Samaki waelea ufukweni Dar. Serikali yachunguza chanzo…

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,583
6,633
Samaki kibao wanaelea katika bahari ya hindi eneo la Aga Khan jijini Dar. Wananchi wanafanya kuokota tu.

Haijulikani chanzo cha samaki hao kuelea.

Hofu ni juu ya madhara yatakayotokana na samaki hawa. Ni sumu gani imewaua samaki hawa?

IMG_4189.jpg

IMG_4188.jpg

IMG_4187.jpg

IMG_4186.jpg

IMG_4185.jpg

IMG_4184.jpg


UPDATE:
Serikali yatoa kauli

9AD91651-77C6-44AD-8C9D-E124B2220CDC.jpeg

934FE08F-2918-4B1E-B5A4-F9E0D4442AFC.jpeg
 
Meli kubwa ya uvuvi imewamwaga samaki wasio na thamani au ni ukosefu wa hewa au ni sumu itokanayo uchafuzi wa mazingira na madawa ya ujenzi wa miradi ya mwendazake baharini n.k

Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira https://www.nemc.or.tz/pages/mission-and-vision NEMC wafanye ziara eneo hilo na kutoa ripoti bila kupepesa macho chanzo cha kupelekea viumbe wa baharini kuonekana wafu ktk eneo hili la jiji la Dar es Salaam
 
Naamini katika mazingira hao ni kwamba wamekufa,

Hivi kweli mtu unakuta samaki kafa mwenyewe unabeba ukalee???
Huku ni kuendekeza njaa kulikopitiliza,

unafika nyumbani na lijibesi lako unajifanya umetoka kununua samaki kumbe umeokotaaa, ukiua familia???
Eti familia imelazwa au imekufa(yote hatuombei yatokee) kisa pelege????
 
Naamini katika mazingira hao ni kwamba wamekufa,

Hivi kweli mtu unakuta samaki kafa unabeba ukalee???
Huku ni kuendekeza njaa kulikopitiliza, unafika nyumbani na lijibesi lako unajifanya umetoka kununua samaki kumbe umeokotaaa... Daaah
Ukiwa mtu mwenye kipato, unaeweza kumudu chakula bila wasiwasi, ni rahisi sana kutoa kauli ya namna hiyo.

You sound like a highly privileged black kid!
 
Serikal iko kmya subl madhara yajitokeze hapo ndy waanze kutaftana na kuanza kuleta siasa zao ktk maisha ya watu...hii nchi hovyo sana, hapo ilitakiwa pafanyiwe uchunguz wa kina, maana hiyo inaweza kuwa dalili mbaya kwa viumbe wa majini, mybe kuna mapandikiz ya sumu yalitegwa ktk maji na kuperekea maafa ya viumbe hao na pia inawezekana viumbe hao(samaki) wakawa bado na chembechembe za sumu ambazo znaweza kuwadhuru watumiaji,

Tunatakiwa kuwa waangalifu, ulafi utakuja kuwatokea puani....wakumbuke na lile la morogoro, watu walimiminika kuchota wese kumbe kuna balaa likawakuta, na baadae gumzo likazuka kuwa kuna uzembe wa askar kutojitokeza mapema kuzuia labda maisha yasingepotea kias kile.....watz tuache ulaf
 
Hali Tete Sana Mpaka Sasa Hivi Haiwezekani Samaki Kufa
Siyo Kwa Idadi Hiyo Mara Moja. Hatari Na Nusu
Hao Wanaozoa Wasile
 
Ukiwa mtu mwenye kipato, unaeweza kumudu chakula bila wasiwasi, ni rahisi sana kutoa kauli ya namna hiyo.

You sound like a highly privileged black kid!
Khaaaa, hili nalo linahitaji mjadala wa kiuchumi?

Yaani unataka uhalalishe Matatizo ya kiafya au hata umauti kwa kigezo cha umaskini?
Hivi kama samaki hao wamekufa kwa sumu ambayo ina uwezo wa kuathiri mpaka binadamu?

Mwaka 2019 kule Micheweni Pemba, Familia moja ya watu 7 walikula samaki waliokutwa wakielea kumbe walikufa kwa sumu, kati yao 5 walikata moto punde tuu baada ya kula, 2 walilazwa hali zao zikiwa mbaya(sijui kilichoendelea).

Kwahio Hili ni suala la afya yako ndugu, ukapata matatizo au ukafa kifo cha kujitakia hivyo hata kwa muumba wako ni kosa....

Acha kutafuta huruma ya umaskini ndugu.
Umaskini hauondolewe kwa kua mnyonge mwenye kauli za kutafuta huruma...

Omba Mungu, Pambana, Subiri matokeo, Ukipata Sawa, ukikosa vuta subira usikate tamaa Pengine mda wako bado.
 
Naamini katika mazingira hao ni kwamba wamekufa,

Hivi kweli mtu unakuta samaki kafa mwenyewe unabeba ukalee???
Huku ni kuendekeza njaa kulikopitiliza,

unafika nyumbani na lijibesi lako unajifanya umetoka kununua samaki kumbe umeokotaaa ukiua familia???
Kule FERI, KUNDUCHI, nk, kesho watu watauziwa bila kujua kinachojiri
 
Back
Top Bottom