Serikali (TAKUKURU) yakamata Tani 4,900 za Sukari iliyofichwa Mbagala na Tabata jijini Dar

Rais Magufuli aache ubabe bhana biashara huria kwan lazma nitoe stock yangu yote? Aboreshe viwanda vya kuzalisha sukar iwe nyng sio kuingilia biashara za watu subir serikali italipa hili km mtataifisha hiyo sukar iwe km zile samak

Ulimsikia alivyoelezea saga ya kesi ya samaki? Ulimsikia alivyosema kuhusu mwanasheria mkuu? Ulisikia alivyokataa kuwalipa wale wa ARV fake? Hivyo sahau kabisa habari hizo za kulipana kwenye serikali hii. Labda baada ya serikali ya awamu ya tano. Serikali inajua watu walikuwa wananufaika katika uagizaji wa sukari. Kuzuia kuagiza sukari kuna mafisadi wameathirika , hivyo wanatumia kila njia kuiyumbisha serikali, na serikali inalijua hilo. Hivyo haya ni mapambano.
 
Kwa watanzania BREAKING NEWS SI HABARI MPASUKO. TASASIRI RAHISI INAWEZA KUWA HANARI MOTOMOTO.AU HABARI ZA HIVI PUNDE.Tafadhali tusitumie lugha kienyeji tunapoteza maana.
 
sukari ya kwangu mnalazimisha nini?wakati nateseka kulima,kupanda na kuvuna mlikuwa kimya leo mnaikomalia sukari kilazima,huu ni ujinga.
kama mambo yakiendelea hivi itafikia kipindi watu walio na pesa nyingi kwenye account zitachukuliwa kilazima ili kusaidia wengine

Wewe hujui kinachoendelea, nitakufafanulia, ngoja tuone hatua itakayochukuliwa baada ya kukamatwa hii sukari
 
Kama wafanyabiashara wananunua sukari ilioharibika na wanaruhusiwa kuingiza na mamlaka husika ya chakula na dawa ipo, ndo nn sasa!?
Sasa hayo unamuuliza nani?? Hizo maalaka si ndo hizi zina wafanyakazi ambao wakifukuzwa watu mnakimbilia kusema wanaonewa?? Au huko kwenye hizo mamlaka unazosema wanafanya kazi makada wa vyama??
 
Nyie endeleeni tu kuashabikia ubabe wa huyu jamaa...kuna siku yakiwageukia msije kulalama tu hap maana kiendacho juu hurudi chini. Yangu macho!
Sijui kama inachagua nani anayetakiwa kutenda makosa. Kama na wewe unatenda ukafikiri kwa vile unajifanya UKAWA hutapatwa, tulia ili ukaseme si wa kwako.

Mlizoea kwa JK kila mtu alikuwa mchambuzi wa siasa.
 
Hakuna namna,watumbuliwe2, wanapanga njama usiku wa manane inchi imshinde jamaa alafu akiwaminya eti oooh utawala wa sheria,Mara dikteta! Wamezoea breaking news za kwenye BBC na DW "eti sukari imeadimika inchini Tanzania" au utaona wana piga picha mistari mire3eefu ya wasakatonge kwenye harakati za Lusaka sukari na kuandika " sukari kitendawili" Sasa yatageuka sukari inagawiwa bureeee' ,Njaa mbaya sana wengi wenu(wafanyabiashara) mmefanya haya either kwa uroho na urafi au political interest! I know mpaka wabunge mmoo! Wengine wa kijani! Wazee wa hoja ya dharura SASA MTAISOMA NAMBA,MTASHIKA ADABU ZENU...#SUKARI#SHIKA ADABU YAKO..!!
 
Ninahisi giza kuhusu democracy na utawala wa sheria huko tuendako. Huu mwendo haufai kushabikiwa asilani. Kweli tulihitaji kiongozi wa kufanya uamuzi lakini sio wa kututawala kimabavu hivi. Tusipomkemea sasa tusijekushangaa siku akitaka kubadilisha katiba ili awe kama Kagame.

Dah nzuri sana, tulimsubiri Raisi wa namna hii kwa miaka mingi. Asante Mungu kusikia kilio cha watanzania
 
Ningependa kujua hata Kama huyo mfanyabiashara amenunua stock kubwa kiwandani kwann viwanda visizalishe tena, si tulisema nchi hii ni ya viwanda na kuzuia sukari kutoka nje mpaka vibali maalum,,, ndo mambo gani ya kuvamia maghala ya watu... Viwanda fanyeni kazi zenu
 
Mwaka wa serikali unaanza July na kuisha June... Hivi unafikiri kuanzia hiyo July 2015 mpaka leo hakuna sukari iliyoagizwa kucover hiyo deficit ya Tani laki 3??? Msitake kuaminisha watu kuwa tatizo la sukari ni kubwa kiasi hicho wakati kabla ya kupiga ban tayari sukari ilishaagizwa nyingi tu.. Mbaya zaidi deficit ilikuwa ni laki 3 lakini walikuwa wanaleta sukari zaidi ya hizo tani laki 3.. Hatuwezi kuruhusu uchumi wa kisanii namna hiyo mkuu..
Tatizo lilianza baada ya zuio la kuagiza sukari, na mpaka sasa serekali inasema imetoa kibali cha kuagiza, bado haijaingia nchini, kwa nn isingejiwekeza zaidi kwenye kuzalisha kwasababu soko ni kubwa? We huoni kama kuna tatizo hapo?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ningependa kujua hata Kama huyo mfanyabiashara amenunua stock kubwa kiwandani kwann viwanda visizalishe tena, si tulisema nchi hii ni ya viwanda na kuzuia sukari kutoka nje mpaka vibali maalum,,, ndo mambo gani ya kuvamia maghala ya watu... Viwanda fanyeni kazi zenu

Wazalishe tena wakati mawakala watakuwa hawaendi kununua? Si sukari watakuwa wamezificha ndani..!! Au unadhani kiwanda kinazalisha sukari ili watu wakanunue kwa kilo kama unavyununua dukani kwa mangi?
 
Tatizo lilianza baada ya zuio la kuagiza sukari, na mpaka sasa serekali inasema imetoa kibali cha kuagiza, bado haijaingia nchini, kwa nn isingejiwekeza zaidi kwenye kuzalisha kwasababu soko ni kubwa? We huoni kama kuna tatizo hapo?
Mkuu sukari sio mchicha kwamba leo leo mseme tuzalishe basi kesho iwe sokoni.. Soko wanaloexpect kuwa kubwa ni la kuanzia July 2016 mpaka June 2017 kwahiyo hizo measures zimeshaanza kufanywa sasahivi.. Nenda Kagera ukaone vijana wanavyopambana kulima miwa kwa wingi sasahivi. Ni kwasababu tayari wana hakika miwa yao itapata soko. Mkuu unakumbuka lile sakata la wakulima kutupiwa miwa yao pale Mtibwa?? Unafikiri kiwanda kingekuwa na uhakika kwamba sukari watakayozalisha kutoka kwenye miwa hiyo itaenda kuuzika sokoni wangeitupa??

Hapo kwenye red naomba nikujibu hivi; wewe hufikiri kama zuio limewaumiza hawa wafanyabiashara na ndio maana wanafanya kila aina ya fitna kumwangusha Rais (hawamuangushi Rais pekee, hata wale wakulima wa miwa ambao ni watanzania wenzetu)... Hapo kwenye blue; ina maana ikiingia itacover deficit na bei inaweza kuwa diluted na kupungua.. Ni jambo jema. Hapo kwenye green nimekujibu kwenye aya yangu ya kwanza..
 
Mkimaliza Sukari kavamieni Banks nao wanaficha Dola ili iadimike na kuuzwa kwa bei ya juu!
Uchumi ni Kanuni sio Amri, Kazi ya kusimamia uchumi inahitaji akili sio sio nyepesi kama kuwasha na kuzima Mwenge!
Ivi unadhani BOT hawajui reserve ya dola hapa nchini? Unajua kuandika neno uchumi tu lakini hauujui practically
 
Sasa hayo unamuuliza nani?? Hizo maalaka si ndo hizi zina wafanyakazi ambao wakifukuzwa watu mnakimbilia kusema wanaonewa?? Au huko kwenye hizo mamlaka unazosema wanafanya kazi makada wa vyama??
Samahani, mimi si mfuasi wa vyama vya siasa, tunaongelea maslai ya wananchi na hatua serekali inazochukua kutatua matatizo yetu. Hata wakichukua sukari yote na kuigawa bado haitatosha, ile iliozuiliwa isiingie hakuna mbadala wake, kwa nn isipande bei!? Wewe mwenyewe umeona tangu bei elekezi imetangazwa nani kaifuata? Na kuna mtu yeyote amechuliwa hatua? Tutegemee upungufu mkubwa zaidi wa sukari..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
A person causing artificial shortage of supplying commodity is regarded as "OFFENSE" under 1st schedule sect.3(1).
 
Back
Top Bottom