Tony Almeda
JF-Expert Member
- Sep 18, 2011
- 397
- 122
Zao la pamba lililokuwa linategemewa sana katika mikoa ya kanda ya ziwa, liko hatarini kutolimwa kabisa kutokana na serikali kuonekana haiwathamini wakulima wa zao hilo na kuwakumbatia wanunuzi.
Kikao kilichofanyika wiki hii baina ya serikali na wanunuzi hao wa pamba, kilionyesha udhaifu wa serikali baada ya kushindwa kufikia muafaka wa bei elekezi, baada ya Wanunuzi hao kung'ang'ania bei ya kuanzia iwe shillingi 450 kwa kilo moja ya pamba isiyochambuliwa, wakati serikali ilikuja na bei ya kuanzia ya shillingi 700 kwa kilo moja ya pamba isiyochambuliwa.
Mwaka 2011 bei ya pamba ilishuka ghafla kutoka shillingi 1400 kwa kilo moja hadi kufikia shillingi 700 kwa kilo na serikali kushindwa kufanya lolote la kuwanusuru wakulima hao wa pamba wakati bei waliipanga wao wenyewe.
Habari kutoka Bariadi zinasema ya kuwa. Kwa kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kuwatetea wakulima wa pamba, Basi watageukia kulima mazao mbadala kama alizeti na choroko kuliko kuumia na wakati huo huo gharama za kulilima zao hilo zikiongezeka maradufu
My take:
Serikali inatakiwa iliangalie kwa umakini hili suala, tusije kutafuta mchawi hili zo pindi litakapokufa,kuna bahadhi ya maeneo hivi sasa hawalimi kabisa au kama wanalima basi ni kidogo sana tofauti na zamani.
Source ni mimi mwenyewe mdau wa pamba