Serikali inapoteza mapato katika kituo cha mabasi cha nyegezi

Gluk

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,856
2,954
Habari wanajukwa.
Leo acha niwasanue wasimamizi wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha nyegezi mkoani mwanza.
Huenda hawajui haya au wanajua ila wanafumbia macho

Kwanza wale wanaokatisha tiketi za kuingia ndani kituoni mara nyingi ukiwapa pesa kubwa wanakata shilingi 300 badala ya sh 200 halali na kukwambia kuwa hawana shilingi 100 na kutokana kuwa watu ni wengi na ww una haraka unaamua kuacha hiyo sh 100.
Cha pili baada ya abiria kupewa tiketi ya kuingia ndani kituoni kuna watu ambao kazi yao ni kuchukua zile tiketi na kuzichana, ila hawafanyi hivyo kwa tiketi zote na matokeo yake baadhi ya tiketi hurudishwa katika mzunguko na kuuzwa kwa mara ya pili.

Wahusika chukueni hatua kama mlizochukua katika kituo cha mabasi Magufuli kwa kuweka mfumo wa kadi badala ya tiketi.
Jumapili njema nyote.
 
Hamna ulichosanua ndg,
Kule juu ndipo tatizo lilipo
Ukiona hao wadogo ni hivyo
Tambua kule juu ni zaidi ya hao

Umesahau hii kauli ya mnakula hadi mnavembewa?
 
Hamna ulichosanua ndg,
Kule juu ndipo tatizo lilipo
Ukiona hao wadogo ni hivyo
Tambua kule juu ni zaidi ya hao

Umesahau hii kauli ya mnakula hadi mnavembewa?
Kabsa nchi wezi wengi sana
 
Back
Top Bottom