Serikali yamfungia Msanii kwa kuweka picha ya utupu Mtandaoni, na BASATA yawataka watayarishaji wa Muziki wajisajili

Serikali kupitia Naibu waziri wa habari na utamaduni na michezo Juliana Shonza imetangaza kumfungia miezi 6 Msanii wa filamu na muziki, Suzan Michael maarufu Pretty Kind kwa kuweka picha za utupu katika mtandao ya kijamii
-
Gigy Money atakiwa kufika Ofisini kwa Naibu Waziri wa Habari baada ya kukaidi ujumbe aliotumiwa
-
Pia Mwanadada Jane Rimoy maarufu kwa jina la Sanchi ametakiwa kufika ofisini kwa Naibu Waziri huyo mara moja kutokana na kuchapisha mitandaoni picha zisizo na maadili.

=======

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema kuwa, serikali inafuatilia kwa karibu wasanii wote wanaoweka picha za kukosa maadili kwenye mitandao na kuwachukulia hatua.

Shonza ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaama alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari. Agizo hilo la Naibu Waziri ni matokeo ya kauli iliyotolewa na Rais Dkt Magufuli aliyoitoa mjini Dodoma wakati akizungumza na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Rais Magufuli alivitaka vyombo husika kuwachukulia hatua wasanii hasa wa kike ambao wamekuwa wakivaa nguo zinazopelekea kumomonyoka kwa maadili.

Wakati akizungumza hayo Naibu Waziri alitaja majina ya wasanii ambao wameanza kuwachukulia hatua ambapo baadhi wametakiwa kufika ofisini kwake huku mwingine akifungiwa kujihusisha na masuala ya sanaa kwa muda wa miezi sita.

Shonza amemtaka msanii, Jane Rimoy maarufu kwa jina la Sanchi kufika ofisini kwake mara moja kutokana na kuchapisha mitandaoni picha zisizo na maadili.

Mbali na Sanchi, Shonza ametoa maagizo, ”Ninamtaka Msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money kufika ofisini kwangu mara moja sababu alitumiwa ujumbe lakini hakujibu, hivyo ajue kuwa hawezi kushindana na serikali.”

Pia, Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza amemfungia msanii wa filamu na muziki, Suzan Michael maarufu Pretty Kind kujihusisha na shughuli zote za sanaa kwa muda wa miezi sita, kutokana na kuweka picha za utupu katika mtandao ya kijamii.

Wakati huo huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amewasisitiza wamiliki wa studio za kutayarisha kazi za sanaa na waandaji wa kazi za sanaa (Producers) kujisajili katika ofisi za Baraza hilo. Asisitiza, kufanya kazi bila kusajiliwa ni kinyume na sheria.

View attachment 670211
View attachment 670212
View attachment 670213
View attachment 670205
View attachment 670217 View attachment 670206
View attachment 670223
=======

[HASHTAG]#Picha[/HASHTAG] Mwanadada Jane Rimoy maarufu kwa jina la Sanchi ametakiwa kufika ofisini kwa Naibu Waziri huyo mara moja kutokana na kuchapisha mitandaoni picha zisizo na maadili.
View attachment 670271
View attachment 670272
View attachment 670276
View attachment 670277

Ni vilio, masikitiko, majuto mjukuu kuanzia Giggy Money, Sanchi, Agnes, mpaka Pretty Kind...
Hi ni baada ya kufungiwa na BASATA na Wizara husika kwa kukatitaliwa kukaa uchi kwenye Video au kupiga picha za utupu!
Ukiwaona wanavyolia kama ulikuwa hujuwi sababu basi waweza amuwa kufanya maandamano na uchochezi kwa dola!
Kwa kweli kizazi chetu ndipo kilipofikia, kutengeneza maisha kwa kuonyesha UTUPU!
Itabidi tujitazame, kusikitika na kukemea hizi tabia mbaya kama Dola...

Ama kweli Rais wangu Mungu ambariki kwani kabla ya tamko lake hayo yalikuwa yakiendelea bila ya hofu yoyote na waliokuwa wakichukizwa walikuwa wakikemea kimoyo moyo lakini waliokuwa wanafurahishwa ni wengi kama unavyoona comments za wenzetu. God bless our dearest president
 
Serikali kupitia Naibu waziri wa habari na utamaduni na michezo Juliana Shonza imetangaza kumfungia miezi 6 Msanii wa filamu na muziki, Suzan Michael maarufu Pretty Kind kwa kuweka picha za utupu katika mtandao ya kijamii
-
Gigy Money atakiwa kufika Ofisini kwa Naibu Waziri wa Habari baada ya kukaidi ujumbe aliotumiwa
-
Pia Mwanadada Jane Rimoy maarufu kwa jina la Sanchi ametakiwa kufika ofisini kwa Naibu Waziri huyo mara moja kutokana na kuchapisha mitandaoni picha zisizo na maadili.

=======

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema kuwa, serikali inafuatilia kwa karibu wasanii wote wanaoweka picha za kukosa maadili kwenye mitandao na kuwachukulia hatua.

Shonza ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaama alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari. Agizo hilo la Naibu Waziri ni matokeo ya kauli iliyotolewa na Rais Dkt Magufuli aliyoitoa mjini Dodoma wakati akizungumza na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Rais Magufuli alivitaka vyombo husika kuwachukulia hatua wasanii hasa wa kike ambao wamekuwa wakivaa nguo zinazopelekea kumomonyoka kwa maadili.

Wakati akizungumza hayo Naibu Waziri alitaja majina ya wasanii ambao wameanza kuwachukulia hatua ambapo baadhi wametakiwa kufika ofisini kwake huku mwingine akifungiwa kujihusisha na masuala ya sanaa kwa muda wa miezi sita.

Shonza amemtaka msanii, Jane Rimoy maarufu kwa jina la Sanchi kufika ofisini kwake mara moja kutokana na kuchapisha mitandaoni picha zisizo na maadili.

Mbali na Sanchi, Shonza ametoa maagizo, ”Ninamtaka Msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money kufika ofisini kwangu mara moja sababu alitumiwa ujumbe lakini hakujibu, hivyo ajue kuwa hawezi kushindana na serikali.”

Pia, Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza amemfungia msanii wa filamu na muziki, Suzan Michael maarufu Pretty Kind kujihusisha na shughuli zote za sanaa kwa muda wa miezi sita, kutokana na kuweka picha za utupu katika mtandao ya kijamii.

Wakati huo huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amewasisitiza wamiliki wa studio za kutayarisha kazi za sanaa na waandaji wa kazi za sanaa (Producers) kujisajili katika ofisi za Baraza hilo. Asisitiza, kufanya kazi bila kusajiliwa ni kinyume na sheria.

View attachment 670211
View attachment 670212
View attachment 670213
View attachment 670205
View attachment 670217 View attachment 670206
View attachment 670223
=======

[HASHTAG]#Picha[/HASHTAG] Mwanadada Jane Rimoy maarufu kwa jina la Sanchi ametakiwa kufika ofisini kwa Naibu Waziri huyo mara moja kutokana na kuchapisha mitandaoni picha zisizo na maadili.
View attachment 670271
View attachment 670272
View attachment 670276
View attachment 670277

Naitafura hiyo pichu ya uchi mbona haipo
 
Kwa taarifa yako hao wote uliowataja hawakuwa wakila kwa sanaa, wapo mjin kwa kudanga hata wakifungiwa maisha wataishi tu kuna mapedesheeee!
 
Back
Top Bottom