Ringo Edmund
JF-Expert Member
- May 10, 2010
- 4,879
- 1,125
wadau tuijadili serikali ya ccm hapa ilipofikia.
nani anayebisha kuwa hatupo pale walipofikia waliokuwa wanajenga mnara wa babeli ili kumfikia mungu.
nani asiyeona uwezo wa kiongozi mkuu wa kuujenga mnara uwezo wake,jana akihutubia umoja wa vijana wa watoto wa wajenzi wa mnara alisema,nanukuu chama chetu kinasemwa vibaya na watu.
hapo ndipo alipofikia mjenzi mkuu.
nani alimtuma chenge atuletee magogo(RADA)wakati tulikuwa kwenye msingi?
nani alimtuma mramba udongo(NDEGE YA RAIS)wakati tunatumia mchanga na siment?
ni nani ameruhusu rasilimali za ujenzi wa mnara(MADINI NA WANYAMA) ziibiwe?
kwa nini foreman (RAIS)hatulii saiti?
kwa nini wazee wetu hawasimamii kumwagilia zege?
kwa nini mama zetu(UWT) tuliowapa jukumu la kutupikia ugali kwa ajili ya kazi ngumu wanatupikia uji saa 8?
Je watoto wa wasimamizi wa ujenzi(UVCCM)walioshuhudia na kuwapa wazazi wao sapoti ya kutuletea mkaa wakati tukihitaji siment wataweza kuwageuka baba zao na kuendelea na ujenzi?
Kwa nini vibarua wa ujenzi(WAISLAMU NA WAKRISTO)lugha zinaanza kubadilika,wengine wananawa na wengine wanakoroga zege?
Je huu mnara(TANZANIA)mungu hauhitaji ujengwe?
Je ni wakati wa kuangalia kiwanja tulichokitelekeza(TANGANYIKA) ili kujaribu kujenga mji badala ya mnara?
Je ni wapi walipopata mafunzo wasomi wetu kuwa ukimwagilia zege kwa kutumia pombe(MIKATABA MIBOVU) inakuwa imara zaidi ya maji?
Wadau kuna mengi tunayofanya na tuliyofanya na mpaka sasa kwa mtizamo wangu kuta zina nyufa kibao na kubomoa ni kazi ngumu sana kwa maoni yangu tungewatimua wasimamizi wa ujenzi(CCM)na kuutelekeza mnara(MUUNGANO)na kurudi katika nchi yetu(TANGANYIKA)na mungu atatusamehe.
Haya ni maoni yangu kama mwananchi mzalendo wa nchi,watu wake na rasilimali zake.
karibuni.