Serikali kuja na mwongozo wa gharama za kumuona Daktari

KWA COMMENTS NYINGI NAZOZIONA NI PICHA HALISI KUWA SERIKALI INAHITAJI KUTOA ELIMU KUHUSU VITU VINGI TU SIO KUHUSU FEDHA PIA HATA KUHUSU KUACHA KUBISHA KILA KITU WAKIAMINI NI VIPYA NA VINA WAKANDAMIZA WAO WAACHE PHOBIA ZA KILA KITU
 
Ni consultation fee….tukisema gharama za kumuona daktari tunakosea sema ndo hvyo waziri nae ni binadamu…Sawa na ukitaka kuonana na mtu ambae anataka kukupa ushauri Fulani kuhusu maisha yako…
 
kutawala wabongo rahisi sana. hapo serikali inataka kuwagombanisha na madaktari ionekane hiyo hela wanachukua hao madaktari.. na uliza madaktari pia hawaipendi hiyo tozo...

tatizo linakuja je wakiifuta , hiyo serikali ita gharamikia Matumizi ya hospital kama maji, umeme, ulinzi..hospitali
Nimekuambia suala hapo sio kuwatawala wabongo ,nimeelza waziri alikua na kikao cha wafanyakazi wa hospital akaona sio vibaya awasikilize wagonjwa kama kuna kero yeyote , uzuri wagonjwa wote hakuna alieponda kuwa huduma inayotolewa pale ni mbovu au chini ya kiwango au kuna rushwa na upendeleo , hakuna alietamka hivyo kilio zaidi ya kumuomba waziri aangalie suala la gharama za matibabu zipo juu sana zinaenda sawa na hospitali za binafsi.Pia yeye nae aliwashauri wananchi wajiunge na bima ya afya akisisitiza kwamba wengi wanajiunga wakati tayari ni wagonjwa.
Kuna kipindi inabidi tuwe tu wakweli tusiwe tunaishi kwa hisia na kutunga mambo .
 
Umi alafu alisema kuwa ni wakati wa kujali afya zenu kwani mkifikilia hizo gharama za kujitibu zitakavyo kuwa so inabidi mjali afya zenu, umi umi daaah
 
Madaktari ni wachache na huduma zao ni za dharura tofauti na hizo kada nyingine.
Hapa tulipofika ni pabaya sana, imagine daktari amesomeshwa kwa nguvu ya mnyonge,,ameajiriwa na analipwa na serikali inayotumia kodi za wananchi wanyonge

Mnyonge huyohuyo atoe pesa ili kumuona Daktari

Kwanini hakuna utaratibu wa gharama za kumuona mwalimu, engineer,hakimu,bar maid, nk
 
Hapa anazungumziwa daktari ambaye ni muajiriwa wa Serikali analipwa mshahara unaotokana na Kodi za wananchi Sasa iweje huyu mlipapa Kodi akiumwa akitaka kumuona daktari alipie tena?

Na pia hapa haraumiwi daktari ila inaraumiwa serikali na sera zake
Kwani hiyo pesa anauchukua Daktari au ni mapato ya Serikali?

Hivi ni Nani aliwaambia kuwa madaktari au watumishi wa Afya ndio huwa wanapanga gharama za matibabu kwenye Hospitali?

Aisee, Wanasiasa wameshaona wanaishi kwenye jamii ya mazuzu kwahiyo wanaishi kwa kuyadanganya tu siku ipite.
 
Wiki ilio pita nili mpeleka ndugu yangu hospitali ya mkoa ya mawenzi moshi asee gharama za pale utazani upo KCMC..movie linaanza kufungua file 10k kumuona Doctor 10k vipimo vingine bei zake ndo usi seme za ajabu ajabu tu kwa siku ili ondoka 179k na sielew iliendaje endaje

Note
Kwa wenye bima ilo folen una enda asubuh una chomoka mchana kama co jion
 
Hapa tulipofika ni pabaya sana, imagine daktari amesomeshwa kwa nguvu ya mnyonge,,ameajiriwa na analipwa na serikali inayotumia kodi za wananchi wanyonge

Mnyonge huyohuyo atoe pesa ili kumuona Daktari

Kwanini hakuna utaratibu wa gharama za kumuona mwalimu, engineer,hakimu,bar maid, nk
Jiheshimu,mnyonge gani anamsomesha daktari nchi hii??
 
Hapa anazungumziwa daktari ambaye ni muajiriwa wa Serikali analipwa mshahara unaotokana na Kodi za wananchi Sasa iweje huyu mlipapa Kodi akiumwa akitaka kumuona daktari alipie tena?

Na pia hapa haraumiwi daktari ila inaraumiwa serikali na sera zake
Sahihi kabisa
 
Nakumbuka mwa 2020 nimefika pale Agha khan hospital....gharama ya kumuona daktari 30,000 tena inabidi kumsubir maana anatoka hospital ya serikali kuanzia saa nne asubuhi nasubir hadi saa 11 jioni

Alivyofika jioni hiyo alinijibu kwa kifupi tu....."Hii huduma hatuna jaribu kwingine".....Elfu 30 imeenda daaah 😪😪😪😪
Daah wizi wa wazi huu
 
Ni consultation fee….tukisema gharama za kumuona daktari tunakosea sema ndo hvyo waziri nae ni binadamu…Sawa na ukitaka kuonana na mtu ambae anataka kukupa ushauri Fulani kuhusu maisha yako…
Hata tukitumia kilatini lakini mantiki ni ile ile
 
Hapa tulipofika ni pabaya sana, imagine daktari amesomeshwa kwa nguvu ya mnyonge,,ameajiriwa na analipwa na serikali inayotumia kodi za wananchi wanyonge

Mnyonge huyohuyo atoe pesa ili kumuona Daktari 😧🙆

Kwanini hakuna utaratibu wa gharama za kumuona mwalimu, engineer,hakimu,bar maid, nk
Mwalimu anaoga usaa na damu? Mbona kwa wanasheria consultation na mhuri mnatoa haraka? Acheni kuwadharau alafu mtegemee muujiza.
 
Kwann wasije na mjadala wa kucontrol English medium school wanapandisha ada kila mwaka bila utaratibu hata kama ndio private
 
Back
Top Bottom