Sera kuu ya CCM ni Dar kwanza, Hongera wamakonde wa Mtwara!!

Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
15,045
5,093
Hivi Kawe na Ubungo mmekosa nini? Ni 'uongo' gani waliwaambia? Au Mnyika na Mdee waliiba kura? Kwa miaka 50 ya uhuru CCM imeifanya Dar kuwa peponi, wanakaa malaika, wenye heri na watakatifu!

Kichwa huuma zaidi kuona CCM inachaguliwa mikoani. Mikoani wanakaa mashetani, misukule na mazimwi kwa mtizamo wa CCM! Mtwara wameanza kujitoa 'usukule', hongera sana japo gharama yake ni kubwa, mmepigwa, mmebakwa, mmeuliwa!

Kwa upendeleo huu wa wazi, si chama pendwa CHADEMA kinachoweza kutuokoa, kwani hata Mbowe ana miradi peponi! Upendeleo wa wazi ni kama:

1. AFYA

Muhimbili iko Dar na wala siyo Dodoma au Singida! Ziada wana Ocean Road, Heart Institute, Temeke, Amana, Mwananyamala! Hadhi ya hospitali za wilaya za Dar ni bora kuliko zetu mikoani kama Kitete pale Tabora

2. USAFIRI

Kila kona ya Dar lami zenye service road! Service road ziko Dar tu, kwa malaika! Barabara zote ziko chini ya TANROADS.

Treni mikoani haziendi ila Dar kila siku zinapiga kazi!

Barabara za mbinguni zinajengwa na magari ya kasi (BRT) kubeba malaika, sisi kule Shinyanga usafiri baiskeli! Kigoma wamelia machozi ya damu kwa miaka 50 ya daraja la Malagarasi, Kigamboni hata hawajaomba linajengwa! Gharama kama mara kumi ya lile ya Malagarasi

3. MAKAZI

Dar umeme upo kila kona, 100%. Kigoma toka uhuru hakuna!! Lindi na Mtwara ni 3%. Shirika la nyumba la taifa (NHC) miradi yake iko Dar tu, jumla ya miradi yote ya mikoani ni sawa na Dar! Shida ya maji Dar ni nafuu kuliko Kigoma wenye mito, ziwa na chemchem. Kanda yote ya ziwa na magharibi hakuna hata kiwanda cha cement kimoja, nobody cares!

Dr. Slaa alizunguka kwa ndege akaona tembe akapaza sauti kushusha bei, CCM kutudhihaki eti nyumba zetu za tembe wanazijenga pale Makumbusho-Kijitonyama kama kumbukumbu!

4. ELIMU

Dar ina vyuo zaidi ya 40 vya elimu ya juu! Mwanza jiji la pili lina vitano tu!
Mwisho: Kauli za mawaziri wetu ndo kero zaidi, mi huwaita mawaziri wa Dar!
*@Anna Tibaijuka: Kigamboni iwe kama London, Jangwani pawe city garden ya kisasa Afrika! Manzese nyumba zibomolewe na kujengwa maghorofa! Dar iwe satellite city!

*Magufuli: Dar ijenge vertical, barabara za juu! Wanaoandamana wapite kwenye lami!-Kibondo je kwa wanaoandamana?

NI DHAMBI KWA MIKOANI KUCHAGUA CCM
__________
Mbowe_ ni m/kiti na KUB kauli yake ikulu lazima wakae vikao
Mnyika_ ni mkurugenzi uenezi na sera CDM
Mdee_ ni waziri kivuli wa ardhi awaambie watoe baadhi ya vyuo Dar na viwanda vijengwe mikoani.
 
Nini hasa mkuu unachotaka kutuambia?

Kindly review it in a summary, so that the objective behind is clearly understood.

CCM inajali Dar pekee mkuu! Mikoani hawana time. Magufuli, Tibaijuka na Mwakyembe wamefanya nini Shinyanga?
 
Nyakageni Umemaliza kulia lia ????
maendeleo hayaji kwa kufukuza wana siasa, kaza buti pamabana
kwani ni karagha bao kama mawazo yako ya maendeleo endelevu unayaweka kwa wanasiasa.
 
Last edited by a moderator:
Sasa mbowe et al mbona hawahusiki na haya malalamiko yako??

Umekisoma vema hichi ulichokiandika kweli??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

mkuu Daudi Mchambuzi! Heshima kwako. Hii ni changamoto kwa m/kiti. Akiongea anasikika. Kwa nini yuko kimya!?
 
Last edited by a moderator:
Nyakageni ,hii nini sasa!?..."baba ni juisi ya mkaa,we kunywa tu baba inaongeza damu"...
 
Last edited by a moderator:
umemaliza kulia lia ????
maendeleo hayaji kwa kufukuza wana siasa, kaza buti pamabana
kwani ni karagha bao kama mawazo yako ya maendeleo endelevu unayaweka kwa wanasiasa.

a human being is a political animal! Hawakwepeki wanasiasa
 
Ha ha ha mleta mada ni haki yako ya msingi lakini hao ulowataja hawausiki na malalamiko yako?na kwanini wafukuzwe jee uwekwe wewe ?hebu soma vizuri mada yako urudi kufanya edit
 
Back
Top Bottom