Samia wa Suluhu ni suluhu kweli kweli

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
Anaandika Mo Mlimwengu

Paukwa!
Paukw !

Watoto wangu eeh eeh,
Mimi mama yenu eeh
Fujo siyo nzuri eeh,
Ilimuua babu eeh
Na ikamuua bibi eeh
Sasa wote njooni kwangu.

Ile ndoto aliyokuwa nayo Martine Luther King alifariki kabla hajaiona kwa macho yako. Leo hii naiona ndoto ambayo niliiota kwamba Tanzania tunarudi kuwa wamoja.

Hii ndoto inatimizwa na mwanamke shupavu, jabali wa siasa na mwanadiplomasia aliyepikwa akapikika. Leo hii tunaona Rais anatembelea nyayo za Mahatma Ghandhi aliyesema In a gentle way you can shake the world.

Naiona ndoto ambayo ulimwengu wote unachukua darasa kwa Dr. Samia maana ya maridhiano, leo hii anatoa darasa kwa mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea nini maana ya utaifa.

Ni nani aliamini kwamba leo Rais wa nchi anahutubia chama cha upinzani na tunaona kila mpinzani ana furaha hadi jino la 32 linaonekana pasipo kuonyesha chuki. Tunaiona maana halisi ya No Hate no Fear.

Leo hii Rais anatufundisha uongozi ni kuvumilia na kusikia yale ambayo hata hayakufurahishi. Ni nadra sana kwa nchi zinazoendelea kumpata Rais kariba ya Samia ambaye anaonyesha maana halisi ya demokrasia na muumini wa haki wa kweli. What a president?

Mlimwengu naomba niache hii simulizi tamu ambayo haichoshi kuisikiliza kuhusu Rais wangu Samia ambaye baba yake amekuwa Suluhu wa taifa letu.

Historia inaendelea kuwekwa awamu ya sita na huku sisi wengine kazi yetu ni kuweka kwenye kumbukumbu kwa ajili ya kizazi na kizazi kwamba alikuwepo mmahiri wa siasa na aliweza kuvunja mfupa ambao uliwashinda wengi.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Rais Samia.
 
Hii ndyo siasa safi," practicing Levelling ", ukiwa Rais kila kitu ni chako " comforting the marginalised ni Role ya kiongozi yeyote anayejitambua. NCHI ILIPATA WRONG LEADER aliekuwa anajua akila mahindi barabarani basi amemaliza kazi. Mi nampa hongera Mwanamke huyu " huyu hata mkimwita Iron lady mtakua mumemtendea haki sana". Hongera Rais!!
 
Back
Top Bottom