Sasa ni dhahiri, NASA=ODM and not otherwise. Kalonzo Musyoka huenda akaachana na Muungano huo

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
Wadau Amani kwenu.

Nianze kwa kuwatakia wakenya wote maandalizi mazuri ya Uchaguzi hapo October 26.

Sasa ni wazi kabisa kuwa muungano wa NASA umeshasambaratika. Baada ya Raila kukimbia kushiriki Uchaguzi sioni tena zile press conference za pamoja alizokuwa akifanya huku Kalonzo MUsyoka na Musalia Mudavadi wakiwepo. Sahivi press zote za hiyo inayoitwa NASA zinafanywa na Orengo na Moses Wetangula. Sijui nini kimewakuta Mudavadi na Musyoka. Lakini kilichopo ni dhahiri; hawafurahishwi na mwenendo wa NASA kwa sasa kwa kuwa inaonekana kuwa wanaburuzwa.

Hata kitendo cha Raila cha kujitoa kugombea urais huenda yalikuwa ni maamuzi yake yeye Raila na ODM yake na wala vigogo wengine wa NASA ambao ni Mudavadi na Musyoka waliafiki kwa shingo upande.

Na hata maandamano yanayodaiwa ya kuipibga IEBC yanafanyika Kisumu, Homabay, Siaya, Migori na baadhi ya sehemu za Nairobi na hasa Kibera. Hatujadikia maandamano ya aina hiyo yakifanyaka Eastern ambalo ni ngome ya Musyoka na chama chake cha WIPER.

Kutokana na hali hiyo, Majaliwa na Musyoka na Mudavadi ndani ya NASA ni ya mashaka. Sitashangaa kusikia kuwa Musyoka amejiondoa kwenye Muungano huo na kujiunga na Jubilee either kabla ya Uchaguzi wa October 26 au mara baada ya Matokeo ya Uchaguzi huo kutangazwa.

Ni mtazamo wangu but mark my words that Steven Kalonzo Musyoka will defect to Jubilee soon.
 
Back
Top Bottom