USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 9,896
- 22,666
SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR,
WIZARA YA AFYA.
TAARIFA YA TAHADHARI KWA UMMA KUHUSU MAJI YA CHEMCHEM YA ILIYOPO PEMBENI MWA BAHARI YA HINDI KATIKA SHEHIA YA MSUKA, MASHARIKI, WILAYA YA MICHEWENI MKOA WA KASKAZINI PEMBA
TAREHE: 05/04/2023
Ndugu wananchi, Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa za kuwepo Chemchem inayotoa maji ambayo ukinywa maji hayo ni tiba ya magonjwa mbali mbali.
Maji haya yanapatikana katika chemchem iliyopo ndani ya bahari katika Shehia ya Msuka Mashariki Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ndugu wananchi, wamejitokeza watu mbali mbali kutoka Kisiwa cha Pemba na nje ya Kisiwa hicho ambao hufika kwa wingi katika eneo lenye chemchem hiyo na kuchukua maji hayo katika vyombo tofauti ikiwemo madumu, chupa na ndoo na kunywa maji hayo wakiamini kwamba maji hayo ni tiba ya magonjwa mbali mbali.
Ndugu wananchi, baada kupata taarifa hiyo, Wizara ya Afya ilituma wataalamu wake kwenda kuchukua sampuli ya maji hayo kwa lengo la kuyafanyia uchunguzi ili iweze kuthibisha kwamba maji hayo ni tiba kama inavyoaminika katika jamii.
Sampuli zilizochuliwa zilipelekwa kwa Mkenia Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya uchunguzi wa maabara ili tuweze kuthibisha madai ya kuwa maji haya ni tiba kwa magonjwa mbali mbali na yapo salama kunywewa.
Ndugu wananchi, Baada ya uchunguzi na uchambuzi wa kina wa maji hayo, uchunguzi umebainisha mambo yafuatayo;-
1. Uwepo wa vimelea vinavyosababisha magonjwa ya kuharisha (bacteria wa E. Coli) wa idadi kubwa kati ya mia mbili na ishirini hadi elfu moja na mia nane kwa kila lita mia moja (220 hadi 1800 kwa kila lita 100), kwa kawaida maji ya kunywa hayatakiwi kuwepo na hata kimelea kimoja cha aina hiyo.
2. Pia uchunguzi umebaini kuwepo vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa kuharisha aina ya “Coliforms” wa zaidi ya elfu moja mia nane kwa kila lita moja za maji (1800 kwa kila lita 100). Kwa kawaida vimeilea hivi vinahitajika viwemo kwenye maji ya kunywa, lakini isiwe zaidi ya watatu kwa lita mia moja kwa kila lita mia moja ya maji.
3. Uchunguzi huu vile vile umebaini uwepo wa Chloride kwa kiwango kikubwa ambapo wataalamu wetu wemebaini kiasi cha upimo wa kuanzia elfu moja mia nne na tisiini milligram kwa kila lita hadi mpaka elfu mbili na khamsini na tisa milligram kwa lita moja (1490.88 mg/L hadi 2059.36 mg/L). kiwango kinachokubalika ni kipimo kisichozidi mia mbili na khamsini milligram kwa kila lita moja (250 mg/L).
4. Kiwango cha Chumvi chumvi (Salinity) kimebainika kwa kiwango cha kupima ukali wa chumvi cha baina ya mbili nukta nane na tatu nukta nane (2.827 hadi 3.827 psu) ambapo ni zaidi ya kiwango kinachokubalika katika maji ya kunywa cha sufuri, (0 psu).
Ndugu wananchi, Kutokana na matokeo hayo yatuthibitishia kwamba maji haya yamechafuliwa na kinyeshi cha viumbe hai na pia kuna kiwango kikubwa cha Kemikali ambazo sio salama katika mwili wa binadamu. Kwa maana hio maji haya sio salama kwa kunywa na kama tukiendekea kuyatumia yanaweza kuathiri Afya zetu na kupelekea matatizo ya kiafya yafuatayo:-
1. Magonjwa ya kuharisha ikiwemo Kipindupindu, kutapika na kupoteza maji mengi mwilini.
2. Kupata maumivu makali ya tumbo na baadae unaweza kupata vidonda vya tumbo hapo baadae.
Ndugu wananchi, Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba Wazanzibari wenzangu kwamba taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii hapa nchi kwamba maji yanayopatikana katika Chemchem iliyopo katika Bahari ya Hindi katika Shehia ya Msuka Mashariki, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba hayawezi kutibu ugonjwa wowote na tuzipuuze taarifa hizi kwa hazina ukweli wowote.
Ndugu wananchi, Aidha, napenda niwasihi wananchi wote kwamba mtu yoyote mwenye matatizo ya kiafya afike katika Kituo cha Afya au Hospitali iliyokaribu kwa ajili uchunguzi na matibabu na tuache kutumia maji haya kama tiba kwani yanaweza kutuletea athari zaidi katika Afya zetu.
Ndugu wananchi, Mwisho kabisa nitoe wito wangu kwa Wanzanzibari wenzangu kwa tuache kuyatumia maji haya tukiamini ni tiba ya magonjwa mbali mbali kwani athari yake inaweza kuwa kubwa na kusabisha matatizo ya kichumi na kijamii.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
NASSOR AHMED MAZRUI,
WAZIRI WA AFYA,
ZANZIBAR.