Anonymous
Senior Member
- Feb 3, 2006
- 124
- 321
Hali ya masoko kwa kweli ni mbaya sana, yaani unaweza kununua bidhaa ukaharibu viatu na ukapata magonjwa mazingira ya masoko yetu. Kila mfanya biashara analipa ushuru wa kuwepo sokoni, hata hivyo inashindwa kubainika hela zinatumikaje? Mbona masoko machafu hadi yanatia kinyaa, na mengine hutoa harufu mbaya kabisa.
Leo nimetembelea soko la Tegeta Nyuki aisee, sijui kama kipindupindu kimetuacha au kinatuvutia kasi tu. Maeneo machafu hata kutembea ni shida. Angalia kama hali ya wauzaji matunda hapa na hayo maji machafu ya pembeni.
Fikiria uchafu huo halafu bado tupo comfortable kununua bidhaa bila kujali afya zetu. Mimi nadhani ni wakati kwa wafanyabiashara kudai matumizi ya fedha za ushuru zinazolipwa kila siku.
Kwa sasa kasi ya magonjwa yasiyoambukiza pia iko juu, kwa uchafu huu magonjwa ya upumuaji yanakosekanaje maana kutakuwa na hewa nzito mfanyabiashara anaivuta kutwa nzima.
Hebu angalia kama hapo, mtu unapitaje, yaani unatoka sokoni kama umetoka shamba miguu imechafuka matope matupu.
Ni kweli tumeshindwa kutumia hela za ushuru kutengeneza mitaro vizuri ili mvua zisilete athari kwa kiasi hiki cha kuhatarisha afya za watu.
Tunasubiri kupindupindu?