Sasa wachota kwa Magufuli - Dola yachunguza utata wa bilioni 10/-

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Waandishi Wetu - Raia Mwema


magufuli224.jpg



Waziri wa ujenzi, Dk. John Magufuli


Dola yachunguza utata wa bilioni 10/-
Wizara, TANROADS wakiri 'uchakachuaji'


UTATA umegubika mabilioni ya shilingi za malipo ya wakandarasi wa barabara, yanayodaiwa kuwa ni hewa, na ambayo yanaelezwa kuwahusisha vigogo ndani ya Wizara ya Ujenzi, inayoongozwa na Waziri machachari, Dk. John Magufuli, Raia Mwema limefahamishwa.

Taarifa zinasema Serikali ilikuwa ikidaiwa na wakandarasi mbalimbali jumla ya Sh. bilioni 425.11 hadi mwishoni mwa mwaka jana, deni ambalo Serikali iliamua kulipa nusu yake (Sh bilioni 200) kati ya mwisho wa mwaka jana na mwaka huu, fedha ambazo sehemu zinahofiwa kuingia katika mikono ya kifisadi kwa kuwahusisha watu mbalimbali wakiwamo wanasiasa, watendaji na wafanyabiashara.

Baadhi ya maofisa waandamizi ndani ya Serikali wamehusisha utata huo na wanasiasa ambao wanafanya maandalizi ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015, wakianzia na uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka huu wa 2012.


Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kwamba kuna utata katika takriban Sh. bilioni 10 kati ya malipo ya Sh bilioni 200 zilizotengwa kwa ajili ya malipo ya wakandarasi na wahandisi washauri wa miradi ya barabara nchini zilizotengwa kati ya Oktoba 2011 na Januari 2012.


Habari kutoka ndani ya vyombo vya dola zimeeleza kwamba, makachero wanaofuatilia matumizi ya fedha za Serikali walibaini ongezeko lisilo la kawaida la Shilingi 9, 909,871,333.55 kwenye malipo kwenda kampuni ya CHICO-CRSG JV.


Malipo ya kampuni hiyo ya CHICO-CRSG JV yanahusu ujenzi wa kilometa 154 za barabara ya Kagoma-Lusahunga mkoani Kagera kwa kiwango cha lami.


Kwa mujibu wa taarifa za ndani ambazo kwa sasa zimeshafikishwa katika vyombo vya dola na uongozi wa juu wa nchi, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umekwisha kukiri utata huo kwa maelezo kwamba utawachukulia hatua waliohusika kuzidisha Sh bilioni 10 katika deni halisi lililopaswa kulipwa kampuni ya CHICO-CRSG JV.


Mawasiliano kati ya Wizara ya Ujenzi na TANROADS ya Novemba 2011, yalionyesha kwamba hadi Oktoba 31, 2011 kampuni ya CHICO-CRSG JV ilikuwa ikiidai Serikali shilingi 38, 805,183,868.53 badala ya deni halisi la shilingi 27,224,917,911.10,
kabla ya ziada hiyo kushitukiwa na kuzuiwa kulipwa na Hazina.


Deni halisi kwa mujibu wa nyaraka rasmi ni dola za Marekani 9,800,588.37 ( sawa na Sh. 17,964,478,482.2 kwa thamani ya dola moja Sh. 1,833 Oktoba 27, 2011), na shilingi 9,260, 439,428.89 sawa na jumla ya shilingi 27,224,917,911.10.


Hata hivyo, TANROADS inayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Patrick Mfugale, iliiandikia Serikali Novemba 2011 kwamba deni ni 38,805,183,868.53 ambazo kati ya hizo Sh 37,134,789,244.65 zilikuwa ni za mkandarasi CHICO-CRSG JV, Sh 1,352,662,536.63 za wahandisi washauri na Sh 317,732,088.25 kama fidia ya kuchelewesha malipo, fedha ambazo zilichomekwa Sh bilioni 10 hewa.


Katika maelezo yao TANROADS wamedai kwamba utata huo ulitokana na "uzembe wa mhandisi anayesimamia mradi huu (Kigoma-Lusahunga) ambaye hakuhakiki vizuri deni la mradi wake kama alivyokiri mwenyewe" na kwamba hatua zimechukuliwa.


"Nitahakikisha uzembe wa namna hii hautokei tena na wahandisi waliohusika nimewachukulia hatua zinazowapasa. Ninaendelea kuhakiki usahihi wa madeni yote na nitatoa taarifa mara nitakapomaliza zoezi hili," anaeleza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mfugale katika barua yake ya Desemba Mosi, 2011 yenye kumbukumbu namba TRD/D/GEN/P 99/01/XVIII/A.


Habari zinaeleza kwamba utata huo wa malipo ya Sh bilioni 10 ni tukio moja tu la fedha nyingi zinazohofiwa kupotea serikalini na tayari uchunguzi zaidi unaendelea katika maeneo mengine ndani ya Wizara ya Ujenzi ambako wakala wake mmoja (si TANROADS) nako kuna deni la Sh. milioni 800 ambazo zinaelezwa kwamba deni halisi ni Sh. milioni 60 tu. (Tunahifadhi jina la taasisi husika hadi wakati mwafaka).


Katika kuficha malipo hayo, imeelezwa kwamba wahusika hutumia mbinu nyingi ikiwamo kutaka yalipwe katika akaunti maalumu badala ya utaratibu unaotumika serikalini unaojulikana kama CPO.


Wakati hayo yakiendelea, jana Jumanne wakurugenzi wote wa TANROADS wamekabidhi ofisi zao baada ya kuagizwa na Mtendaji Mkuu kwa waraka wa Januari 24, 2012 wenye kumbukumbu namba TRD/HQ/CE/15.


Hatua hiyo inafuatia mabadiliko yanayolalamikiwa sana ya mameneja wa mikoa, yaliyofanywa na TANROADS, mabadiliko ambayo yanaelezwa kwamba yamegubikwa na utata mkubwa unaohusishwa na mahusiano kati ya wahusika na uongozi wa juu wa wakala na Wizara ya Ujenzi.


TANROADS imekuwa ikizungumzwa sana kabla ya kuondoka kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wake aliyeondolewa Ephraem Mrema, lakini hali ilitulia kidogo alipoingia Mfugale ambaye watendaji serikalini wanaeleza kwamba kuingia kwake nako kuna utata kama ilivyo kwa Wakala wa Umeme (TAMESA).


Tayari Rais Jakaya Kikwete ameombwa kuingilia kati hali ilivyo ndani ya Wizara ya Ujenzi na asasi zake kwa kumuomba kutupia macho wizara hiyo kwa kutumia vyombo vyake badala ya kutegemea wizara ambayo kwa sasa imekuwa ikiendesha mambo kwa kuzingatia maslahi ya wachache.


"Mheshimiwa Rais kama anataka ahadi zake zitekelezeke basi zoezi la uteuzi wa wakurugenzi wa wizara na taasisi zake upitie kwake na si vinginevyo kwa maslahi ya nchi na umma," anaeleza ofisa mmoja ndani ya serikali.


Ofisa huyo ambaye kitaaluma ni mhandisi, ametoa mfano Mtendaji Mkuu aliyetangulia Ephraem Mrema, alikuwa akimsingizia Rais katika kila jambo alilotuhumiwa nalo, mambo ambayo yalibainika yalikua uongo.








 
And I believe nothing will be done about it. Hivi yule boss wa TBS bado anaingia ofisini baada ya kuwadanganya wabunge?
 
Mbona mnamtuhumu mtu ambaye hajawa proven guilt?
Ngojeni mambo yawekewe hadharani tujue nani kakwapua izo ela.
Alafu iyo dola yenyewe ya kuchunguza ilo iko wapi?Naona watakuwa wameamua kuchafuana tuu
 
Mbona mnamtuhumu mtu ambaye hajawa proven guilt?
Ngojeni mambo yawekewe hadharani tujue nani kakwapua izo ela.
Alafu iyo dola yenyewe ya kuchunguza ilo iko wapi?Naona watakuwa wameamua kuchafuana tuu


Haya mambo ya kusubiri watu wawe proven guilty wakati hakuna hatua zinazochukuliwa tumechoka nayo. Kama kungekuwa na chances za wao kuchunguzwa na hatimaye kupelekwa mahakamani atleast tungesubiri. Tatizo huo uwezekano haupo kwa sasa. Ndiyo maana huko mtaani wananchi wakipata mwizi au jambazi wanamalizana nalo bila vyombo vya dola.
 
Mbona mnamtuhumu mtu ambaye hajawa proven guilt?
Ngojeni mambo yawekewe hadharani tujue nani kakwapua izo ela.
Alafu iyo dola yenyewe ya kuchunguza ilo iko wapi?Naona watakuwa wameamua kuchafuana tuu

Umeona Nani kwenye Serikali ya Chama Cha Mapinduzi Mtu yeyote aliyepatwa guilty on anything tangu Nyerere aachie Ngazi?
Mahakama zimelala, Bunge limechoka linataka pesa zaidi, Mawaziri matumbo makubwa, Rais Mtembezi, makamu yeye ni kufunga kila kitu, watumishi ni kuiba chochote kilicho wazi na bure

Kenya wanatushinda na watu kuwa GUILTY hapa bongo kila mtu ni Msafi hadi waliotiana Sumu ni wazuri wanapelekana India wanapokeana wanaambiana kaa nyumbani wizara ni yako haufukuzi na usifanye kazi and it is common USIFE TU
 
Back
Top Bottom