Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,623
Wanabodi,

Hii ni sehemu ya pili, au muendelezo wa ile Makala yangu ya "Kwa Maslahi ya Taifa na Pascal Mayalla", ambazo zinachapishwa kwenye Gazeti la Raia Mwema la kila siku za Jumatatu.

Makala hii ni swali, la Jee Bunge linajipendekeza kwa serikali?, na sio statement, kuwa Pascal Mayalla, amesema Bunge Linajipendekeza kwa Serikali!.

Nimeuliza swali hili kwa mujibu wa haki zilizotolewa kwenye ibara ya 18 ya Katiba yetu za uhuru wa kujieleza, na kutoa maoni, Freedom of Expression, ila maoni hayo yasiingilie na kukiuka uhuru wa mtu mwingine.

Sehemu ya kwanza ni hii Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?

Leo naendelea na sehemu ya pili ya makala hii ambayo ni swali, ikiuliza Jee Bunge letu linajipendekeza kwa serikali?. Katika sehemu ya kwanza wiki iliyopita, nilisema wazi kuwa hili ni swali, na jibu lake, sitalitoa mimi, ili nisije nikaitwa katika Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, na kuambiwa nimelidhalilisha Bunge. Ninachofanya hapa ni kukuwekea tuu tukio lilitokea, kisha wewe msomaji ndio ufikie uamuzi kama Bunge letu, linajipendekeza au laa, na wajuvi wa hoja hii wawe huru kupangua hoja kwa hoja, kama ni kweli linajipendekeza, au halijipendekezi!.

Na kwa vile mhusika mkuu wa huku kujipendekeza kwa Bunge kunakozungumziwa hapa ni Mhe. Spika, then naamini mjadala huu utafungwa kwa taarifa rasmi kutoka kwake au kutoka Bungeni kuwa Bunge halijipendekezi.

Rais Anauwezo Wa Kuunda Tume, ni Tume ya Rais. Ana Uhuru Nayo.
Rais wa JMT anauwezo wa kuunda tume kuchunguza jambo lolote, hii ni tume ya rais. Matokeo ya tume hiyo, yanawasilishwa kwake. Kwenye Tume ya Rais, rais ndie mwenye uhuru ama atangaze matokeo ya tume hiyo, au asitangaze, na kwenye mapendekezo ya tume hiyo, rais yuko huru kuyapokea mapendekezo ya tume hiyo, kuyakubali yote kama yalivyo au kuyakubali baadhi, au kuyakataa yote na hakuna mtu yoyote wa kumuuliza chochote kwa sababu hiyo ni tume yake!. Kwenye hili la Tume za rais, tumshukuru sana rais Magufuli kwa kuwa muwazi zaidi, kwa kutangaza wazi matokea ya Tume zake, kule nyuma zimeundwa tume kibao na hakuna ajuaye matokeo ya tume hizo. Katiba yetu imempata rais wetu mamlaka ya kuteua wasaidizi, na inaelekeza kwenye baadhi ya maamuzi, rais atashauriana na wasaidizi wake, lakini katika kufikia maamuzi, katiba hiyo imempa rais wetu mamlaka ya kufikia maamuzi yeye mwenyewe peke yake bila kufuata ushauri wowote wa mtu yoyote. Hivyo uamuzi wa rais Magufuli kuyapokea mapendekezo ya Tume ya Bunge na kukubali kuyatekeleza kwa asilimia 100% chini ya 100 ni kwa hisani tuu na sio wajibu, lakini angepelekewa azimio la Bunge, kulitekeleza sio hisani ni wajibu. Kitendo cha rais kupelekewa maoni badala ya azimio kunamaanisha Bunge linafanya kazi kubwa, nzuri, halafu linasubiri hisani tuu ya rais. Huku tukuiteje?.

Kamati Teule ya Bunge Sio Kamati ya Rais, Ushauri wa Kamati Teule Sio Ushauri Kwa Rais, ni Ushauri kwa Bunge.
Kamati Teule ya Bunge inapofanya uchunguzi, kamati hiyo inakuwa na nguvu za kisheria na hadhi ya kimahakama, Quasi Judicial Committee, kama ilivyo mahakama inaposikiliza kesi au shauri, ikimaliza kusikiliza kesi, inatolewa hukumu, hukumu ikiishatoka inafuatiwa na utekelezaji, hivyo taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, na mapendekezo yake, sio ushauri kwa rais, ni ushauri kwa Bunge, ni kama kuendeshwa kwa kesi, taarifa hiyo ilipaswa iwasilishwe bungeni ili mapendekezo hayo yajadiliwe na kutolewa hukumu kupitia Azimio la Bunge, azimio hili likitoka, linakuwa ni hukumu kwa serikali kulazimishwa kulitekekeza au kulipinga, kama ilivyo amri ya mahakama, utekelezaji wa maazimio ya Bunge, ndipo angepelekewa rais hapa sasa rais hapelekewi kama ushauri kusubiri hisani, bali hupelekewa kama azimio la Bunge, hii ni amri, sio kama ule ushauri wa rais kuwa huru kuufuata au kuupuuza, azimio la bunge ni amri kwa rais kuitekeleza kama amri ya mahakama!. Hapo ndipo Bunge linapoidhibiti serikali kwa kuiamrisha kutekeleza maazimio ya Bunge kwa amri na sio kwa ridhaa tuu! yaani sio at Presidents pleasures, but it is a must, na asipotekeleza, Bunge linaweza kukutana na kuhitaji maelezo na ikibidi kumuondosha rais madarakani!.

Uwezo wa Bunge na Kamati Zake
Bunge limepewa mamlaka na uwezo wa kutunga sheria yoyote, ila bunge kabla halijaitunga hiyo sheria, sheria hiyo inayopaswa kutungwa lazima kwanza ianzie kwenye "the Executive" na Bunge likiisha itunga hiyo sheria, sheria hiyo haiwi sheria hadi Mkuu wa "the executive" yaani rais, aridhie!, na kuisaini, "accent" asiposaini haiwi sheria!. Hivyo kwenye uwezo wa Bunge kutunga sheria, bunge ni kikaragosi tuu, the real powers lies with the Executive!. Bunge likitunga sheria, rais anaweza kuikataa na kuirudisha bungeni waibadilishe, wabunge wakigoma, then rais analivunja Bunge. Bunge linaelezwa linayo mamlaka ya kumuondoa rais madarakani, "impeachment" na rais anaelezwa kuwa ni sehemu ya Bunge!, ila huyu rais amepewa mamlaka ya kuliunda bunge, kulivunja bunge wakati wowote!. Hivyo hata ikitokea tukampata rais dikiteta wa ukweli, akavunja Katiba na Bunge likaamua kumuondosha madarakani kwa impeachment, rais atalivunjilia mbali Bunge kabla halijamuondoa!.

Ingawa Mkuu wa Mhimili wa Bunge ni Spika, ambaye anachaguliwa na wabunge, Mtendaji Mkuu wa `Bunge ni Katibu wa Bunge, rais ndie anayemteua mtendaji Mkuu wa Bunge, kuna kitu kinaitwa nguvu, mamlaka na madaraka, kati ya spika na katibu wa Bunge, Spika kama mkuu wa mhimili wa Bunge, ana Mamlaka makubwa tuu ya kupiga kelele bungeni, lakini nguvu na madaraka ya kuendesha bunge kiuwezeshaji, ni Katibu wa Bunge, Spika lazima anyenyekee na kumpigia magoti katibu kumuomba fedha za uendeshaji, kama walivyo mawaziri lazima amnyenyekee Katibu Mkuu wake, where money lies, its where the real powers lies!, ndio maana imeelezwa mahali kuna mhimili uliojichimbia chini zaidi.

Bunge Linapaswa Kuwa Independent
Bunge lilipaswa kuwa independent kuisimamia serikali, ikiwemo wabunge wasiwe mawaziri ili kuisimamia kikamilifu kabisa serikali kiukweli kweli haswa kama alivyopendekeza Warioba!, lakini wabunge wetu ambao tuliwachagua wakaisimamie serikali, ndio hao wamepewa uwaziri, ambao huku mtaani tunaita "ulaji!", kuna cha usimamizi tena hapo?!, unaweza kumlinganisha Dr. Mwakyembe yule wa Kamati Teule ya Richmond na Mwakyembe huyu waziri?!, au umlinganishe Prof. Kabudi yule wa Tume ya Warioba na Prof. Kabudi huyu waziri?. Msimamizi unapopewa ulaji kwa hisani tuu, unategemea utasimamia kuukata mkono unaokulisha?, au kulikata tawi la mti uliolikalia?, hivyo hiyo japo independence of the parliament kwa Tanzania is just likeva myth, lakini Bunge lionyeshe makali yake katika kuisimamia serikali kwa vitu vya kuonekanika.

The Myth of "The Doctrine of Separation of Powers and Checks and Balances",
Kiukweli hii doctrine "The Doctrine of Separation of Powers and Checks and Balances", ilikuwa iko supposed kuwepo kiukweli ukweli, ila kiuhalisia, hakuna kitu kama hiki, its just a myth, serikali ndio kila kitu!, hakuna mahali popote bunge na mahakama zina total independence!, serikali ndio mambo yote, hivyo hili Bunge letu, ni Bunge ni kama Bunge zuga tuu mbele ya serikali, na hizi mahakama zetu, ni kama mahakama zuga tuu mbele ya serikali, serikali ndio mambo yote!, sasa inapotokea hivyo vyombo viwili ambavyo vyote ni lama zuga tuu vinataka kupimana ubavu kwa jambo ambalo mtuhumiwa mkuu ni serikali, unategemea nini?.

Hili Swali la Bunge Kujipendekeza Kwa Serikali, Lina Hoja Kweli?
Wengi kati ya yote niliyowahi kuyashuhudia katika hoja hii ya the separation of powers, na Checks and Balance, kubwa kuliko ni hili la Bunge kuonekana kama kujipendekeza kwa serikali, kwa sababu Bunge linawajibu wa kuisimamia serikali, kamati teule za Bunge huundwa pale serikali inapofanya madudu, taarifa ya kamati teule ya Bunge ni taarifa ya mhimili wa Bunge na sio taarifa ya yule yule aliyefanya madudu, yaani serikali, na inapaswa kuwasilishwa Bungeni, na mapendekezo yake, kisha waheshimiwa wabunge waijadili na kuyakubali mapendekezo, kuyapunguza, au kuyaboresha, kisha linatolewa Azimio la Bunge ambalo sasa ndilo linalopaswa kuwasilishwa serikalini kwa utekelezaji wa lazima. Kitendo cha taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuwasilishwa kwa rais Magufuli, sio jambo la kawaida ndio maana nimeuliza, huku sio kujipendekeza?.

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge inapaswa kuwasilishwa Bungeni na kujadiliwa

122.-(1) Kamati Teule itatoa taarifa Bungeni kuhusu maoni na uchunguzi wake pamoja na kumbukumbu za ushahidi uliopokelewa na vilevile inaweza kutoa taarifa maalumu juu ya mambo yoyote ambayo itaona yanafaa kuwasilishwa Bungeni. (2) Taarifa ya Kamati Teule itawasilishwa Bungeni na Mwenyekiti. (3) Iwapo baada ya hoja kutolewa, Bunge litaamua kujadili taarifa hiyo, hoja itakayotolewa Bungeni itakuwa ni kwa madhumuni ya kuliomba Bunge likubali mapendekezo yaliyomo katika taarifa hiyo. (4) Bunge linaweza kuamua vinginevyo kwa kutumia utaratibu wa kubadilisha hoja ambao umeelezwa katika Kanuni ya 57 ya Kanuni hizi. (5) Katibu wa Kamati Teule ataweka kumbukumbu zinazoonesha majina ya Wajumbe waliohudhuria mikutano ya Kamati na maamuzi yaliyofanyika.

Kwa kumbukumbu zangu, please correct me if I'm wrong, Taarifa iliwasilishwa kwa mujibu wa kanuni 122 (2), baada ya kuwasilishwa, ilibidi kanuni 122 (3) ifuatwe kwa Bunge kujadili, hapa linazungumzwa Bunge ndilo lililopaswa kuamua kujadili au la na sio spika kuamua!, kumbukeni Spika ni Spika na Bunge ni Bunge, Spika hawezi kujigeuza yeye ndio Bunge na kuzuia taarifa ya kamati teule isijadiliwe Bungeni!. Spika alipaswa kuliuliza Bunge lijadili, na kama kama kuna hoja kuwa taarifa hiyo isijadiliwe, then ingetumika kanuni ya 122(4) ambayo inaliruhusu Bunge kutojadili na kuibadilisha hoja.

Kama Spika ametumia kanuni 122 (4) ya Bunge lisijadili, then uamuzi huu ungefuata kanuni ya 57 ya kubadilisha hoja kwa kuibadili jina isiitwe tena kuwa Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, bali ibadilishwe hoja iitwe Taarifa ya Kamati ya Rais, na itawasilishwa kwa rais, na sio tena Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, kwa sababu taarifa ya Kamati Teule inawasilishwa na kujadiliwa na Bunge, taarifa ya rais ndio inakabidhiwa kwa rais.

Ili hili liweze kufanyika, ingebidi kanuni hii ifuatwe
57.-(1) Hoja ikishatolewa ili iamuliwe inaweza kubadilishwa kwa:- (a) kuondoa maneno fulani kwa ajili ya kuingiza maneno mengine; (b) kuondoa maneno fulani bila kuongeza mengine; au (c) kuingiza au kuongeza maneno mapya.

Sina kumbukumbu ya hili kufanyika na sikusikia likiripotiwa na media yoyote!. Kwa vile Bunge letu linafanya baadhi ya mambo kwa kujifungia, kama hili lilifanyika lakini halikuripotiwa, then taarifa iliyowasilishwa kwa rais, ilipaswa iwe na jina jingine!, Tangu lini rais ambaye sio mbunge akapokea taarifa ya Kamati Teule ya Bunge badala ya kupelekewa Azimio la Bunge?!.

Wabunge wetu walilikubalije hili la Spika kujigeuza Bunge na kuamua kwa niaba ya Wabunge wote, huku waheshimiwa Wabunge wetu wakiwa wanaangalia tuu, like worshipers waiting for their priest, longed to hear him pray, play their minds away?!. Kama Spika ndiye mwenye uwezo wa kuwafahamu wabunge wote, their abilities and capabilities, halafu Spika huyo anapiga simu kwa rais Magufuli kumuuliza nimteue nani kuongoza kamati hii?!, nanukuu hapo Spika alipopiga simu "Mh spika, nakumbuka ulinipigia simu ukaniuliza utachagua nani?, nikakujibu Mungu atakuongoza", then huku sii kujipendekeza?, kwa maoni yangu, huku ni zaidi ya kujipendekeza!, ni kama kujikomba!. (Mhe rais Magufuli naye ni muwazi sana!). Sasa kama Spika anapeleka kwa rais Ripoti ya Kamati Teule badala ya kumpelekea Azimio la Bunge!, kitendo hiki tukiiteje?. Kiukweli mimi binafsi nimemkumbuka sana Spika Sitta (RIP), mzee wa SS, Speed and Standars!. Kwa maoni yangu, Spika wa sasa Mhe. Job Ndugai ndie awe spika wetu wa mwisho asiye mwanasheria!.

Bunge la Ajabu, Wabunge wa Ajabu, Mnatupeleka Wapi?.
Tukisema Bunge letu ni Bunge la ajabu, tutakuwa tunalionea?, tukisema baadhi ya Wabunge wetu ni wabunge wa ajabu, tutakuwa tunawaonea?!. Nimepitia kanuni za Bunge, sikufanikiwa kuona popote ni kanuni ipi ilitumika kuiwasilisha ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kwa rais!.

NB. Bunge pia linayo mamlaka ya kutengua kanuni yoyote ili kufanya jambo lolote lililo inje ya kanuni, sikumbuki kama kulifanyika utenguaji wowote wa kanuni, kuruhusu ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuwasilishwa kwa rais bila kujadiliwa na Bunge na kutolewa Azimio la Bunge.

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG, serikali imefanya matumizi kadhaa bila kuidhinishwa na Bunge, jee Bunge letu limefanya nini?, tukisema Bunge letu limeshindwa kuisimamia serikali kutokana na kujipendekeza kwa serikali, tutakuwa tunalionea Bunge?.

“Wee Washughulikie Huko, Wakija Huku Nitawashughulikia!”.
Mhe Rais aliwahi kumpongeza Spika wa Bunge kwa kuwashughulikia Wabunge na kumuamuru "Wewe washughulikie huko, wakija huku mimi nitadeal nao”, hivi kuna mbunge yoyote aliwahi kutaka ufafanuzi, huko kushugulikiwa huku nje ni kushughulikiwa vipi?!. Msikilize mwenyewe



Wabunge Ndani Wanashughulikiwa Ipasavyo na Huku Nje Wanashugulikiwa Kikamilifu!.
japo haikufafanuliwa wabunge washughulikiweje, au kivipi, lakini kinachoonekana ni kweli wabunge kule ndani ya Bunge, wamekuwa wakishunguliwa ipasavyo, na hata makazi rasmi ya waheshimiwa Wabunge ambalo ni kama eneo la Bunge, pia wanashughulikiwa!, tumeshuhudia wabunge wakikamatwa bungeni bila taarifa kwa Spika!.

Japo mimi siamini jinsi Lissu alivyoshughulikiwa ndiko kushughulikiwa kwenyewe!, Lissu yeye ameshambuliwa na watu “wasiojulikana”, ila huku nje, kiukweli kabisa, kila mwenye macho, anaona jinsi baadhi ya wabunge wanavyoshughulikiwa kikamilifu!.

Baada ya kutoa hoja hizo, namalizia kwa kusisitiza kuwa
Haya ni maoni yangu binafsi yenye swali kuu la msingi kama jee bunge letu linajipendekeza kwa serikali, nikitaraji kupokea majibu, ama ni kweli linajipendekeza, au sii kweli, bunge letu halijipendekezi. Jibu la mwisho likiwa Bunge ni halijipendekezi, then Bunge letu na Wabunge wetu waendelee kuchapa kazi tuliowatuma kule Mjengoni, Bungeni Dodoma na kwenye majimbo yao. Lakini jibu likiwa Ndio Bunge linajipendekeza, then hapa tutahitaji mjadala wa kina, tufanyeje ili Bunge letu la Tanzania litimize wajibu wake ipasavyo ikiwemo kuisimamia serikali na sio kujipendekeza kwa serikali?.

Mungu Ibariki Tanzania
Wasalaam

Paskali
 
Mkuu umejipanga vizuri.. na hoja zako katika mfumo wa swali ni nzito.

Uzi huu na udumu, uje kusomwa na vizazi vijavyo. Kabla historia haijapotoshwa.

naibu spika na katibu wa bunge wote ni wateule wa Mh. Rais... hapo watawezea wapi kumwajibisha.

sisi tuliopata kuishi kwenye awamu hii ya tano, ya bunge la mh. Ndungai, hatutaacha kusimulia vizazi vijavyo.. kuwa "tulikuwa na Bunge la ajabu haijawahi kutokea."
 
Binafsi nimepitia hoja zako zote hizo naona umetoa mawazo yako vizuri tu sijaona polipo na shida labda wao watawala wanalengo lao ambalo wamekusudia kulifanya ktk Taifa hili kwa maelezo hayo kwa nini uhojiwe? Tunafurahia uongo wakati wa kuapa tumeshika vitabu vya dini tukimalizia uongo mwiko kwangu, mi niseme mkuu upo vizuri tatizo tupo kwenye dora linalokumbatia maovu.
 
Mkuu Pascal Mayalla watu wamekutahadharisha humu kuhusu nyendo zako. Nami ngoja nirudie. Inabidi uwe makini mno unapokuwa kwenye hadhara yoyote ile. Kinywaji chako usikiache kikacheza pekee yake. Matembezi yako hasa saa za usiku usiwe pekee yako na usikubali kuhojiwa popote pale kama huna mtu wako wa karibu au lawyer.
 
ni aibu kwa bunge kutoa madaraka yake kwa mihimili mwngne.wanajisahau mpaka wanamwomba mweheshmiwa rais awaletee upinzani mpya kana kwamba rais ndyo anawateua wabunge ni aibu aibu aibu kwa bunge ambalo halijui wamefikafikaje pale..hawana uwezo kabisa ni bora wafutwe tuokoe pesa zetu.madiwani na rais kwnye uchaguz wanatutosha.aibu aibu aibu kwa bunge letu
 
Ninachofanya hapa ni kukuwekea tuu tukio lilitokea, kisha wewe msomaji ndio ufikie uamuzi kama Bunge letu, linajipendekeza au laa, na wajuvi wa hoja hii wawe huru kupangua hoja kwa hoja, kama ni kweli linajipendekeza, au halijipendekezi!.

Jambo la msingi katika swali lako ni kutoa tafsiri ya neno "kujipendekeza" kwa mapana. Je, una maanisha "independence" au "autonomy"?
 
pasco mm napendekeza bunge lifutwe kabisa tuokoe mabilion wanaochukua nibora tuwawezeshe madiwani na rais wanatosha.hawana uwezo wakusimamia serikali.tuangalie mbeleni huko labda watatokea kina lisu wengi bungeni kuliko hawa wanaotafuna pesa zetu bure huku hawaelewi wajibu wao
 
Back
Top Bottom