Sasa ni wakati Wamachinga wapewe maeneo rasmi ya kufanyia Biashara

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,450
10,209
Baada ya Mwendazake kuondoka sasa ni wakati wa kuwaondoa wamachinga wote sehemu zisizokuwa rasmi kibiashasha na kuwatafutia sehemu rasmi.

Lazima tuwe na utaratibu sasa, jiji la Dar wamachinga wamekuwa kama uchafu, ukifika Kariakoo barabara Msimbazi, makutano ya Msimbazi Uhuru wamacinga mpaka barabarani, mbaya zaidi wanajenga mabanda mabovu.

images.jpeg
 
Ni kweli serikali yapaswa kulitizama hili jambo kwa umakini wake kwani kadri muda unavyokwenda wanazidi kujaa barabarani, hii itakuja leta changamoto kubwa siku za usoni itafika mahala kuwahamisha hayo maeneo itakuwa ni vita kwa kuwa wataona wana haki kufanya biashara maeneo hayo, kwa hiyo ni vyema kwa sasa serikali ikatengeneza maeneo yao rasmi ya kufanyia biashara halafu wahamishwe kuelekea .maeneo hayo.
 
Waachwe hapohapo nao wapate urahisi wa riziki si kuja kuwaondoa na kuwapeleka maeneo ambsyo ni tabu hadi kufikika. Kama njia yako ya riziki ipo sawa, usitibue za wengine, siku zote wanapopelekwa hata Wateja hakuna
 
Baada ya Mwendazake kuondoka sasa ni wakati wa kuwaondoa wamachinga wote sehemu zisizokuwa rasmi kibiashasha na kuwatafutia sehemu rasmi.

Lazima tuwe na utaratibu sasa, jiji la Dar wamachinga wamekuwa kama uchafu, ukifika Kariakoo barabara Msimbazi, makutano ya Msimbazi Uhuru wamacinga mpaka barabarani, mbaya zaidi wanajenga mabanda mabovu.

Sio kariakoo tu, hata ndani ya bunge wamejaa haohao
 
Machinga ni kundi ambalo ukiliendekeza unapotea na kodi hauwezi kukusanya ipasavo
 
Sio kariakoo tu, hata ndani ya bunge wamejaa haohao
Sasa hilo ni tatizo tukiendelea kuwalea litakuja kuwa Bomu kubwa mbele ya safari watakuja mpka maeneo hatarishi na majumbani kwetu
 
Waachwe hapohapo nao wapate urahisi wa riziki si kuja kuwaondoa na kuwapeleka maeneo ambsyo ni tabu hadi kufikika. Kama njia yako ya riziki ipo sawa, usitibue za wengine, siku zote wanapopelekwa hata Wateja hakuna

Akili ndogo sana. Barabara imejengwa kwaajili ya wamachinga unajua imetumika fedha kiasi gani kuijenga. Riziki zako tafuta lakini sio kwenye eneo la barabara.
 
Maghufuli si aliwanyima vijana ajira, lengo lake wawe wachuuzi kama hvo na mabanda yao mabovu , Ila akawaahdi kuwalinda wafanyie popote ili wasimsumbue, Jamaa alitengeneza tatizo kubwa sana
 
Waachwe hapohapo nao wapate urahisi wa riziki si kuja kuwaondoa na kuwapeleka maeneo ambsyo ni tabu hadi kufikika. Kama njia yako ya riziki ipo sawa, usitibue za wengine, siku zote wanapopelekwa hata Wateja hakuna
Ungekua wewe unafanya biashara ungeelewa ni nini hasa hawa Machinga wanakizuia, Lakini kwa vile hujawai kufanya biashara mahali si ajabu kuwatetea hawa machinga,Mamlaka za miji zitekeleze wajibu wao wa mipango miji , Hakuna mahali pengine duniani kunafanyika hali ya namna hii, Watu wanapanga bidhaa barabarani wengine mpaka kupika chakula wanapika na majiko ya mkaa barabarani? Magufuli alituharibia nchi sana sasa sheria zitumike kuwaondoa sababu wana maeneo yao tengefu pembezoni na miji.
 
Huwezi kuwajengea machinga soko au sehemu ya biashara. Hiyo ipo duniani kote. Sijui wajinga gani walimdanganya JK kujenga machinga complex!! Cha muhimu ni kutowaruhusu au uwaruhusu kufanya biashara. Nyingine ni kuwakataza kuweka kambi rasmi kama meza, vibanda au kupanga biashara chini. Kama kweli ni marching guy basi waishi kulingana na jina lao. Watembeze biashara.
 
Back
Top Bottom