Serikali kuhamia Dodoma: Ni kuitenga au kuiangamiza Zanzibar

MaamuZi haya yanafanyaa bila kuzingatia dhana nzima ya kubana matumizi.kwa sasa viongozi wandamizi wa smz watahitaji gharama mara dufu kuifikia serikali yao ya muungano iwapo dodoma.Muungano huu una nguvu zaidi Tanganyika wanaloamua zanzibar haiwezi kuuliza
 
Tatizo lako umerukia mada bila kusoma. Hapa tunazungumzia gharama na si aina ya usafiri

Kama tatizo ni gharama mbona uchaguzi wa juzi mmerudia mara mbili au haukuwa na gharama? Hivyo ninaamini hata gharama za kuhamia Dodoma mtazimudu tuu mkuu.
 
Acha ujinga, Dom ni capital city toka 70s. Mbona hujapinga toka enzi zile? Kuna generation fulani ya wap*mb*v* imeibuka karibuni mnaandika vitu vya hovyo tu. Sijui ni kwa ajili ya sifa au nini lakini mnazidi sasa.

Uhai wa mzee karume mji mkuu ulikua wapi?????
 
Hoja yako ina mashiko tatizo ni upofu walionao watawala wa zanzbar kisa madaraka
Tatizo mnakula sana ulojo hadi hoja zenu zinakuwa laini kama ulojo,kuhamia Dodoma ni uamuzi uliopitishwa miaka mingi bali utekelezaji wake ndio ulikuwa unasuasua kutokana na kutokuwa na miundo mbinu ya kutosha na sasa imekamilika .Na ni kuulize yupi anayetoka mbali kwenda Dodoma je ni yule wa Zanzibar au Tunduru,wakati mwingine tuwe na busara tunapojadili mambo na sio kuwa watu wa kulalama tu kwa malengo ya kisiasa.
 
kwani inayoamua kuhamia Dodoma ni serikali ya Muungano au ni serikali ya Tanganyika ambayo haipo? Mimi naona kuwa muungano unahusiana zaidi na CCM kama ccm haipo Muunganao ni tatizo. unakoelekea itakuwa vigumu sana Zanzibar kutoa rais wa muungano
Ha ha ha! JPM ni Rais wa Muungano au wa Tanganyika? Kumbuka alipigiwa kura Zanzibar tena kura ambazo hazikuwa na utata wowote.
 
.......Ilani ya uchaguzi ya ccm 2015/20 inasemaje juu ya hili?
Ilani (manifesto) ni kitu kimoja na sheria ni kitu kingine. Ilani ikishapita kwa maana ya chama chenye ilani kupewa ridhaa, yaliyomo kwenye ilani hutungiwa sheria mbali mbali za utekelezaji. Je, hiyo sheria ipo? Hata kama ilitungwa zamani ila utekelezaji ulikuwa bado naomba kufahamishwa ni ya mwaka gani na kama kuna amendments zozote.
 
Maamuzi ya kumtoa hata Rais wa Zanzibar hufanyikia Dodoma, sasa kuhamishia makao makuu ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dodoma kuna shida gani? Unaweza kunambia Abeid Amani Karume Jr kama sio Dodoma angekua Rais wa Zanzibar? au hata Shein kama ungekua sio Dodoma angekua Rais wa kule marashi ya karafuu?
Umezungumzia issue ya katiba, hivi Waziri kiongozi wa Zanzibar ni nani? Hicho ndio cheo cha pili kimadaraka kwa Zanzibar kwa mujibu wa katiba. Nyie mkivunja katiba ni sawa, baraza ikivunja utaratibu uluozoeleka sio sawa. Bado naendelea kufanya research yangu; ni wapi duniani ambako kuna Waislam na hawalalamiki kwa chochote? Bado sijapata jibu, naendelea kutafuta.
Nawao wanatafuta ni nchi gani ya kiislam inayo wauwa wakristo wengi kwakutumia mandege ya kivita na mavifaru na majeshi ya angani na aridhini pia wanatafuta ni nchi ipi ya kiislam inayo uwa marais wa kikristo wanao tawala nchi zao na wenye maendeo kama libya na nyinginezo bado wanatafuta.........


.
 
Mleta mada ni "Ipomea batatus"
Dodoma ni makao makuu ya nchi. Hutaki nenda zako kwa mababu zako kule Oman au Yemen
 
Kama tatizo ni gharama mbona uchaguzi wa juzi mmerudia mara mbili au haukuwa na gharama? Hivyo ninaamini hata gharama za kuhamia Dodoma mtazimudu tuu mkuu.
Uli gharamiwa nawatawala wa " kijani" ili wabaki madarakani na hatimaye watupeleke Dodoma. Zanzibar ya sasa haijipatii na haiwezi hata kujikuna bila ya msaada ya "mkuno" wa kijani!
 
Acha ujinga, Dom ni capital city toka 70s. Mbona hujapinga toka enzi zile? Kuna generation fulani ya wap*mb*v* imeibuka karibuni mnaandika vitu vya hovyo tu. Sijui ni kwa ajili ya sifa au nini lakini mnazidi sasa.
Sasa nani mjinga? Anaesoma riwaya za hao wanasema ETI Dodoma mji mkuu wa Tanzania. Hiyoo ilikuwa "ndoto" ya Nyerere kwa ajili ya Tanganyika na ndoto hiyo haipo kisheria na ndio ikafa kwenye vitabu vya CCM. Kama inataka kufufuliwa lazima ifuate taratibu, sheria na "Artcles of the Union" Nchi haiongozwi na ndoto wala mihemk wala matusi kuwaita wengine wajinga kumbe kichwani mwako kuna chemka ujuha!
 
Katika vitendo vilivyokithiri ukiritimba na vinavyoonekana kukiuka makubaliano ya msingi ya Muungano wetu adhimu ya kuwa kila jambo linaliohusu na kugusa maslahi ya nchi zetu mbili lazima zipate ridhaa na baraka ya pande zote mbili za Muungano.

Hoja ya "elfu lela-ulela" ya kuhamisha Makao Makuu ya Serikali ya Muungano sasa imepamba moto licha ya kuchagizwa na utatuzi wa pingamizi ziliokuwepo awali;zilioifanya hoja hiyo iwe ndoto ya kufikirika na kuishia kwenye vitabu vya riwaya.

Hata muasisi wa "ndoto" hiyo alishindwa kuitetea kivitendo na uhalisia maisha yake yote.

Kimsingi naunga mkono kwa dhati kabisa kuwa Makao Makuu ya chama cha CCM na hata Mwenyekiti wake kuhamia Dodoma. Yumkini himaya ya kisiasa ya mji mkuu wa sasa Dares salaam kuhodhiwa na UKAWA inaweza pengine kuwa si rafiki na kuwa kichocheo kilichohamasisha ndoto mfu ya kuhamia Dodoma kufufuka na uzima uliobarikiwa.

kwa misingi hiyo pia sipingi hata Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma ikiwa tu(if and only if) inayohamia Dodoma ni serikali ya Tanganyika (Wizara ambazo si za Muungano).Wizara zote za mambo ya Muungano ziendelee kubaki Dar es salaam ili kuendelea kurahisisha mawasiliano na utekelezaji kwa gharama nafuu kwa pande zote.

Hali hiyo iendelee mpaka pale maslahi makuu ya Zanzibar yatakapokidhi na kuridhiwa kuwa ni rafiki kwa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar na wananchi wake walio wengi(2/3).

Kwa bahati nzuri falsafa ya kura ya maoni Zanzibar ipo na inalindwa na Katiba. Tuangalie kwa undani gharama itazolazimika Zanzibar kuzibeba kutokana na kuhamishwa kwa Makao Makuu na ukubwa wake na vipi zitazidi kuelemea uchumi legevu wa visiwa na watu wake.

Isionekane kuwa viongozi wa Zanzibar hawajaliona hili au wameishiwa mbinu na maneno ya kujenga hoja kulinda maslahi ya Zanzibar,la hasha,lakini inatokana na hali tete ya kisiasa visiwani inayowafanya kuwa nusu bubu ili alau ionekane kuwa wanajaribu kulipa fadhila zenye machungu!

Waungwana wanasema "Uso wa kufadhiliwa umeumbwa na haya (u-chini)".
Kwani znz inaingia gharama gani? Watendaji wote wa serikali wanalipwa na Tanganyika. Wabunge wanaokuja Dodoma wanalipwa na Tanganyika.

Bajeti yao inalipwa na Tanganyika

Pengine ungesema litaongeza gharama kwa Tanganyika. Zanzibar haina gharama zozote katika muungano!

Wazanzibar watulie tu, hawana gharama wala hawajui gharama za muungano

Hawajui maumivu ya gharama, hawajui kuchangia! Watulie tu wale mafao
 
kwa misingi hiyo pia sipingi hata Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma ikiwa tu(if and only if) inayohamia Dodoma ni serikali ya Tanganyika (Wizara ambazo si za Muungano).Wizara zote za mambo ya Muungano ziendelee kubaki Dar es salaam ili kuendelea kurahisisha mawasiliano na utekelezaji kwa gharama nafuu kwa pande zote.
Gharama za kuendesha Wizara za Muungano (mfano Wizara ya Ulinzi) hutolewa na Serikali ya Muungano (of which is purely Tanganyika) au hotolewa na SMZ?
 
Hili ni wananchi wa Zanzibar na si la SMZ. Wananchi wanahaki kuomba kura ya maoni kwa muibu wa Katiba ya zanzibar
Hiyo kura ya maoni ni kwa ajili ya mambo yaliyoko Zanzibar tu. Huku nje ya Zanzibar kuna Katiba nyingine.
 
Muu hapa umenena. Hoja yangu imetokana na makubaliano ya awali. Kitu Dodoma kuwa Makao Makuu hakikuwepo. Hii ndoto ilikuja hata Baada ya muasisi wa Muungano Karume kufa.
Hujajibu swali. Swali liliuliza, kwenye hayo uliyoyaita makubaliano ya awali yalieleza kwamba Makao Makuu yawe wapi?
 
Maamuzi ya kumtoa hata Rais wa Zanzibar hufanyikia Dodoma, sasa kuhamishia makao makuu ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dodoma kuna shida gani? Unaweza kunambia Abeid Amani Karume Jr kama sio Dodoma angekua Rais wa Zanzibar? au hata Shein kama ungekua sio Dodoma angekua Rais wa kule marashi ya karafuu?
Tena ngoja tumkumbushe huyu. Ni kwamba hata kiapo cha utii kwa Baraza la Mawaziri wa JMT alichokula Rais wake wa Zanzibar, ilikuwa ni hapo hapo Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
 
Nawao wanatafuta ni nchi gani ya kiislam inayo wauwa wakristo wengi kwakutumia mandege ya kivita na mavifaru na majeshi ya angani na aridhini pia wanatafuta ni nchi ipi ya kiislam inayo uwa marais wa kikristo wanao tawala nchi zao na wenye maendeo kama libya na nyinginezo bado wanatafuta.........


.
Ninacho wapenedeaga watu wa aina yako hua ndio hicho; matukio ya Libya ni ya juzi tu hapo. Walibya kwanza wajilaumu wenyewe, waliiga mambo ya Tunisia (kilicho tokea Libya, Misri na hata Siria ni copy and paste ya Tunisia, Misri walifauru) walijikuta na wao wana copy na ku paste bila kujali watawala wa Tunisia walikua sawa na mtawala wao? Marekani na jumuia ya NATO walidandia train kwa mbele, walipoona Gadafi anawashikisha adabu raia wake ndipo na wao wakaingia (ni kweli mataifa ya magharibi yalikua na chuki binafsi na Gadaff) So msianze kusingizia tu kwamba Wamarekani. Lakini pia, nani kakwambia kama Wamarekani ni Wakristo? Katika umri hu wa miaka 40 na kidogo sina hakika kama nimewahi kuisikia nchi inayoitwa ya Kikristo. Labda kama utanitajia walau 1 tu.
 
Back
Top Bottom