Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba, mwanamke ambaye anavaa kwa njia yenye kuchokoza hisia, hawezi kutazamwa kama aliye na uwezo sawa na wengine mahali. Hii iko duniani kote, bila kujali kama ina ukweli au haina.
Njia rahisi kwa wanawake wasiopenda kuwajibika kwa maisha yao ni kuwalaumu wanaume, na ndio maana mie hata sishangai ninaposhambuliwa pale ninapoweka mada kuwakosoa wanawake. Mtu anazungumzia kuhusu kuvaa vibaya kwa wanawake kwamba, kunachangia kuwafanya waonekane ni bidhaa, wanawake wengine wanabisha. Kubisha huku ni kukataa kuwajibika. Lakini hata wakibisha, bado jamii zote zinaushikilia huo wanaoukataa kuwa ndiyo ukweli.
Mtu akijichukulia kwa udhati fulani, wengine nao watamchukulia kwa udhati huo. Akishindwa, wengine nao watashindwa kumchukulia kwa udhati unaostahili. Kama unataka kubishana na hao wengine, ni suala la kujaribu kuipinga hali halisi na kupinga kuwajibika kwa maisha yake. Hebu fikiria, hata kama ni mwanaume. Leo hii mwanasheria wa kiume amevaa 'pensi' huku akiwa ameteremsha mlegezo mpaka makalio yanaonekana na shati la 'ki-modo' na makobazi, unadhani ni nani atamkabidhi kesi yake. Hata kama ni mwanasheria mzuri vipi, labda tu kama mtu anamjua vizuri sana tangu hapo kabla.
Mwanamke ambaye ni afisa mahali kama Mamndenyi, akienda ofisini na kimini na kitopu chenye kuonesha kitovu, hakuna atakayetilia maanani maneno yake. Mhuni hatiliwi maanani. Kwa jamii, hizo ni nguo za kihuni, iwe ni kweli au sio kweli, ndiyo tafsiri yake. Mwanamke anapovaa kama kifaa, wanaume wanapomzonga au kumchukulia kama kifaa, hilo sio suala la unyanyasaji kijinsia, bali ndiyo hali halisi. Mtu wa zima-moto tunamjua kwa mavazi, mcheza mpira tunamtambua kwa mavazi, mwanafunzi hivyohivyo. Ndiyo maana kuna wakati makahaba wa jijini Dar walikuwa wanavaa kama wanafunzi na mashugadadi wakawa wanawachangamkia sana. Mavazi husema sisi ni nani na ni jamii imepanga siyo wanaume.
Huwa tunawaambia wengine sisi ni akina nani kwa lugha za ishara za aina mbalimbali, na ndio maana wengi hawashangazwi na majibu ya baadhi ya wana JF wanapojibu hoja humu jamvini, mfano mzuri kama, mzee mwenzangu Rejao, rafiki yangu Bujubuji, Ndyoko, au Washawasha. Hawa wamejijengea sifa moja kubwa humu jamvini, huwa hawamung'unyi maneno. Inawezekana wasichana wengi siku hizi hawajui kwamba huwa wanasema wao ni nani kupitia mavazi. Wanachojua wao ni fasheni ambayo wameiyona kwa wanawake fulani maarufu hususan wa nchi za Magharibi, lakini hawajui jamii inapokea ujumbe gani kwa mavazi yao.