Selasini: Polisi haina tofauti na UVCCM, Ben Saanane ni wa Rombo na Watu wa Rombo tutaamua..

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,022
Mh.Selasini namchukulia kama mmoja wa viongozi moderates na wenye uvumilivu ndani ya CDM.

Sasa kama imefika mahali hata yeye anazungumza kwa uchungu kama anavyoonekana ktk video hapo chini basi nalazimika kuamini kwamba hali siyo nzuri.

Kwa kweli inabidi kila mtu ktk nafasi yake ajitathmini ni wapi tunakosea.

Mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini, amemtahadharisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro kwamba wananchi wa jimbo lake hawajasahau tukio la Msaidizi wa Mbowe aliyepotelea kusikojulikana kwani bado wana hasira inayofukuta na kwamba

rabiu%20saanane.jpg

hautaisha pasipo kufanya maamuzi.

Mhe. Selasini amesema kwamba yeye kama Mbunge wa Rombo na Ben Saanane akiwa ni mpiga kura wake analitaka jeshi la polisi pamoja serikali waweze kutoa ripoti ya kijana huyo kama bado yupo hai au ameshafariki ili wafanye matanga vinginevyo wao wataamua wenyewe cha kufanya.

"Nataka nimwambie IGP Sirro na watanzania wote kwa ujumla ipo siku warombo tutaitana kufanya maamuzi, nataka niwaambie warombo damu ya mwenzetu haiwezi kupotea Halafu sisi tukakendelea kukaa kimya kama wajinga, Lazima tufanye maamuzi sahihi. Vijana wa Rombo popote pale mlipo nataka kuwaambia mwaka huu hautaisha lazima tukutane tuamue juu ya mwenzetu".... Selasini amesema

selasini%20Joseph.JPG

Hata hivyo Mbunge huyo ameeleza kwamba familia ya Ben Saanane imekuwa na huzuni tangu kupotea kwa kijana wao ambapo mpaka sasa jeshi la polisi halijawahi kutoa ripoti tangu taarifa za kupotea kwake zilipotangazwa

Hata hivyo amesema kwamba kadiri watanzania wanavyoendelea kuteseka ndivyo ambavyo wanaendelea kukomazwa hivyo hali hiyo siyo njema kwa afya ya nchi kwani itafika kipindi kwamba nchi italipuka.

Ben Saanane ambaye alikuwa Msaidizi wa Mwenyekiti Freeman Mbowe, tangu kuripotiwa kupotea kwake ni takribani mwaka sasa ambapo si familia, jeshi la polisi au Chama chake wanajua ni wapi alipopotelea huku chama chake kikiendelea kuliomba jeshi la polisi na serikali kufanya uchunguzi kuhakikisha anapatikana.
 
Mh.Selasini namchukulia kama mmoja wa viongozi moderates na wenye uvumilivu ndani ya CDM.

Sasa kama imefika mahali hata yeye anazungumza kwa uchungu kama anavyoonekana ktk video hapo chini basi nalazimika kuamini kwamba hali siyo nzuri.

Kwa kweli inabidi kila mtu ktk nafasi yake ajitathmini ni wapi tunakosea.

Noted
 
Kila ninapokutana na mdogo wake Ben huniuliza "hujasikia hata tetesi alipo kaka yangu "

Na anayoongea Selasini ni kweli, kuna wakati marafiki wa Ben walipanga wakutane sehemu fulani walipofika hapo walikuta defender ya polisi na polisi wakiwa hapo
 
Aise hii ni hatari,ila tusubirie majibu ya polisi maana watakuja na kumkamata.
 
Mh.Selasini namchukulia kama mmoja wa viongozi moderates na wenye uvumilivu ndani ya CDM.

Sasa kama imefika mahali hata yeye anazungumza kwa uchungu kama anavyoonekana ktk video hapo chini basi nalazimika kuamini kwamba hali siyo nzuri.

Kwa kweli inabidi kila mtu ktk nafasi yake ajitathmini ni wapi tunakosea.

Anayosema Mbunge huyu mengi yalihitaji majibu miaka mingi iliyopita kwa viongozi tofauti. Kwa nini tulikaa kimya kwa miaka yote na leo hii ndo tunasema tumechoka? Kifo cha mtu au mtu kupata kilema cha kudumu haihitaji wengine wachoke ndo mambo yapate ufafanuzi. Namsikia mtu huyu akisema Wangwe pia aliuwawa! Jambo hili halijawahi tamkwa na tulielewa ni ajali ya kawaida na hata dereva kupata adhabu. Kumbe aliuwawa na waliofahamu wakakaa kimya!

Ninachokiona kwa wa-TZ kumbe ukiwaacha na maisha yao ya rushwa, ufisadi, wizi, dili mitaani, nk. hakuna atakayekuuliza juu ya mambo machafu kama haya. Wewe iba na wao waruhusu waibe, hakuna tatizo. Leo tumebanwa ndo maana sasa ni kukosana kila mtu anakuwa mtu shujaa wa kusema kila kitu alichokifahamu!
 
Back
Top Bottom