Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya kupotea kwa uzalendo miongoni mwa watanzania kutokana na tabia na mienendo mbalimbali iliyokuwa na inayoendelea kujitokeza.Mengi yamezungumzwa na kutafsiriwa kama ni ukosefu wa uzalendo hasa yanapojitokeza kwenye nyanja za kisiasa katika mikutano,washa,makongamano na hata bungeni.
Kuelekea mwishoni mwa miaka ya 1990 tulishuhudia kusimamishwa kwa uchukuaji wa vijana wa JKT kwa mujibu wa sheria kwa sababu zilizotolewa kwa wakati huo lakini miaka ya hivi karibuni baada ya serikali kung'amua mmomonyoko wa maadili na ukosefu wa uzalendo miongoni mwa vijana ,serikali iliamua angalau baadhi ya vijana wanaohitimu elimu ya juu ya sekondari huchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria .Tuna imani hapo baadae wote wanaohitimu watashirikishwa kwenye mafunzo hayo.
Kati ya mwanzoni mwa miaka ya 1970 na miaka ya 1990 sekondari ya wavulana ya Tabora maarufu kama Tabora Boys' ilikuwa ni shule inayochukua vijana kutoka kila mkoa wa Tanzania ambapo mbali ya kufundishwa masomo ya kawaida ,vijana walifundishwa na kuiva kikamilifu katika masuala ya siasa na ulinzi wa nchi yao na ni vijana waliokuwa wamejaa uzalendo wa dhati kwa nchi yao kwa muelekeo na vitendo vyao.
Siyo kwa uzalendo huu wa sasa wa watu kujinasibu wenyewe wakati wa mchana lakini ifikapo usiku hubadilika .Matunda ya vijana hao wa miaka hiyo kutoka Tabora Boys' yanaonekana mpaka sasa kwani wengi ni viongozi katika taasisi ,makampuni ,taasisi za elimu ya juu,makamanda wakubwa katika majeshi yetu nakadhalika wakiwa bado wamejawa na heshima ya uzalendo wa nchi yao.
Tunaiomba serikali kwa jinsi ilivyofikiria umuhimu wa kuanzisha tena mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria basi ione tena umuhimu wa kuirudisha shule ya sekondari ya wavulana Tabora katika mfumo wake ule ili tuendelee kuzalisha vijana wenye maadili mazuri na wenye uzalendo kwa Taifa lao.