Serikali: Marufuku kupiga kelele Maeneo ya Makazi!

safi san utitiri wa bar zilizojaa sinza na ya mkelele .....
 
Nionavyo mimi sheria inayotakiwa kufuatiliwa ni sheria inayozuia uwepo wa hivi vitu(bar,kumbi za starehe n.k)kwenye makazi ya watu,kwa kuwa issue sio kelele tu bali mbali na kelele zipo kero nyingine kama kuporomoka kwa maadili katika jamii,mfano kama bar ipo karibu na makazi ya watu yanayojiri bar baada ya watu kulewa sote tunatambua ni pamoja na matusi,ugomvi na mengine yasiyofaa ambayo ni sumu kwa kizazi cha watoto wanaokuwa.Wapo itakaowacost kutokana na uzembe wa mamlaka usika zillizofumbia macho tatizo hili mpaka limekuwa kubwa kwa kiwango hiki lakini hakuna jinsi serikali ikaze buti na kusimama katika mstari wa sheria bila kuangaliana usoni kwani faida ya kusimamia sheria hii ni kubwa kuliko hasara.Tunaamini waziri wa mazingira yupo na siyo tu yupo bal YUPO KAZINI.
Msem nakubakiana nawe kabisa. Suluhisho si kuruhusu watu wafanye makelele kwa kulipia bali kuzuia kabisa. Madhara ya kelele hizo hayaondokinkwa mtu kukipa milioni kumi! Nafikiri wangesimamia hizi kumbinza starehe zisijengwe kwenye makazi ya watu na pia ziwe ni kumbi zile zinazozuia kelele kutoka nje. vinginevyo naona hii itakuwa njia ya kukusanyia mapato ya serikali
 
Hii kero ni ngumu kutekelezeka Kama ilivyo vigumu kutekeleza sheria ya kuvuta sigara Mbele za wengi
 
Wakimaliza huko kwenye mabaa na majumbani, warudi kwenye hizi bodaboda.

Tunawapenda sana ndugu zetu wa bodaboda kwani wamerahisisha sana huduma za usafiri.....tatizo ni hayo makelele ya hizo pikipiki zao jamaniii dah..ni kero kubwa sana na chakushangaza sio zote zina makelele.

Wengine nafikiri wanang'ofoa mafla kwa makusudi kabisa ili zipige makelele....hii imekuoa ni kero mpya na inatusumbua sana humu majumbani na mitaani kwa kweli.
 
Adhana ikipigwa haizidi 10 min ila kuna yale madisko ya walokole .. 24/7 kero sana
 
Nionavyo mimi sheria inayotakiwa kufuatiliwa ni sheria inayozuia uwepo wa hivi vitu(bar,kumbi za starehe n.k)kwenye makazi ya watu,kwa kuwa issue sio kelele tu bali mbali na kelele zipo kero nyingine kama kuporomoka kwa maadili katika jamii,mfano kama bar ipo karibu na makazi ya watu yanayojiri bar baada ya watu kulewa sote tunatambua ni pamoja na matusi,ugomvi na mengine yasiyofaa ambayo ni sumu kwa kizazi cha watoto wanaokuwa.Wapo itakaowacost kutokana na uzembe wa mamlaka usika zillizofumbia macho tatizo hili mpaka limekuwa kubwa kwa kiwango hiki lakini hakuna jinsi serikali ikaze buti na kusimama katika mstari wa sheria bila kuangaliana usoni kwani faida ya kusimamia sheria hii ni kubwa kuliko hasara.Tunaamini waziri wa mazingira yupo na siyo tu yupo bal YUPO KAZINI.
bar uswahilini ndipo kuna balaa na huko kuwadhibiti ni vigumu mmo hata Wamiliki wake wengi huwa hawafuati sheria watu huanza kunywa Pombe hata Asubuhi mapema .
 
Wakimaliza huko kwenye mabaa na majumbani, warudi kwenye hizi bodaboda.

Tunawapenda sana ndugu zetu wa bodaboda kwani wamerahisisha sana huduma za usafiri.....tatizo ni hayo makelele ya hizo pikipiki zao jamaniii dah..ni kero kubwa sana na chakushangaza sio zote zina makelele.

Wengine nafikiri wanang'ofoa mafla kwa makusudi kabisa ili zipige makelele....hii imekuoa ni kero mpya na inatusumbua sana humu majumbani na mitaani kwa kweli.
Hata bajaji pia nazo zina miziki mikubwa siku hizi hata baadhi ya Magari binafsi yanapiga miziki yakiwa kwenye foleni,
 
Serikali imeanza kuifwatilia sheria ya kuzuia makelele yanayofanywa na bar, mahoteli, kumbi za starehe zilizo kwenye makazi ya watu pmj na makanisa yanayohubiri usiku kucha kwa kuweka spika ya sauti kubwa, mambo ambayo yamekuwa yakitukera watu wengi lkn tulikuwa hatuna la kufanya, sasa Serikali yetu imesema STOP!

Na saa nne usiku ni mwisho wa makelele kwani watu wana kazi za kufanya, watoto wanataka kusoma, wanafunzi wanajitayarisha kwa mitihani, wafanyakazi wamechoka na wanataka kupumzika!

======
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeanza kung’ata kwa kutumia kanuni ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kelele na mitetemo.

Kwa sasa mtu akitaka kufanya sherehe mtaani, kupiga muziki kwa kelele, kuendesha ngoma za kukesha za nusu uchi (vigodoro) au ‘bai koko’ au kufanya ibada kwa kelele mitaani, atapaswa kulipa Sh milioni 10.

Pia, baa na kumbi za starehe za usiku zitakazopiga kelele, zitapaswa kulipa kiasi hicho.

Aidha, NEMC imesema pia kuwa wale watakaohusika na kelele za migodini za kutumia baruti, kupasua miamba zilizo zaidi ya matakwa ya sheria ya mazingira ya kelele na mitetemo, watapaswa kulipa Sh milioni tano ili kupata kibali.

NEMC imetaka watu kuheshimu kanuni za viwango vya kelele na mitetemo katika maeneo mbalimbali nchini. Imeonya kuwa watakaokiuka, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Kanuni hizo zimeanza kutumika mwaka jana (2015).

Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC, Bonaventure Baya alisema hayo Dar es Salaam jana. Alisisitiza kuwa uchafuzi wa mazingira, unaosababishwa na kelele na mitetemo, umekuwa ukifanyika bila kujali sheria za nchi na sasa watashughulikia suala hilo ipasavyo.

Alisema hivi sasa kanuni za kudhibiti suala hilo, zimekamilika na zimeanza kutumika kikamilifu. Mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha kanuni na sheria, atachukuliwa hatua kali. Baya alitoa ufafanuzi kuwa yapo maeneo yenye kelele zaidi ya viwango vinavyoruhusiwa kisheria, ikiwamo maeneo ya migodini.

Alieleza kwamba kanuni zimeweka vigezo na tozo maalumu la kuanzia Sh milioni tano hadi Sh milioni 10, kulingana na eneo na aina ya kelele na mtetemo. Alisema mambo mengine ambayo kanuni zimeweka ni faini kwa kila kanuni itakayovunjwa na kusisitiza kuwa hatua hizo zitachukuliwa ipasavyo.

Kulingana na hatua hiyo ya NEMC, sasa mtu mwenye kutaka kufanya sherehe mtaani, itakayohuisha kelele zitakazosumbua jamii pamoja na majirani zake, ikiwamo muziki maarufu wa ‘kigodoro’, ibada za makanisani zinazozidi matakwa ya kisheria ya uanzishwaji wa makanisa hayo katika jamii, atapaswa kulipa Sh milioni 10 ndipo aruhusiwe kuendelea na shughuli yake.

Kwa mujibu wa NEMC, ruhusa hiyo inayo lipiwa, pia ina muda na viwango vyake, ambapo kila muda husika unapoisha, kelele zinapaswa kupunguzwa ama kuzimwa. Hii inahusisha pia baa na kumbi za starehe za usiku.

Baya aliitaka jamii kuepuka uchafuzi huo wa mazingira wa kelele na mitetemo, ambao watu wengi wamekuwa wakidhani si tatizo. Alitaka watu kuheshimu matakwa ya sheria na kanuni kwa nyakati za mchana na usiku.

“Tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa watu wengi, wakilalamikia usumbufu wa kelele na mitetemo kutoka kwa watu wanaoendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii katika jamii,” alifafanua Baya.

Alitoa angalizo kwa wanaotumia vyombo vya muziki na sauti katika maeneo ya makazi, ambavyo vimeleta madhara kwa afya za watu. Alisema matumizi ya vipaza sauti na vyombo vya sauti kubwa, wanapaswa kuwa na kibali maalumu.

Alieleza kuwa kanuni za kelele na mitetemo, zimeweka vigezo na viwango vya sauti kwa ajili ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya hospitali, makazi, migodini, kumbi za kijamii, kumbi za usiku za starehe, matangazo, baa na maeneo mengine.

Baya alisema baraza limepata changamoto kadhaa, ikiwamo uelewa mdogo wa jamii kuhusu kiwango cha sauti kinachotakiwa na kisichoruhusiwa na baadhi ya watu kwa makusudi huvunja sheria.

Kuhusu faini, alisema sheria ya mazingira imeweka wazi faini kwa wanaokiuka na kuchafua mazingira kwa kelele na mitetemo. Faini hiyo haiingiliani na tozo la Sh milioni tano hadi Sh milioni 10 lililoelezwa, ambapo mtu anapaswa kulipa si chini ya Sh milioni 50 na si zaidi ya Sh milioni 50 ama kifungo jela.

Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sheria za Mazingira wa NEMC, Ruth Lugwisha alisema tatizo la kelele na mitetemo, limekuwapo kwa muda mrefu. Alisema tangu kupitishwa kwa kanuni, tayari watu kadhaa wamewajibishwa.

Alisema miongoni mwa waliowajibishwa ni makanisa, kumbi za starehe na baa. Hata hivyo, hakuwa tayari kuwataja wahusika wala maeneo. Alisema uwajibishwaji huo ulihusisha faini, kufungiwa na onyo.

Tukio la Masasi Oktoba mwaka huu wakazi wanne wa eneo la Masasi Mbovu katika Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara, walifikishwa mahakamani kwa kosa la kucheza wakiwa watupu kwa staili ya ‘vigodoro’ kwenye sherehe ya ndoa.

Wakazi hao ni Jemima Jordan (22), Aziza Chukachuka (20), Anna Yohana (25) na mtoto mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa). Watuhumiwa hao baada ya kupatikana na hatia, walilipa faini na kuachiwa huru.

Maoni ya wananchi wa Tanga Huko Tanga, baadhi ya wananchi walisema hivi karibuni kuwa matamasha na promosheni mitaani, sasa zimekuwa kero. Waliomba idara ya utamaduni kwa kushirikiana na mamlaka nyingine, zinazohusika na utoaji wa vibali kwa ajili ya mikutano, maonesho na matamasha jijini Tanga, kupunguza kero ndani ya jamii.

Walitaka mamlaka hizo, kuacha kutoa vibali vya matamasha ya burudani na starehe zisizo na staha katika jamii, kwa sababu zinasababisha kelele mitaani na kuwanyima wanafunzi muda wa kujisomea.

Wananchi hao walidai matamasha yanayoambatana na kelele za ngoma na muziki, yanakwamisha ustawi wa elimu na kukua kwa kiwango cha taaluma, hasa kwa wanafunzi wa sekondari.

Damas Mboya, mkazi wa Ngamiani, alisema matamasha na promosheni zinazofanyika mitaani nyakati za mchana na usiku, hudumaza maadili na ni kero kwa jamii kwakuwa zinatumia vipaza sauti kucha usiku kucha.

Merina Kimweri, mkazi wa Chumbageni, alisema “Naishauri serikali na mamlaka husika, zipunguze idadi ya vibali vya kuruhusu shughuli hizi, hasa zinazofanywa mitaani bila viingilio.

Nasema hivyo kwa kuwa mara kadhaa zinaambatana na burudani za ngoma za kukesha, maarufu kama vigodoro na baikoko ya usiku, ambapo washiriki wakuu ni wanafunzi” .

CHANZO: HabariLeo
hakuna jipya hapa. kama kweli serikali ina ubavu wa kuzuia KELELE kwa maana ya KELELE, waanze kupiga ban zile kelel za SAA 11 ALFAJIRI. hakuna kelele zinazokera na kuudhi kuliko hizi kelele za maspika ya alfajiri.

CC: @FaizaFoxy
 
Kwako ni adhana kwa wenzio ni kelele, ni sawa na mabaa kwenye sehemu za makazi wanaokunywa wanafurahia lakini kwako ni karaha. Anti-social behaviour isikubalike na kuhalalishwa. Misikiti ya ulaya mbona hawatumii loud speakers ni kwa sababu sheria zinafuatwa na hakuna anayelalamika.
exactly! kwanza katika enzi hizi za dijitali, ni USHAMBA NA KUTOKUJITAMBUA ikiwa bado watu wanatarajia kuamshwa kwa maspika badala ya alarm. dhana nzima ya maspika inakosa uhalali kwa kuwa kila raia anayo saa ambayo anaweza kuweka alarm ili imsaidie kuamka kama kweli anataka kwenda kuswali.
 
Tupatieni namba za simu .tupige mbara tunapo sikia kelele mtaani .kama kweli mpo serious kuondoa hili tatizo
 
NI KUMBI GANI? YA STAREHE AMBAYO IPO MBALI KIASI CHA KUTOSHA KUTOBUGUDHI WATU??/
KWA MAANA YAO / KUMBI ZIJENGWE JANGWANI AU KULE BONDE LA SUKITA! MAANA HATA MZIKI MARA UPIGWAPO JANGWANI PIA HUKERA VILEVILE/,HEKIMA ITUMIKE ZAIDI NEMC WAACHE SHUGULI ZA SOCIAL ZIENDELEE NA MARA MZIKI UNAPOZIDISHWA MAJIRANI WAKAE WATAFUTE MNAMA YA KUTATUA / HIVI NDIVYO WATANZANIA TUNAVYOISHI SIKU ZOTE!
Nashauri serekali isirukie kila jambo ili ati waziri au muhusika aonekane ni mpambanaji nope!
n.b
****
NI BUSARA KWA WAKATI HUU SEREKALI IKAJIKITA KTK UKUSANYAJI MAPATO KWA UMAKINI MKUBWA /
#KUZIBAmianyaYOTE/
 
Saa 4 usiku...?? Huko ni mbali sanaaaaaaaaa wangefanya saa 2 usiku ni mwishooo...!!! Sasa walokole na baikoko, vigodoro mwisho ingefaa saa 2 usiku... maana wanapiga makelele kutangaza biashara zao za dini na ngono usiku kucha...!!
Kila siku naipenda serikali ya Magufuli... hakuna mchezo... ni kazi tu... wako watu wanacheza vigodoro makalio nje nje mjini hapa Dar ni balaaa, pia walokole wamekuwa kama machangudua tu, usiku makelele na wanafanya uzinzi sana tu...

Stooop... saa 2 usiku...!!
 
safi san utitiri wa bar zilizojaa sinza na ya mkelele .....
Wamiliki wengi wa bar sinza ni Watumishi wa umma ni vigumu kuzifunga na hii ndiyo changamoto ya mwaka maana hawatakaa wafanikiwe Kwa Hilo.
 
Saa 4 usiku...?? Huko ni mbali sanaaaaaaaaa wangefanya saa 2 usiku ni mwishooo...!!! Sasa walokole na baikoko, vigodoro mwisho ingefaa saa 2 usiku... maana wanapiga makelele kutangaza biashara zao za dini na ngono usiku kucha...!!
Kila siku naipenda serikali ya Magufuli... hakuna mchezo... ni kazi tu... wako watu wanacheza vigodoro makalio nje nje mjini hapa Dar ni balaaa, pia walokole wamekuwa kama machangudua tu, usiku makelele na wanafanya uzinzi sana tu...

Stooop... saa 2 usiku...!!
Pia ule Uvaaji wa nguo chini ya matako unaopendwa na wengi Vijana sasa ni mda wa kurejesha maadili ingawa ni kazi ngumu kuliko zote maana Waziri wa Utamaduni hathubutu kuwagusa hao Vijana Wavaaji mlegezo .
 
NI KUMBI GANI? YA STAREHE AMBAYO IPO MBALI KIASI CHA KUTOSHA KUTOBUGUDHI WATU??/
KWA MAANA YAO / KUMBI ZIJENGWE JANGWANI AU KULE BONDE LA SUKITA! MAANA HATA MZIKI MARA UPIGWAPO JANGWANI PIA HUKERA VILEVILE/,HEKIMA ITUMIKE ZAIDI NEMC WAACHE SHUGULI ZA SOCIAL ZIENDELEE NA MARA MZIKI UNAPOZIDISHWA MAJIRANI WAKAE WATAFUTE MNAMA YA KUTATUA / HIVI NDIVYO WATANZANIA TUNAVYOISHI SIKU ZOTE!
Nashauri serekali isirukie kila jambo ili ati waziri au muhusika aonekane ni mpambanaji nope!
n.b
****
NI BUSARA KWA WAKATI HUU SEREKALI IKAJIKITA KTK UKUSANYAJI MAPATO KWA UMAKINI MKUBWA /
#KUZIBAmianyaYOTE/
Wakaige mfano kule South Africa kuna bar za mitaani lakini hazipigi miziki Kwa sauti kubwa wengi hujenga sound proof kuzuia bar mitaani haiwezekani bali wadhibiti usumbufu wa sauti kubwa tu.
 
Hii huenda ni pato jipya la wajanja Kwa mwaka 2016 maana kila mkwara huwanufaisha wajanja wachache ambao huwa wepesi wa kutumia fursa Kwa kasi kubwa, walizuia pikipiki zisiingie mjini sasa umegeuka kuwa mladi wa wajanja na sasa wajanja watakuwa wakipita kwenye Hizo bar kuwachukulia pesa Wamiliki wake. Nadhani hili jambo linahitaji utafiti na tathimini ya kutosha kabla hawajaanza kuchukua Hatua.
 
SEREKALI LAZIMA IFANYE KAZI KWA PHASES
PHASE I --KUDHIBITI MAPATO,KUDHIBITI MIANYA.
PHASE II---MATUMIZI BORA YA MAPATO HAYA/ VALUE FOR MONEY.
PHASE III---GOVT TENDERS,e-tendering/openness in every tenders.
PHASE IV--->>
 
AZANA HUWA INANISUMBUA SANA SAA 11ASB,SAA 8MCH,SAA 10JIONI, SAA 2,USK.
HAKIKA NI KERO SANA!
NA HILI LIFUATILIWE!
ii
Eti saa 8MCH, Uwe unajaribu kuficha ujinga kidogo, kwenye hilo andiko kuna mahala pametajwa adhana au msikiti, au unafikiri walioandaa hili andiko wana akili kama zako.
 
Back
Top Bottom