Msemaji wa Serikali: Suala la mashabiki kukaguliwa ‘Passport’, Waziri Ndumbaro alikuwa anatania

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462


Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akizungumza na Wanahabari, leo Machi 24, 2024, mada Miaka Mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

KUHUSU KAULI YA WAZIRI NDUMBARO
Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema “Katika Lugha za michezo utani ni kitu cha kawaida, mnapozungumza 80% ni utani na 20 ndio ukweli, mkizungumza habari za Simba na Yanga ukang’ang’ana kitu kama kilivyoandikwa utafika hatua utawachosha watu.”

Amesema hayo wakati akifafanua kauli iliyotolewa na Waziri wa Michezo, Damas Ndumbaro kuwa mashabiki watakaguliwa pasi za kusafiria wakati wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayohusisha Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Ameongeza “Hizo ni timu ambazo zinapenda utani, zinapokea ujumbe katika lugha rahisi, si kweli kuwa Waziri alimaanisha kutakuwa na ukaguzi wa Passport, anayehusika na ukaguzi halali ni Idara ya Uhamiaji ambayo hakuitaja alipozungumza.”

Matinyi ameongeza kuwa “Watu wamekomaa na utani hadi Mamelodi wamesikia, wameingia uoga hadi TFF wameamua kuandika barua kuwaeleza suala hilo halipo.”
 
Ndumbalo hajawahi kuwa na akili na amezunguka mawizara chungu nzima hana tija

Msemaji wa serekali Acha kupaka rangi kinyesi. Kinyesi ni kinyesi tu.

Eti utani, we unaona kulikuwa na utani pale au wewe msemaji ndio unaleta utani sasa.

Sijui mh Rais huwa anawapata wapi baadhi ya mawaziri na sijui kwann huwa anawakumbatia hata wanavyoonesha failures sehemu mbali mbali!!!
 
“Alichozungumza Mheshimiwa Waziri wa Michezo Dkt.Ndumbaro alikuwa anahamisha Uzalendo wa timu zetu na katika lugha zetu za michezo waandishi wa michezo tunafahamu, mimi niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) sisi tukizungumza 80% utani, 20% tunazungumza vitu vimekaa vimenyooka.

Ukizungumza vitu vinavyohusu Simba na Yanga ukang’ang’ana kuzungumza kitu kama kilivyoandikwa mahali fulani inafika muda unawachosha watu, hizi ni timu zinazopenda utani ni timu zinazopokea ujumbe wakati mwingine kwa lugha rahisi, si kweli kwamba Mheshimwa Waziri alimaanisha pale itakaguliwa pasipoti, anayejua pasipoti halali na isiyo halali ni idara ya uhamiaji, hakusema idara ya uhamiaji itaenda uwanjani.

Kwa hiyo katika ushabiki huohuo wa mpira watu wamelifanya jambo hili la mzaha mpaka Mamelodi wamesikia wameingia uoga”- Mobhare Matinyi, msemaji Mkuu wa serikali akifafanua juu ya alichokisema Waziri wa utamaduni, sanaa na michezo, Damas Ndumbaro alipotangaza kuwa shabiki atakayekwenda uwanjani kutazama mechi za kimataifa za @SimbaSCTanzania na @YoungAfricansSC anapaswa kuvaa jezi za Simba au Yanga kinyume na hapo atalazimika kuwa na hati ya kusafiria ya nchi ambayo klabu anayoenda kuishangilia inatokea ila vinginevyo hatoruhusiwa kuingia uwanjani.
 
Screenshot_20240324-135441~2.png
 
Asirudie tena huo ujinga na wala sio kweli kuwa alikuwa anatania.

Wasingem-pressure hilo tamko lake lilikuwa linaenda kutekelezeka, ni basi tu kwasababu kila mwana sports amepinga hadi TFF ndio sababu unaona anakuja na kauli hiyo.
 
Waziri ambaye na mashaka sana kama Mh. Rais atamrudisha kazini 2025 ni huyu Ndumbaro.
 
Dah.... Yaani Hawa viongozi wakikaa wanatuona kama watoto wa chekechea, hata tanesco watakuja siku watuambie swala la kumaliza mgao wa umeme walikua wanatutania
 
Back
Top Bottom