Sala zenu zinahitajika (Somalia's famine crisis)

Namshukuru Mungu kwa chakula ninachokipata, kama kuna dhambi zozote eheee Mungu naomba uwasamehe. Kwa kweli inasikitisha sana

Mkuu hili ni janga na kimataifa na tuwaombee wenzetu na tumshukuru Mungu hata kwa kile tunachopata ni kweli hali ni mbaya
 
itakuwa bora sana kama tukailinda shibe yetu na amani tuliyonayo ingawa tunaonewa.
 
Mshukuru Mungu kwa kila jambo, wengine wanadai hawawezi kula chakula kilicholala (kiporo) wengine wanakufa kwa njaa wakitamani kula hata huo uporo unaoukataa. Mungu tunusuru na uwalinde hawa binadamu wenzetu kwani sio kama sisi ni wema kuliko wao.
 
Sala tu hazitoshi mdau, hivi wewe ukisikia njaa huwa unaenda kusali au unaenda kutafuta msosi???? Kama kweli inakuuma jipigepige mfukoni uwatumie angalau chochote, kuna mashirika kama red cross/crescent wanakusanya michango.
 
Kusema nivyepesi, lakini kutenda ni vigumu, na kila mtu anahukumiwa kutokana na vitendo vyake sio maneno ya kutoka kinywani mwake! eeh Mola wasaidie ndugu zetu hao :)
 
Hapa NATO wako waq? Au hapa hakuna maslah. Ingekuwa Libya wangetoa misaada. Mungu wasaaidie hawa viumbe wako.
 
Yaani hawa jamaa wa kimataifa bana wanakaa vikao kuulizana kama pembe ya africa kuna njaa wakati kila siku wanaona taarifa kwenye vyombo vya habari
hii ni sawa na wakati ule wa rwanda watu wanaua wao wamekaa wanaulizana ile ni genocide au ni masacre yaani hawana maana kabisa
 
Hivi kwanini tusiiteke Somalia na kuikalia kimabavu kama wanavyofanya wamarekani ktk nchi za kiarabu? mie naona hili tatizo lao la njaa tungelimaliza
 
Back
Top Bottom