Serikali inawatapeli wazee

Baba Clara

Member
May 10, 2011
94
27
Chama cha Tanzania legion and Club(TLC) cha maaskari wa K.A.R waliopigana vita ya pili ya dunia wanailaumu serikali kwa kuwatelekeza na kuwaacha wakihujumiwa mali zao.

Tangu chama hiki kianzishwe na kupata usajili mwaka1966 kimekuwa na misukosuko mingi lakini hakuna ushirikiano wa kutosha kutoka kwa serikali ili kuwatetea maslahi yao pamoja na ruzuku ambayo huwa inatumwa kutoka Royal Common wealth Ex-service league(RCEL) lakini hawaipati na wala serikali haioneshi msaada wowote katika kushughulikia hizo pesa bali zinaliwa na wajanja wachache ambao serikali inawafahamu. Wazee wanasema mwaka 2007 katibu mkuu wa RCEL alipo kuja Tanzania alisema pesa zao zitakuwa zinakuja kupitia serikalini hasa wizara ya ulinzi lakini hakuna kipya mpaka leo.

Vilevile jengo lao la kariakoo limefungwa bila wao kuwa na taarifa na vifaa vyao vya ofisi kuibwa pamoja na kuyafikisha malalamiko yao mahali husika lakini hakuna tija yoyote ile mpaka sasa

Naishauri serikali ya Mh. Kikwete rais wetu ahakikishe anawasaidia hawa wazee kwa kufatilia wale wote waliokabidhiwa dhamana ya kuwalea hawa wazee wetu wawajibishwe na yafuatayo yatekelezwe kwani wazee ndio hazina ya Taifa. Serikali tunaiomba ifanye yafuatayo;

  1. Kufatilia ruzuku zinazotumwa kutoka RCEL kwa ajili ya kuwalipa wazee huwa zinaenda wapi?
  2. Kuwarudishia jengo lao la ofisi kwani bado wananguvu na nijengo ambalo kwao ni kitega uchumi.
  3. Vifaa vilivyoibiwa pale ofisini kwao wahusika wakamatwe maana wanafahamika.

DEOGRATIUS KISANDU
KATIBU WA UHUSIANO NA UENEZI TAIFA, KITENGO CHA VIJANA WA NCCR-MAGEUZI.
25/01/2013
 
chama cha tanzania legion and club(tlc) cha maaskari wa k.a.r waliopigana vita ya pili ya dunia wanailaumu serikali kwa kuwatelekeza na kuwaacha wakihujumiwa mali zao.

Tangu chama hiki kianzishwe na kupata usajili mwaka1966 kimekuwa na misukosuko mingi lakini hakuna ushirikiano wa kutosha kutoka kwa serikali ili kuwatetea maslahi yao pamoja na ruzuku ambayo huwa inatumwa kutoka royal common wealth ex-service league(rcel) lakini hawaipati na wala serikali haioneshi msaada wowote katika kushughulikia hizo pesa bali zinaliwa na wajanja wachache ambao serikali inawafahamu. Wazee wanasema mwaka 2007 katibu mkuu wa rcel alipo kuja tanzania alisema pesa zao zitakuwa zinakuja kupitia serikalini hasa wizara ya ulinzi lakini hakuna kipya mpaka leo.

Vilevile jengo lao la kariakoo limefungwa bila wao kuwa na taarifa na vifaa vyao vya ofisi kuibwa pamoja na kuyafikisha malalamiko yao mahali husika lakini hakuna tija yoyote ile mpaka sasa

naishauri serikali ya mh. Kikwete rais wetu ahakikishe anawasaidia hawa wazee kwa kufatilia wale wote waliokabidhiwa dhamana ya kuwalea hawa wazee wetu wawajibishwe na yafuatayo yatekelezwe kwani wazee ndio hazina ya taifa. Serikali tunaiomba ifanye yafuatayo;

  1. kufatilia ruzuku zinazotumwa kutoka rcel kwa ajili ya kuwalipa wazee huwa zinaenda wapi?
  2. kuwarudishia jengo lao la ofisi kwani bado wananguvu na nijengo ambalo kwao ni kitega uchumi.
  3. vifaa vilivyoibiwa pale ofisini kwao wahusika wakamatwe maana wanafahamika.

deogratius kisandu
katibu wa uhusiano na uenezi taifa, kitengo cha vijana wa nccr-mageuzi.
25/01/2013
hii ni serikali ya kufa kufaana
 
Masalia mnatafuta pa kutokea, poleni sana, habari ya Mujini ni gesi, imekula kwako kwa sasa,
 
Back
Top Bottom