Serikali ianzishe Kitengo cha Msaada wa Kisheria kwa Umma, sio Watu wote wanamudu kuwa na Wakili Binafsi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Nchi kuwa na Ofisi au Kitengo cha Umma Cha msaada wa Sheria (Public Pro Bono Office/ Department) ni muhimu ili kuhakikisha Upatikanaji sawa wa Haki. Ofisi ya kutoa msaada wa Kisheria (Pro Bono Services) ni sehemu kubwa na muhimu katika Mfumo wa Haki.

Mfumo huu unawezesha kutoa Ushauri na Uwakilishi wa Kisheria kwa Watu wasioweza kumudu Mawakili binafsi.

Hii inasaidia kudumisha Kanuni kwamba kila Mtu, bila kujali hali yake ya kifedha anastahili kupata Haki. Msaada wa kisheria, unasaidia kuziba mapengo ya Haki yanayotokana na kushindwa kumudu gharama za kuweka Wakili binafsi.

Kwa kutoa Huduma za msaada wa Kisheria, Ofisi au Kitengo cha msaada wa Sheria kitachangia kuzuia hali ambapo Watu wanaweza kuachwa bila Uwakilishi wa kutosha na kupelekea ukosefu wa Haki.

Kwa kuweka Ofisi au Kitengo cha msaada wa Sheria cha Umma, Nchi inakuza Mfumo wa Kisheria wenye usawa zaidi na inachangia katika kutimiza Haki ya ushauri wa kisheria kwa Raia wote kwa kuweka kinga dhidi ya uwezekano wa dhuluma.

Serikali yazindua kituo cha msaada wa kisheria kwa wote Uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia - Singida, 10 Januari, 2024
 
Serikali inavyolipaga watumishi wa umma mshahara mdogo, hao mawakili wataomba hongo mpaka basi.Mtumishi wa TRA tu mwenyewe analipwa pesa ndefu na bado anakula mlungula. Kwa nchi yetu it won't work.
 
Back
Top Bottom