Serikali ya China yaipongeza Yanga

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,741
6,293
Summary

Salamu za China zimetolewa na Balozi wao wa nchini Tanzania Chen Mingjian kupitia ukurasa wake wa Twitter akiwapongeza Yanga kwa kufika hatua hiyo ya kihistoria.

YANGA imeendelea kupokea salamu za pongezi ambapo China nayo imetoa pongezi zake kufuatia timu hiyo kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Sambamba na salamu hizo Balozi Mingjian amewataka Yanga kujitahidi katika mechi za fainali watakapokutana na USM Alger ya Algeria.
Baaada ya salamu hizo naye Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amemshukuru Balozi Mingjian huku akisema hatua hiyo imetokana na jitihada na mapambano ya klabu yao.

"Hii inaonesha namna watu wa Jamhuri ya China mmejawa na utu,uhusiano wa China na Tanzania ni wa kipekee,"ameandika Arafat.

Aidha Arafat amemkaribisha Balozi Mingjian kwa mualiko maalum kwenye mchezo wa kwanza wa fainali utakaopigwa Mei 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga imefuzu fainali baada ya kuwang'oa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-1 wakishinda nyumbani za ugenini

Mwananchi Gazeti
 
Pinga Pinga "Watani" bado wamelala usingizi wa pono, ngoja waje wakuoneshe jinsi gani Utopolo hawafai kwa lolote isipokuwa wao pekee Makolokolo

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom