Serikali yaondoa katazo kwa wavuvi la kutokuvua samaki wazazi kuanzia sentimita 85

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Serikali imeondoa katazo la kutokuvua samaki wazazi kuanzia sentimita 85 hivyo kuanzia kesho wavuvi watavua samaki hao bila kukamatwa.

Aliyetangaza kuondoa katazo hilo katika kijiji cha Kikumbaitale wilayani Chato mkoani Geita ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, wakati akizindua ushirika wa chama wavuvi wa mwalo wa Kikumbaitale na kuwakabidhi hundi ya shilingi milioni tano ikiwa ni kuwawezesha kukuza mtaji.

Hatua hiyo imefuatia matokeo ya utafiti uliofanyika na kubaini nchi za Kenya na Uganda hazikatazi samaki wazazi kuvuliwa, kwakuwa wakipelekwa sokoni wanapata wateja, huku wafanyabiashara wa nchini wanapopeleka samaki zao katika nchi hizo hukosa wateja.

"Wavuvi Serikali imesikia kilio chenu cha muda mrefu, hivyo imeruhusu uvuaji wa samaki kuanzia sentimita 85 na kuendelea, lakini bado mchakato unaendelea wa kuangalia namna gani ya kuruhusu samaki aina ya ngele, gogogo na furu na kuwekwa kwenye utaratibu wa sheria na kanuni", alisema Ulega

FB_IMG_1557734787200.jpeg
IMG_20190513_111851_027.jpeg
 
Walikataza kabla ya tafiti, waondoa katazo baada ya tafiti..Ama kweli Kupanga ni kuchagua..!
 
Juzi tulisikia tra hawatafungia wenye maduka tena....naona makosa yanaenda yakirekebishwa... Tunaomba na bunge live na Local channels nazo zifunguliwe maana pale kuna revenue nyingi inapotea
 
Tra walisema juzi hawatafunga maduka.... Naona tunaendelea kujirekebisha bado bunge live, bureau de change na local channels zifunguliwe twapoteza revenue huko
 
Serikali imeondoa katazo la kutokuvua samaki wazazi kuanzia sentimita 85 hivyo kuanzia kesho wavuvi watavua samaki hao bila kukamatwa.

Aliyetangaza kuondoa katazo hilo katika kijiji cha Kikumbaitale wilayani Chato mkoani Geita ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, wakati akizindua ushirika wa chama wavuvi wa mwalo wa Kikumbaitale na kuwakabidhi hundi ya shilingi milioni tano ikiwa ni kuwawezesha kukuza mtaji.

Hatua hiyo imefuatia matokeo ya utafiti uliofanyika na kubaini nchi za Kenya na Uganda hazikatazi samaki wazazi kuvuliwa, kwakuwa wakipelekwa sokoni wanapata wateja, huku wafanyabiashara wa nchini wanapopeleka samaki zao katika nchi hizo hukosa wateja.

"Wavuvi Serikali imesikia kilio chenu cha muda mrefu, hivyo imeruhusu uvuaji wa samaki kuanzia sentimita 85 na kuendelea, lakini bado mchakato unaendelea wa kuangalia namna gani ya kuruhusu samaki aina ya ngele, gogogo na furu na kuwekwa kwenye utaratibu wa sheria na kanuni", alisema Ulega

View attachment 1095782View attachment 1095783
Wakati mwingine inashangaza! Ilihitaji utafiti kweli kujua hilo ambalo lilikuwa linajulikana na wadau wote wa uvuvi! Mmewaingiza wananchi wetu, wanaotegemea uvuvi kama shughuli zao za kipato, katika umasikini mkubwa. Sasa mnakuja na sababu za utafiti! Aibu kubwa na hasa ukichukulia kauli zulizokuwa zikitamkwa na viongozi wakubwa kabisa wa nchi hii na matendo ya kikatili na kejeli. Inaudhi sana.
 
Back
Top Bottom