Serikali kupoteza trillion 3 ukwepaji kodi

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
WAKATI Serikali IKIJIGAMBA kwa kukusanya takriban Sh. trilioni 8 kutoka vyanzo vya ndani vya mapato katika miezi 12 kuanzia wiki ijayo, uchambuzi wa misamaha ya kodi nchini unaonyesha kuwa takriban Sh. TRILLION TATU zimekuwa zikipotea kutokana na biashara za kimataifa, pamoja na uzembe katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Biashara za kimataifa

Katika eneo la biashara za kimataifa, takwimu zilizopo ambazo baadhi ni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonyesha kuwa, upotevu wa mapato umekuwa ukiongezeka kutoka jumla ya Sh. bilioni 359 mwaka 2006 na 2007 hadi Sh. bilioni 616.5 kati ya mwaka jana hadi Februari mwaka huu.


Taasisi za Serikali kati ya mwaka 2011 hadi mwanzoni mwa mwaka huu zilikuwa zimesababisha ukosefu wa mapato kwa kiwango cha Sh. bilioni 5.184, wakati mashirika ya umma yakisababisha upotevu wa Sh. bilioni 5.153.

Aidha, kupitia eneo hilo hilo la Idara ya Forodha kwa upande wa Biashara za Kimataifa, takwimu zinaonyesha kuwa baadhi ya taasisi za kidini nazo zimo kwenye ufujaji wa mapato ya nchi, na kati ya mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu, milioni 114 zimepotea huku, Sh. bilioni 7.5 zilizopaswa kukusanywa kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) zikiishia katika ‘mifuko’ ya wajanja.


Miradi ya wafadhili nayo imekuwa sehemu ya upotevu wa mapato makubwa ya Serikali na katika kiwango cha jumla cha upotevu wa Sh. trilioni tatu, miradi inayofadhiliwa na nchi wahisani, ujanja umefanyika na upotevu wa Sh. bilioni 170 kati ya kipindi kisichozidi miaka miwili, kati ya mwaka huu na mwaka jana.

Uchochoro mwingine wa upotevu wa mapato ni baadhi ya ofisi za balozi za nchi mbalimbali zilizopo nchini na katika eneo hili, Sh. bilioni 4. 62 zilizopaswa kukusanywa zimeliwa na mafisadi.


Bidhaa mbalimbali zinazoagizwa na kuingizwa katika majeshi ya ulinzi na usalama, ambako huku kumekuwa na maduka maalumu ya bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wanajeshi, nako imebainika kuwa takriban milioni 885 hazijakusanywa.

Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwenye majeshi, katika eneo linalohusu bidhaa za kimataifa zinazoingiwa na kampuni au watu binafsi nchini takriban Sh. bilioni 150.2 ‘zimeliwa.’


Sekta ya madini ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu na watu wa kada mbalimbali nchini nayo imepoteza mapato ya Sh. bilioni 92.7, wakati kituo cha uwekezaji nchini kikifanikisha upotevu wa Sh bilioni 179.8.


Idara ya Mapato ya Ndani


Mchanganuo huo wa upotevu wa mapato pia unahusisha eneo la Idara ya Mapato ya Ndani na takwimu zikionyesha kuwa eneo hili limepoteza takriban Sh. trilioni 1.05, ambazo pia zinajumuisha upotevu wa Sh. bilioni 429.2 kutokana na misamaha ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

SOURCE: GAZETI RAIA MWEMA

[h=2][/h]
 
Back
Top Bottom