sata hakwenda Australia

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Rais Sata amesema ni ngumu kusafiri kwenda australia kuhudhuria mkutano wa commonwealth kwa sababu ya kazi nyingi
badala yake amemwomba makamu wa raisi Guy Scoot kwenda badala yake
sasa hapo ina maana Rais wetu hawezi kuwapa wengine nafasi wahudhurie mikutano?
kwani lazima ahudhurie mikutano yote anayo alikwa?kazi zake anamwachia nani?
hana mzigo na taifa?hizo starehe anazofata huko zitamsaidia nini?
kwani ni yeye peke yake mtanzania?
 
Mkweree ameacha kuwa VASCO DAGAMA sasa amegeuka kuwa YOHANA MTEMBEZI!!
 
kwani jk si anasafiri mara nyingi kwa ajili ya kukimbia matatizo ya wananchi wake.
Satta anadili na matatizo ya wananchi wake.
 
Labda yeye sio mcheza kamari, sasa aende kucheza kamari Aussie ili iweje?
 
Si tu amefikiria kuhusu wingi wa kazi, kiuchumi pia. Msafara wa rais unakuwa na kenge, mamba na mijuzi wengi, lakini wa makamu wa rais au waziri mkuu, wanakuwa wachache.

Halafu mikutano kama hiyo haina tija kabisa they are merely talk show.
Kama Common wealth ndiyo haina maana kabisa siku hizi maana UK imeshajifunua wazi kuwa ni Great Ally wa USA tu.
 
Asipoenda nani atabembea? Me hujiuliza kama ni goodtimes anafuata kashindwa nini kuzijenga hapa kwetu? Ufukwe upo, milima ipo, tambarare, mbuga na mengine. Zingejengwa hapa na wageni zingeleta.

Na kama ni picha kafuata hapa si kuna kina Kanumba apige nao?
 
Mwacheni Rais wetu jamani aende akatuombee vyandarua kwa ajili ya kujikinga na malaria
 
na huku bado tuna shule full suit nyasi na ubao kipande cha bati!

ndugu yangu, nimeiona hii jana. nilisikitika sana kwa kweli. inaonesha jinsi "tulivyothubutu, tukaweza na kusonga mbele" kwa dhati katika miaka yetu 50 ya uhuru...
 
......hana kazi nyumbani, afanye nini hapa. Bado anajifunza wajameni...
 
Back
Top Bottom