Pigo la pili kwa mwakyembe alitegemea albaki hapa kwa Kipande kutokana na kumlinda muda wote huu aliokuwa akifanya udhalimu. sauti ya wengi ni sauti ya mungu. Umejidhalilisha sana mkuu na hakika mtalipa kwa uonevu wote mliofanyaNdiyo ukweli halisi mwakyembe aliteleza kabisa.
kilichobaki sasa wataanza kurogana wenyewe kwa wenyewe... kazi kweli kweliWadau salama....
Katika kile kinachoonekana mbio za urais kushika moto, Leo waziri wa uchukuzi Samwel Sitta bila kupepesa macho wala kutikisa masikio amemshughulikia aliyekuwa mshirika wake wa muda mrefu. Akiwa anaongea kwa ujasiri na kwa dharau Sitta amewasimamisha kazi mara moja aliyekuwa mpambe mkubwa wa Mwakyembe Bwana Madeni Kipande (kaimu DG wa Bandari). katika hatua nyingine Sitta amemsimamisha kazi pia ndugu yake Mwakyembe ambaye ni kaimu mkurugenzi wa ATC Bwana Kapten Lazaro.
Ni jambo la wazi Mwakyembe alitumia gharama kubwa sana kulinda uozo uliokuwa unafanya na Kipande pamoja na huyo ndugu yake wa ATC. kwa haraka haraka tafsiri ya hili jambo ni kwamba Sitta na Mwakyembe wamefungua ukurasa mpya wa kushughulikiana. Muda sii mrefu tutasikia pia Mwakyembe kuwafukuza kazi watu wa Sitta katika wizara ya Africa Mashariki.
Hotuba ya Nyerere
kwa haya yanaoendelea kati ya Sitta na Mwakyembe nakifananisha na maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, pale aliposema kwamba dhambi ya usaliti ni sawasawa na kula nyama ya mtu.... ukishakula nyama ya mtu huwezi kuacha, ina maana kwamba ukiwa na damu ya usaliti utazidi kuwa msaliti daima. Leo hii Sitta na MWAKYEMBE wameanza kusalitiana na kurogana wenyewe baada ya kumaliza wote. Sitta na Mwakyembe wa 2008 siyo wa leo, Sitta na Mwakyembe waliopika majungu na fitina dhidi ya kampuni ya Richmond leo hii hawako wamoja tena, ni wazi Mungu ni mkubwa..... wananchi tupo mkao wa kusikia yatakayojiri
Mytake: Ukiwa msaliti utazidi kuwa msaliti daima, ukiwa mnafiki utazidi kuwa mnafiki daima, ukiwa mtu wa majungu utazidi kuwa mtu wa majungu daima na ukiwa mzandiki utazidi kuwa mzandiki daima...
Asanteni
Agwambo
Sita na Mwakyembe ni wanafiki wakubwa sana....... Dhambi ya usaliti inawasuta
Malalamiko kwa Mhandisi Kipande yalianza siku nyingi ila wakubwa waliamua kuweka pamba masikioni mwao.
Bila shaka watakuwa wanashangilia kurudishwa tena kwa mabonanza pale harbours club .Ni kweli Mkuu. Sitta amemsimamisha kazi Madeni Kipande na nafasi yake imechukuliwa na Awadhi Massawe. Huko Bandari ni chereko, vifijo na nderemo.
Bila shaka watakuwa wanashangilia kurudishwa tena kwa mabonanza pale harbours club .
Mbona Sitta watamtambua tu, na bado.
Ndio huyu Kipande aliwekwa na KASSIM MTAWA?
Japo hili la Kipande mlipongeze Gazeti la Jamhuri jamani!!
Alisema ni gazeti la kufungia vitumbua!!! Da, huyu binadamu jeuri sana.Hili jambo najua limekufuraisha sana mkuu.... Kwa kweli Jamhuri lilipigana sana sana....