Serikali ipige marufuku matamasha ya fiesta

Mkuu naona hoja ya mleta mada ni sahihi...inatakiwa iundwe tume ya kijasusi ichunguze haya matamasha walete evidence ya videos na audios ya kinachofanyika humo..

Pia whatever the case,kwa walio na watoto teenagers hasa wa kike,aisee haya matamasha na media za Shigongo na Clouds hazifai kabisa....kwa wote wenye watoto,kwa uchungu uliopo wa malezi haya matamasha na hizi media ni za kufuta kabisa...

Zimeharibu akili za watoto 100%,kila mtoto anaabudu hawa watu na haya matamasha,hii ni hatari,mind control ni kubwa

Clouds ni tawi la ccm. Usitegemee kiongozi yoyote akosoe utendaji kazi wao.
 
Hajaota wasanii leo kwenye mitandao ni kuvaa nusu uchi kutaja wanaume au wanawake wangapi wameshagegedwa. Tusipochukua hatua vijana wa kesho hatuna. Very fact usibishe kwa sababu labda wasanii wakionesha vimapaja vyao labda ndo wengi hujisikia
Babu na bibi zako walivaaje au waliowatangulia walivaa je. Mavazi ni tofauti na akili ya mtu. Watu wanafunika nyuso lakini wanapelekea hawara vyakula wengine ndo wanalipua wenzao? Mavazi ni kitu cha kupita. Nani anavaa pekosi siku hizi, nani anavaa turnup siku hizi? Ndo maana mwaka 1974 Kawawa alipotuchania skirt shuleni, Mwalimu alisema msiwasumbue hii ni fashion itapita. Usiwe na wasi wasi ipo siku watu wataishi kiafrika hasa kama wahadzande na waswazi ndo utajua unasema nini. Culture is not religion it is something inborn. Dini unaletewa unasikiliza unakubali lakini kuna siku utasema kumbe nilikosea? Culture huwezi badilisha hivyo waache watu waishi wanavyotaka.
 
Fiesta inashawishi kuongezeka vitendo vya ngono zisizo salama kwa vijana wenye umri mdogo vitendo ambavyo aidha vinachangia kueneza ukimwi ama huwa ni chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani kwa vile mara nyingi malezi ya watoto wanaopatikana kwenye matamasha ya aina hii huachiwa mwanamke pekee , kwa ufupi faida za fiesta ni ndogo kuliko hasara na madhara yaletwayo na tamasha hilo. naunga mkono hoja ya mleta mada serikali ikae chini na kutafakari upya swala hili.
 
Naona Majizo&Co mmehamia kwenye majungu baada ya propaganda na takwimu zenu za kupika kugonga miamba.

Matamasha mangapi nchi hii yanafanyika yenye taswira kama ya Fiesta? Mbona Fiesta Tu ndiyo inatia watu jambajamba?

JembeFm naye kaanzisha Jembeka festival yenye image kama ya Fiesta Tu nyie efm komaeni Tu na hiyo majungu festival si ndiyo uwezo wenu ulipoishia.

NyamaChoma festival...
 
Babu na bibi zako walivaaje au waliowatangulia walivaa je. Mavazi ni tofauti na akili ya mtu. Watu wanafunika nyuso lakini wanapelekea hawara vyakula wengine ndo wanalipua wenzao? Mavazi ni kitu cha kupita. Nani anavaa pekosi siku hizi, nani anavaa turnup siku hizi? Ndo maana mwaka 1974 Kawawa alipotuchania skirt shuleni, Mwalimu alisema msiwasumbue hii ni fashion itapita. Usiwe na wasi wasi ipo siku watu wataishi kiafrika hasa kama wahadzande na waswazi ndo utajua unasema nini. Culture is not religion it is something inborn. Dini unaletewa unasikiliza unakubali lakini kuna siku utasema kumbe nilikosea? Culture huwezi badilisha hivyo waache watu waishi wanavyotaka.
Wewe huwezi vaa kama mpumbavu unaonesha maumbile yako kisa msanii msanii huchwara. Mtu mwenye akili anajua nani nmuoneshe maumbile yangu nani asione

Wasanii wa kiafrika ni kuiga utakuwa binadamu gani wewe copy and paste life ndo style yako. Kutangaza mahawala napo ni maadali ya wasanii

Mi nashangaa mbona cyber crime haiwagusi siwapendi kama non. Wewe imba mbona waimbaji wa taarabu hatujawagusa wanaoshabikia wasanii wanaovaa nusu uchi na kutangaza mahusiano yao ni wafusika wanaofanana

Kuna baadhi ya vyombo vya habari ni kutangaza tu Jana msanii fulani alitoka na fulani ndo maisha nayo eti tuyafurahie mmi nmelelewa baba na mama najua kipi nikipulic kipi cha moyoni

Wasanii wamekuwa miongoni mwa watu wanaobomoa maadili ya vijana kama serikali itanyamazia vyombo vinavyowatangaza then taifa la kesho linaweza lisifae
 
*SERIKALI IPIGE MARUFUKU MATAMASHA YA FIESTA NA MATAMASHA MENGINE YOTE YANAYOZIDI KUMOMONYOA MAADILI YA VIJANA WA KITANZANIA KWA KUENEZA, KUHALARISHA NA KURASIMISHA UHUNI NCHINI*

Na Emphraim Makamba

Kwa hakika Muheshimiwa angejua mambo ambayo huwa yanatokea kwenye matamasha ya Fiesta, ninaamini angeomba siku zirudi nyuma ili abadilishe maneno yake aliyoyaongea kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ikulu.

SABABU kuu ya mimi kuandika waraka huu ni hofu kubwa inayo niandama baada ya kuona matamasha haya yameachiwa kuendelea kutamalaki nchi nzima kwa kuvuka mipaka ya majiji na sasa kuanza kuzitafuna mpaka halmashauri za miji midogo midogo ya Tanzania. Kwa hakika majiji kama Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya, mambo ya kihuni na ya hovyo hovyo imekuwa sasa ni kama moja ya mambo muhimu katika maisha ya watu wahuni ila sasa ninapoona uhuni huu unapelekwa mpaka vijijini siwezi kuendelea kuwa mnafki na kunyamaza kimya. Ninaomba mnisaidie kupaza sauti yangu iwafikie wale wenye mamlaka waliopo kule juu.

Fiesta ni tamasha kubwa la KIHUNI nchini. Mahali popote ambapo tamasha hili linapokuwa likifanyika ni wazi kabisa mambo mbali mbali ya kihuni huwa yanakuwa yakifanyika sambamba na tamasha hilo kabla, wakati na baada ya tamasha.

NUSU UCHI ndio namna ya kuvaa mavazi kwa dada zetu na binti zetu wakati tamasha hili linapofanyika. UKAHABA na UFUSKA ndio mahala pake na hufanyika wazi wazi katika viwanja hivyo na biashara ya ukahaba na madawa ya kulevya hufanyika kupendezesha matamasha haya. Wasanii wanaoimba MATUSI MATUSI katika nyimbo zao ndio hupata nafasi kubwa ya kusherehesha matamasha haya na husafirishwa kwenda kusambaza UCHAFU huo mpaka mikoa ambayo haina hatia na uchafu wa mijini. Fiesta Rukwa, Tabora, Singida, Lindi, Manyara na mikoa midogo midogo mingi mpaka kufikia hali ya kusikitisha sana. Wasanii kama Snura wa chura, ManFongo wa hainaga ushemeji, Shilore na Kanga moko na wasanii wengine wengi wanaosifika kwa mashairi ya kihuni kihuni na kutumbwiza kwa kucheza nusu uchi ndio hupata nafasi kubwa sana ya kusafiri kwenda kusambaza huu UPUUZI katika mikoa yote midogo midogo nchini.

Mwaka 2005 baada ya Rais wa awamu ya nne ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuingia madarakani kwa mara ya kwanza kama mkuu wa nchi, nilipata nafasi ya kukutana na Chief of Staff kwa chakula cha mchana na alitaka kujua nini maoni yangu kuhusu swala la vijana hasa hasa nyanja za utamaduni na maadili. Tuliongea mengi ila nilimwambia kitu kimoja ambacho nilimuomba akichukue kama dira. Nilimwambia kwamba:

*Erick Shigongo* na *Joseph Kusaga* ni vijana wawili nchini wanaotakiwa kudhibitiwa haraka sana kupitia vyombo vyao vya habari vya Global Publishers Limited na Clouds Media Group kabla ya janga kuu la mmomonyoko wa maadili utakaoikumba taifa hili na isipatikane tiba ya haraka kwa muda mrefu. Wote tumeshuhudia namna magazeti ya udaku ya Global publishers yanavyoharibu kwa kasi jamii yetu. Wote tumeshuhudia na tunaendelea kuwa mashahidi wa namna jinsi CLOUDS MEDIA GROUP kupitia vyombo vyake vya habari vya Clouds Fm na Clouds TV vinavyojitahidi kila siku kubomoa kizazi hiki cha vijana wetu wa kitanzania kwa namna mbali mbali mpaka kufikia kuanza kuhamasisha USHOGA kwa kufanya mahojiano na shoga kupitia televisheni hiyo ambayo vijana wengi wanaiangalia na kuipenda. Juhudi na ushauri wangu uligonga mwamba baada ya kuona mkuu ndio kwanza anashikamana na hawa ambao kwangu mimi ninawaita Prime Suspects wa chanzo kikubwa cha kasi ya mmomonyoko wa maadili ya vijana wetu hapa nchini.

Wito wangu kwa serikali ni kwamba, *IT IS NOW OR NEVER* Kama tunataka kuokoa taifa hili la vijana wetu basi tuchukue hatua sasa lasivyo ifafikia mahali tutashindwa kuzuia upuuzi huu kama vile ilivyo kwa mataifa mengi ambayo ni wahanga wa upuuzi huu. Wazazi tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kuwatunza na kuwalea vijana wetu katika maadili safi na bora ya kumcha mwenyezi Mungu lakini pia serikali nayo itusaidie kwa maswala ya kiujumla. Tusikubali UHUNI kuwa sehemu ya utamaduni wetu.

_Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki vijana wetu wote nchini._
SHETANI at work bro
 
Mtoa mada kafafute sayari yako ukaishi na familia yako....... Yadunia hutoyaweza tecnologia inavyokuwa na ndivyo mambo yanavyokuwa haya mambo duniani kote yapo sasa wewe unavyosema yazuiwe wewe kama nani kwenye taifa hili..... Nadhani unachuki zako binafsi na hawa clouds media embu waache vijana wale ujana wao labda wewe muda wako umeshakwisha umekuwa mzee. Lakini dunian kote starehe zipo na zina kuwa na security ya jeshi la porisi...... JPM mwenyewe kasema IMOOOOOOOOOO harafu wewe unakuja hapa unasema HAIMOOOO IFUTWE EBO!
 
Wewe utakuwa huna hela hivyo unaona gere wenzio wanapofanikiwa maadili yameanzia kuvunjika kwa Kusaga na Shigongo baada ya kuanzisha kampuni zao?!!.hili ni suala la dunia nzima.
 
Wewe huwezi vaa kama mpumbavu unaonesha maumbile yako kisa msanii msanii huchwara. Mtu mwenye akili anajua nani nmuoneshe maumbile yangu nani asione

Wasanii wa kiafrika ni kuiga utakuwa binadamu gani wewe copy and paste life ndo style yako. Kutangaza mahawala napo ni maadali ya wasanii

Mi nashangaa mbona cyber crime haiwagusi siwapendi kama non. Wewe imba mbona waimbaji wa taarabu hatujawagusa wanaoshabikia wasanii wanaovaa nusu uchi na kutangaza mahusiano yao ni wafusika wanaofanana

Kuna baadhi ya vyombo vya habari ni kutangaza tu Jana msanii fulani alitoka na fulani ndo maisha nayo eti tuyafurahie mmi nmelelewa baba na mama najua kipi nikipulic kipi cha moyoni

Wasanii wamekuwa miongoni mwa watu wanaobomoa maadili ya vijana kama serikali itanyamazia vyombo vinavyowatangaza then taifa la kesho linaweza lisifae
Usitokwe jasho bure nenda Dodoma ndani uone wamama wa kiafrika na akina baba wa kiafrika wanavaaje. Wewe kama umezaliwa mjini shauri yako. Huko vijijini akina mama matiti nje, watoto midudu nje, akina baba ni kale ka nguo ka kufunika otherwise kila kitu free.
Nenda umang'ati unakutana na yale yale, umasaini, uhadsambe je. Hata wabantu wengine toa wagogo, kuna mahali wasicha wanatembea na magome ya miti kuficha sehemu nyeti. Tatizo hamtembei mnadhani maisha ni mjini tu. Wa mjini wanajitahidi kumodify maisha waliyiacha vijijini. Kama unataka uafrika nenda makumbusho kwanza ujifunze maisha ya waafrika na siyo hayo ya Dar sababu hayana mengi tembelea mikoa yote yenye makumbusho ndo urudi na story yako. Tusichanganye dini na uhalisia. Dini zililetwa utamaduni tulirithi chagua cha kuletewa au chakurithi.
 
Bila shaka una chuki na
*Shigongo (Mzee wa kuikopesha ccm, na kulia lia na maandishi)
*Luge na Joseph kusaga
*Zamarad
Sasa unataka wadhibitiwe ili hawa wakale wapi? Hakuna anayelazimishwa kuhudhuria matamasha yao kama utawalea vyema wanao basi maadili yao yatabaki salama na huko fiesta hawatokanyaga kuuona ufuska, Jitahidi kuwaombea pia.
 
Back
Top Bottom