Scandnavia Bus Ltd: THE END

Watu

JF-Expert Member
May 12, 2008
3,231
1,470
Kuna tetesi ile kampuni ya mabasi iliyoanza kwa kishindo ya Scandnavia Express yaelekea ukingoni.

1. wamesimamisha hudauma zote za usafiri wa mabasi
2. wafanyakazi wote wamepewa likizo ya miezi mitatu.
 
Ni kawaida..........hata UFI ilifilisika itakuwa scandinavia bana!!
Mbona hata ATC (L) inafilisika...........ina ndege moja tu kimeo. na madeni lukuki.
 
Ukiona hivyo, ujue walisimamia miguu isiyo na strategic plan, biashara za opportunism. Kumbuka ilianza kusinyaa Mr Zero aliposemekana kutoa hisa zake ili apate pesa ya kugombea urais wa Jamhuri. Alipopiga mweleka ndio ukawa mweleka wa mende kwelikweli. Waliaminiwa na serikali kwa sababu wenye hisa kubwa walikuwamo serikalini.
 
Kumbuka ilianza kusinyaa Mr Zero aliposemekana kutoa hisa zake ili apate pesa ya kugombea urais wa Jamhuri. Alipopiga mweleka ndio ukawa mweleka wa mende kwelikweli.

Duh! Mr Zero anaonekana akizunguka town kwenye Toyota cresta Exeed ya 1999 ndio huwo mweleka? jamaa nampa Big UP kwa kuachana na shangingi(4X4). sio kawaida EX-PM
 
Abdulla, ameingia kwenye biashara nyingine kama ya maji na nafaka (diversification), halafu mengi yalikuwa ya mikopo na alishindwa kuhudumia ile mikopo na ndiyo maana mengine alimpa mwarabu mwenzake Mohamed Trans (Mohamed Trans amenyanyukia kwenye magari ambayo Abdulla either kamwuzia au alihamishia kwake ili kukwepa kodi, etc)
 
So sad kwa kampuni kama hiyo ilipokuwa imefikia

RIP

Usidanganyike na rangi ya chai, UTAMU wa chai ni sukari sio rangi yake

Sawa kabisa!!!! chai inaleta ladha tu! lakini utamu upo kwenye sukari sio??
 
ha ha haha,unanikumbusha mbali,kuna siku moja gari liliondoka kituoni na abiria wasiozadi watano tu.
 
R.I.P Scandnavia Express! Pia pamoja na kuwa na big shots watatu ambao waliondoa hisa zao au magari yao pia mikopo ilikuwa ni mingi na magari yake yalikuwa yamekamatwa mwaka 2008/2009 na kuwekwa yard pale Temeke ili kunadiwa. At the same time, from the reliable sources, yule mganga wake wa kienyeji ambaye pamoja na kutambikia mambo fulani fulani na ni lazima kwa mafanyakazi kufa kila mwaka head office ghafla na kuanza kutokwa na damu every opening of the body alifariki!!!!. Jamani tutumie elimu ya ujasiriamali na bishara zaidi ya mazindiko!!! Huwa hayalipi!! ni madhara kwa familia au wafanyakazi! Imagine kuna a true strory mkinga mmoja last month alimua mtoto wa dada yake wa damu kwa ajili ya zindiko, maiti ilileta kasheshe maana dada mtu alijua fika mtoto kauliwa na kaka yake kwani alijaribu kumuua mtoto mwingine wa huyo dada ikashindikana!! Alipopata mwanya tu huyu wa pili alipoenda kwake akamuua. Ilibidi wazee wa kikinga waombe sana yule dada apokee maiti na kuzika. Baada ya maziko mkinga pesa iliingia na sasa ameshanunua site 3 Kariakoo anajenga ghorofa na duka la ngua ni balaa!!! But yote hayo yana mwisho jamani, kwa nini uwe na fedha za masharti?

Na huko Mbeya nako kuna mganga mmoja ambaye yeye hutumia kuku kula punze za mahindi. Anaahidi kukupatia utajiri ambao ni sawa na idadi za punze za mahindi atakazoweza kudonoa na kumeza kuku wake wa uganga. Ni hivi anamwaga punze nyingi za mahindi chini, anamchukua kuku ili adonoe akidonoa kumi jua kuwa utapata utajiri babukubwa kwa miaka kumi halafu utakufa!!! Kuna jamaa alienda kuku akadonoa punze moja tu na kweli akapata utajiri kwa mwaka 1 na kufariki!!! Sasa yote ya nini kujitoa kafara mwenyewe au ndugu zako. Struggle hard, with determination you will win!!!
 
Mbeya.....
Home sweet home...
Kweli wako advanced kwenye sayansi pori.

na huko mbeya nako kuna mganga mmoja ambaye yeye hutumia kuku kula punze za mahindi. Anaahidi kukupatia utajiri ambao ni sawa na idadi za punze za mahindi atakazoweza kudonoa na kumeza kuku wake wa uganga. Ni hivi anamwaga punze nyingi za mahindi chini, anamchukua kuku ili adonoe akidonoa kumi jua kuwa utapata utajiri babukubwa kwa miaka kumi halafu utakufa!!! Kuna jamaa alienda kuku akadonoa punze moja tu na kweli akapata utajiri kwa mwaka 1 na kufariki!!! Sasa yote ya nini kujitoa kafara mwenyewe au ndugu zako. Struggle hard, with determination you will win!!!
 
Na huko Mbeya nako kuna mganga mmoja ambaye yeye hutumia kuku kula punze za mahindi. Anaahidi kukupatia utajiri ambao ni sawa na idadi za punze za mahindi atakazoweza kudonoa na kumeza kuku wake wa uganga. Ni hivi anamwaga punze nyingi za mahindi chini, anamchukua kuku ili adonoe akidonoa kumi jua kuwa utapata utajiri babukubwa kwa miaka kumi halafu utakufa!!! Kuna jamaa alienda kuku akadonoa punze moja tu na kweli akapata utajiri kwa mwaka 1 na kufariki!!! Sasa yote ya nini kujitoa kafara mwenyewe au ndugu zako. Struggle hard, with determination you will win!!!
Wajameni!! siyo punze ni PUNJE!!!!cmon!
 
R.I.P Scandnavia Express! Pia pamoja na kuwa na big shots watatu ambao waliondoa hisa zao au magari yao pia mikopo ilikuwa ni mingi na magari yake yalikuwa yamekamatwa mwaka 2008/2009 na kuwekwa yard pale Temeke ili kunadiwa. At the same time, from the reliable sources, yule mganga wake wa kienyeji ambaye pamoja na kutambikia mambo fulani fulani na ni lazima kwa mafanyakazi kufa kila mwaka head office ghafla na kuanza kutokwa na damu every opening of the body alifariki!!!!. Jamani tutumie elimu ya ujasiriamali na bishara zaidi ya mazindiko!!! Huwa hayalipi!! ni madhara kwa familia au wafanyakazi! Imagine kuna a true strory mkinga mmoja last month alimua mtoto wa dada yake wa damu kwa ajili ya zindiko, maiti ilileta kasheshe maana dada mtu alijua fika mtoto kauliwa na kaka yake kwani alijaribu kumuua mtoto mwingine wa huyo dada ikashindikana!! Alipopata mwanya tu huyu wa pili alipoenda kwake akamuua. Ilibidi wazee wa kikinga waombe sana yule dada apokee maiti na kuzika. Baada ya maziko mkinga pesa iliingia na sasa ameshanunua site 3 Kariakoo anajenga ghorofa na duka la ngua ni balaa!!! But yote hayo yana mwisho jamani, kwa nini uwe na fedha za masharti?

Na huko Mbeya nako kuna mganga mmoja ambaye yeye hutumia kuku kula punze za mahindi. Anaahidi kukupatia utajiri ambao ni sawa na idadi za punze za mahindi atakazoweza kudonoa na kumeza kuku wake wa uganga. Ni hivi anamwaga punze nyingi za mahindi chini, anamchukua kuku ili adonoe akidonoa kumi jua kuwa utapata utajiri babukubwa kwa miaka kumi halafu utakufa!!! Kuna jamaa alienda kuku akadonoa punze moja tu na kweli akapata utajiri kwa mwaka 1 na kufariki!!! Sasa yote ya nini kujitoa kafara mwenyewe au ndugu zako. Struggle hard, with determination you will win!!!

Umesomeka vyema mkuu. Hizi ndo zinaitwa dini za jadi za kiafrica na Asia hasa. God forbid.
 
Back
Top Bottom