Serikali kugawa Magari ya Wagongwa 2 na Gari ya Huduma za Chanjo kwa kila Halmashauri nchini

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,123
49,844
ummy.jpg


Magari hayo 528 yamenunuliwa na TAMISEMI kwa kasi hiyo.

Aidha Wizara ya Afya iliwahi kusema imeagiza Ambulance zaidi ya 700 na zitagawiwa nchi nzima.

My Take
Mbona magari hayafiki kila siku ahadi?

======

Serikali imetangaza kupeleka magari ya kubebea wagonjwa mawili na gari moja la uendeshaji kwa kila Halmashauri nchini na tayari baadhi ya magari yameshashuka bandarini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Angela Kairuki leo Jumanne April 18, 2023 wakati akijibu Hoja za wabunge kwenye maombi ya fedha kwa Wizara yake.

Kairuki amesema magari 528 yameagizwa na yanaingia kwa awamu ambapo baadhi yameshafika kazi iliyopo ni kuyakomboa tayari kwa kuanza kuyasambaza kwenye maeneo mbalimbali.

Waziri amesema idadi ya magari hayo yamefikiwa kutokana na namna ambayo waliitumia Tamisemi kwani awali walikuwa na bajeti ya kuagiza magari 407 kabla ya kutumia alichokiita namna wakaongezewa magari 121.

“Hivi ninavyozungumza kila siku napiga simu, hata juzi magari mengine yaliingia nchini na mengine yako njiani yanaletwa, niwahakikishe wabunge kwamba kila halmashauri inapata mgao wa magari mawili ya wagonjwa na gari moja la uendeshaji mapema iwezekanavyo,” amesema Kairuki.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, tayari magari 25 ya kubebea wagonjwa yameshalipia gharama zilizotakiwa na sasa yanapelekwa kwenye maeneo husika.

Mwananchi
 
Mm nikajua unaonyesha magari yapo halmashauri tayari. Kumbe unazungumzia stories tu
 
Tulia watu walambe asali hayo magari yatakufikieni baadae baada ya kelele nyingi za wananchi kuyachosha masikio ya hawa majambazi wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom