Separation time: Majira ya kutengana na watu

2 of Amerikaz most wanted

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
1,328
3,692
Majira ya kuhachana na watu, kutengana na kitu au vitu fulani katika maisha yako, sio lazima kutokea ugomvi au Hali yeyote mbaya ndio utengane na vitu au watu fulani katika maisha yako.

Separation wakati mwingine inaweza kutokea kwenye tabia fulani ulizo zizoea au kufanya kitu kwa mtindo fulani muda ukifika inabidi kuhachana na mtindo huo ulio uzoea.

Watu walio fanikiwa wana uheshimu sana huu muda wa separation maana unaepushwa na mambo mbaya, inakuletea fursa mpya.

Sababu za separation

1. Ina mruhusu mungu kuzungumza na wewe. Unapo kuwa pekeyako mungu anazungumza na wewe kupitia amani na mioyo yetu, Unapo ambatana na watu fulani unakosa utulivu na amani ya moyo.

2. Inakusahidia kuona fursa fulani. Unapo ambatana na watu fulani utakutana na sight limitation. Mara nyingi mawazo yetu yanachagizwa na watu wanao tuzunguka na kuelekea kushindwa kuona fursa kubwa zaidi.

3. Separation Inakusahidia kukuunganisha na watu wengine. Watu wapya hawawezi Pata nafasi kabla ya kuwahachilia watu wa amani.

4. Kuexpand. Kuna watu walifanya mambo makubwa baada ya kuhachana na mtu fulani, mfano biashara kuwa kubwa baada ya kuhacha kuwa chini ya mtu fulani au kumshirikiana na mtu fulani.

5. Inakupa muelekeo mpya wa maisha yako. Kuna watu leo hii wangekuwa mbali sana kimaisha lakini wameshindwa kwasababu ya kumng'ang'ania kukaa sehemu moja, kuwa shikilia watu fulani. Wengine walifanikiwa baada ya kuhachana na kampuni ya zamani au bosi wa zamani.

Separation inatusahidia kutuweka salama katika maisha yetu.

Mungu uwaondoa watu wa aina hii wakati wa separation.

1. Watu wenye hidden agenda katika maisha yako. Kuna watu maagent wametumwa kuja kukuchunguza na kujua udhaifu wako hili wa kudondoshea. Mfano anaweza kuwa mpenzi wako ana act anakupenda mwisho wa siku anakurekodi video za uchi Kisha kudai malipo ili hasivujishe au kuku haribia brand yako.

2. Watu ambao sio sahii kwako. Kuna watu katika maisha yako ni wazuri lakini sio sahii kwako, mara nyingi watu hawa wanakuchelewesha kule unakoenda.

3. Destructor . Mungu huwaondoa watu hawa wakati wa separation, unakuta wanakushauri mambo tofauti na unayo takiwa kuyafanyia kazi au wanakuingiza katika circle ya marafiki wapya watakao Kuletea shida mfano kesi kila siku, utapeli nk.

Kuna wakati unaweza kukosa amani na mtu fulani husijilazimishe mungu anakulinda na madhara yatakayo tokea baada kwa kuendelea kumshikilia mtu Huyo au kazi fulani.

Source joel nanauka
 
Back
Top Bottom