiyo, kunamaanisha kuruhusu umwagaji damu kwa kuwafanyia mauaji watoto ambao hawajazaliwa.

Alisema endapo sheria hiyo itapitishwa, Watanzania wajiandae kushuhudia watoto ambao ni taifa la kesho, wakiangamizwa bila sababu za msingi huku wanawake wakiteseka kutokana na madhara ya utoaji mimba.

“Utoaji mimba haujawahi kuleta manufaa yoyote katika nchi zilizowahi kupitisha sheria hiyo... Inabidi serikali na viongozi wote watambue wajibu mkubwa walio nao katika kulinda maisha ya watu wao tangu wakiwa tumboni, wakizaliwa, wakiwa vijana na hata wanapozeeka,” alisema Hagamu.

“Kwa kuwa haki ya mwanamke haipatikani kwa kumuua mtoto wake aliye tumboni, bali kwa kulinda hadhi yake ya umama, tunaitaka serikali kuachana kabisa na wazo la kutaka kuleta sheria hii ya mauaji kwa watu wasio na hatia wala uwezo wa kujitetea,” alisema Hagamu.

Tanzania ilisaini itifaki hiyo Novemba 5, 2003; Bunge likaridhia Machi 3, 2007 na rais kutia saini Mei 7, mwaka huohuo.


Kati ya nchi 53 za Umoja wa Afrika, nchi 45 zimesaini itifaki hiyo na 25 tayari zimeridhia kupitia mabunge na Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo 25.

tunaweza tuka ambiwa na ndoa za jinsia moja ruksa, hakuna cha bure dunia hii, kutegemea vya watu kunasabisha utumwa
 
Nyie mnaopinga abortion sasa sisi tuliooa na hatuna huwezo wa kuwatunza watoto wote ambao tunauwezo wa kuwazaa, Kumbuka mayai kwa wastani yanafika mpaka 400 yaani mama anaweza kupata hedhi mara 400. watoto mpaka 20. Condoms na mipango mingine ya uzazi dini wanakataza tufanyeje?tusishiriki tendo la ndoa?. Au tuzae tu hata tusipowatunza?
kama mimba yangu ingetolewa ningekwepo? je hii ni hoja kweli kwa sasa?je nisingekwepo Tanzania isingekwepo?.Ni mpaka baada ya wk 24 ndipo mtoto anaanza kuwa na viungo. kabla ya hapo ni Damu tu hata siyo mtoto.kwaiyo msiseme mtu anaua.


Hoja zake zina uzito lakini mwisho wa yote uamuzi anafanya mtu mwenyewe. Binafsi ningependa mtu awe huru kuamua. Lakini maamuzi ya hatari kama haya yasiruhusiwe kabisa. Hebu soma hizi data toka Kagera na Temeke
Of the 278 women admitted with alleged miscarriage in Kagera Regiona Hospital (KRH), 173 (62%) stated they had had an unsafe induced
abortion. The same applied for 296 (63%) of the 473 women admitted with alleged miscarriage in Temeke Municipa Hospital (TMH). In both settings the women who had an unsafe induced absortion were characterised by being aged 24 years or below, being single and not having delivered previously

Report kamili ya utafiti huo iko hapo, anayependa aisome!
 

Attachments

  • Abortin in Tz.pdf
    66.3 KB · Views: 84
Napinga utoaji mimba. Kama mwanafunzi amepata ujauzito aruhusiwe kuingia darasani na akijifungua apewe muda wa kulea mtoto wake for a year halafu arudishwe shuleni kuendelea. Yaani kama alikuwa la sita basi arudie darasa aliloachia kabla hajajifungua. Kuua no no no no no with all my vains.
 
Hakuna mtu mwenye haki ya kutoa mimba. Mtu huyo, awe mwanaume au mwanamke, hakuna mwenye haki ya kuondoa uhai wa binadamu mwingine. Utaoji mimba ni makosa na ninaupinga na nitaupinga kwa nguvu zangu zote. Natamani watoaji mimba wote mama zao wangezitoa mimba zao...nyambaaaf kabisa. Mijitu inajitolea tu mimba unadhani inaenda haja kubwa....hivi wao mama zao wangezitoa hizo mimba zao leo hii wangekuwepo kweli hao watu? Na kwa nini mtu umnyime binadamu mwingine fursa ya kuishi na kuonja raha na karaha za dunia hii kama ulivyopewa hiyo fursa wewe na wazazi wako? Kwenye utoaji mimba hakuna cha haki ya mwanamke wala nini. Haki pekee iliyopo ni haki ya kiumbe hicho kilicho defenseless kulindwa. Hiyo ndio haki pekee.

I oppose abortion and YES, I am against the death penalty also...now what?

Seriously, you sound like Rush Limbaugh.
 
I like Rush. He doesn't mince his words and doesn't care about what people say or think of him. Abortion is wrong in every kind of way. Do you support it?

I don't support abortion, but also I don't want to be a hypocrite. Many Tanzanians enjoy unprotected sex which is the major cause of unwanted pregnancy and sexual transmitted diseases. Hivyo kama nitapinga abortion ni lazima nikubali aina fulani ya sex education ambayo itahimiza watu ku-practise safe sex. Cha ajabu ni kuwa wengi wanaopinga abortion ndio haohao wanaopinga sex education.
 
I don't support abortion, but also I don't want to be a hypocrite. Many Tanzanians enjoy unprotected sex which is the major cause of unwanted pregnancy and sexual transmitted diseases. Hivyo kama nitapinga abortion ni lazima nikubali aina fulani ya sex education ambayo itahimiza watu ku-practise safe sex. Cha ajabu ni kuwa wengi wanaopinga abortion ndio haohao wanaopinga sex education.

Sex education ni muhimu na mimi ninaiunga mkono. Ni vyema kuwaonya watu kuwa wasipokuwa waangalifu watakamata magonjwa ya zinaa na kuoza huko chini. Sasa nani anataka kuoza na kuanza kutoa usaha huko chini? Hakika sio mimi na nadhani si wewe pia. Au nimekosea?
 
I like Rush. He doesn't mince his words and doesn't care about what people say or think of him. Abortion is wrong in every kind of way. Do you support it?

I do. I support the right of a woman to choose. It is better and more humane than dumping babies in the garbage dump!

Amandla......
 
I do. I support the right of a woman to choose. It is better and more humane than dumping babies in the garbage dump!

Amandla......

You are wrong and you are going to hell for this one (jk). Fundi, abortion and dumping babies in dumpsters are both wrong. You can't make a moral equivalency and say one of them is more humane than the other.

The only humane thing to do is to birth the child and give it up for adoption. Killing it before it comes out of the womb is wrong and dumping it and leaving it to die after birth is also wrong. Giving up babies for adoption is not the best thing but it is highly encouraged over abortion and dumping.

No human being with a heart would do that to a defenseless human being, born or unborn. And if you had a soul you wouldn't support abortion. How can you say you support ending the life of another human being? How could you? You have no heart. Shame on you.

NB: No human being should choose to end the life of another human being. The only sensible and humane choice is to choose life not death.
 
Sex education ni muhimu na mimi ninaiunga mkono. Ni vyema kuwaonya watu kuwa wasipokuwa waangalifu watakamata magonjwa ya zinaa na kuoza huko chini. Sasa nani anataka kuoza na kuanza kutoa usaha huko chini? Hakika sio mimi na nadhani si wewe pia. Au nimekosea?

Kuna watu wengi ambao kwa sababu za imani ya kidini wanapinga vyote. Wanapinga sex education na wanapinga watu kufanya abortion.

Nilipokuwa boarding school kwa bahati mbaya umri ulikuwa mdogo, lakini vijana wengi walikuwa wanawashawishi girl friends zao kutoa mimba. Au wasichana wenyewe walihamua kutoa mimba. Na kulikuwa na instance ya msichana nilikuwa nakaa naye kwenye dawati kufariki kwa kutoa mimba.

Sheria za sasa za shule zilivyo kali, utoaji wa mimba ni horrifying experience. Lakini haya yangeepukwa kama sex education ingetiliwa mkazo.
 
Bora kufanya legal kwa sababu hata wakikataza wataendelea tuu kwa njia za uchochoroni,hayo mambo waachiwe wanawake na madaktari wao na wapenzi wao ndio waamue lakini kuweka sheria kukataza naona ni kupoteza muda tuu na msilete sababu za dini humu maana sio kila mtu anaamini mungu na sheria zetu hazijawekwa kufuata dini yeyote,kama wewe hutaki abortionmkwa ajiri ya dini yako then fine lakini usilazimishe wengine kutokana na dini yako!
 
Back
Top Bottom