Serikali wanasoma JF?

palalisote

JF-Expert Member
Aug 4, 2010
8,335
1,455
Nitajikita zaidi na maamuzi ya PM Pinda kuwasimamisha Mganga mKuu wa serikali na Katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii, blandina nyoni.

Nanukuu:"

Sababu ya kuwasimamisha watendaji hao ni tuhuma za kuingiza nchini robo tatu ya vifaa bandia vya vipimo vya Ukimwi kutoka Korea Kusini na tuhuma za kuanzisha kampuni ya kusambaza nguo kwa madaktari na kuiingiza kinyemela kampuni ya kufanya usafi ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili"

mwisho wa kunukuu.

Haya yote yalilipotiwa na jf hapa mwishoni mwa mwezi januari yakapuuzwa lakini baada ya ile tume ya bunge kuchunguza imebaini yaleyale yaliyolipotiwa hapa jf.

Mungu awape maisha marefu wanajf.

Naimani watu wengi tunaoingia hapa jamvini tunatamani kuiona nchi yetu kupitia serikali yetu ikiheshimika, ikifanya mambo kwa ajili ya wananchi wake si vinginevyo. Jambo lolote kinyume na matakwa ya wengi, linatunyima usingizi kama si kutusababishia msongo wa mawazo.
Hata kama mimi nawewe tunao uwezo wa kupata mkate wa kila siku, kuna raha gani kula ukashiba wakati ndugu zetu wakipoteza matumaini ya kuishi. Hii ndiyo sababu moja ya wanaJF members kuendelea kuwanyooshea vidole viongozi wanaotanguliza maslahi yao mbele badala ya kuwatumikia wananchi na taifa.
 
Na ndio maana wale wenye vichwa hewa eti wanaitaka serikali ifungie jf na hii inatokana na uovu wao kufumuliwa humu.
 
Kumbe kusimamishwa kwao hakuhusiani na mgomo/madai ya madaktari au hili nalo lilikuwa mojawapo ya tuhuma walizopewa na madk?

Mgongano mwingine wa Mawazo! Mkuu mtu akiamua anakutafuta kokote kule ili mradi uwajibishwe tu. Nadhani Madokta wao walikuwa wanataka mama atoke sasa ikawa ni kazi ya serikali kutafuta jinsi ya kumtoa.
 
leo itv nimemsikia mtangazaji analalama eti ata watoto viongozi wamefeli na wameandikiwa kwenye mitandao ya kijamii..mmmh jf inausika hapa.
 
Mkuu, serikali wanasoma JF aidha direct au indirect kupitia kwa wapambe wake.
Nina sema hivi kutokana na vuguvugu la waheshimiwa kutaka JF ipigwe ban eti inasambaza chuki pamoja na uwongo kwa wananchi, jambo ambalo si kweli!
Majuzi tumeshuhudia kauli ya Mama Lwakatare kule mjengoni Dodoma akitaka JF ifungiwe kwamba anadhalilishwa kupitia hii community Forum. Hiki ni kiashiria (indication) kuwa
hawa wakubwa wako hapa JF wakitumia ID bandia. Kutokana na nature, binadamu uwa hapendi kuambiwa ukweli. JF inasema kweli, ndio maana sampuli ya watu kama Mama Lwaka. wanaichukia JF.
 
Yupo mbabe mmoja serikalini alitaka kubomoa nyumba za watu atakavyo kwa kisingizio cha kufuata sheria, hizo sheria anazodai kutumia tulizichambua hapa JF kwa ustadi mkubwa ninamini wakuu wa nchi huita humu mara kwa mara. Nikapata tetesi toka kwa mmoja wa wasaidizi waliompiga top mbabe huyo " Mkuu huyo alinukuliwa kuwa kumbe wananchi wanajua sheria za barabara hata kumshinda waziri: matokeo yake mbabe huyu akapigwa top kubooa kiholela nyumba za watu bila kuzingatia haki za wananchi zinzpatikana kupitia sheria zingine ama kwa maneno mengine wananchi ambao barabar ziliwafuata wana haki ya kulipwa fidia tofauti kabisa na kauli za awli za mbabe huyo. Big JF!!!
 
Serikali sio tuu wanasoma jf bali wanayafanyia kazi mengi tuu yanayoibuliwa hapa jf. Jana Waziri Mkuu alisema kuhusu kelele mitandaoni japo hakuitaja jf moja kwa moja lakini mtandao unaoogoza kwa kupiga kelele kuhusu maslahi ya taifa ni jf!.

Sisi kama wana jf tunatakiwa kuwa more resiponsible kwenye hoja za msingi zinazoletwa humu tuachane na majibu ya kipuuzi puuzi na matusi ya rejareja yanayotushushia hadhi ya jf!.
 
mwanakijiji nakumbuka sana hili la vifaa vya HIV ulilipigia sana kelele hapa jamvini lakini watu kama kawaida yetu hatukuliona kama ni tatizo maana bongo ni tofauti na ulaya pale utakaponipa majibu tofauti na ukweli na ikajabainika nakushitaki, ila bongo unambiwa tu kipimo kilikosea thats it na issue inaishia pale pale yaani kirahisi rahisi

nadhani ni wakati sasa wa jf kuimarisha jina lake kwa kuwa na check and balance kwa issue zote hata zinazoihusu jf yeyewe wacha watu walipoti ukweli

SWALI hivi pinda alishindwa nini kufanya haya aliyo yafanya jana kuliko kuwatisha madaktari? kwa nini asingelifanya wakati ule ule ambapo angekuwa ameokoa maisha ya watu waliokuwa wakifa?

mabadiliko ya fikra ni muhimu vichwani mwetu watanzania.
 
Nitajikita zaidi na maamuzi ya PM Pinda kuwasimamisha Mganga mKuu wa serikali na Katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii, blandina nyoni.

Nanukuu:"

Sababu ya kuwasimamisha watendaji hao ni tuhuma za kuingiza nchini robo tatu ya vifaa bandia vya vipimo vya Ukimwi kutoka Korea Kusini na tuhuma za kuanzisha kampuni ya kusambaza nguo kwa madaktari na kuiingiza kinyemela kampuni ya kufanya usafi ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili"

mwisho wa kunukuu.

Haya yote yalilipotiwa na jf hapa mwishoni mwa mwezi januari yakapuuzwa lakini baada ya ile tume ya bunge kuchunguza imebaini yaleyale yaliyolipotiwa hapa jf.

Mungu awape maisha marefu wanajf.

duh hapo kwenye vipimo feki hapo si wengi tutakuwa tumeingizwa kingi
 
Serikali sio tuu wanasoma jf bali wanayafanyia kazi mengi tuu yanayoibuliwa hapa jf. Jana Waziri Mkuu alisema kuhusu kelele mitandaoni japo hakuitaja jf moja kwa moja lakini mtandao unaoogoza kwa kupiga kelele kuhusu maslahi ya taifa ni jf!.

Sisi kama wana jf tunatakiwa kuwa more resiponsible kwenye hoja za msingi zinazoletwa humu tuachane na majibu ya kipuuzi puuzi na matusi ya rejareja yanayotushushia hadhi ya jf!.

Litakuwa jambo la busara kama hoja zetu ziwe zenye uhakika na kujiepusha na hoja zisizo na mshiko !
 
Mgongano mwingine wa Mawazo! Mkuu mtu akiamua anakutafuta kokote kule ili mradi uwajibishwe tu. Nadhani Madokta wao walikuwa wanataka mama atoke sasa ikawa ni kazi ya serikali kutafuta jinsi ya kumtoa.

Aksante kimbunga kwa kunielewesha. Ok ila wasiwasi wangu ni ukigeugeu wa serikali yetu. Haikawii kuja na hadithi za hawana makosa tuhuma hizi hazikuwa za kweli! Kisha haoooo wanaendelea kupeta kwa kupewa ulaji mwingine.
 
Back
Top Bottom