Sakata la Morrison Kinachoendelea

Ni sheria gani hiyo inayomnyima haki mtu asiye na fedha na kumpa haki aliyenazo?
Ni hivi ndugu

Hata mahakama za kawaida (isipokuwa mahakama ya kazi kwa sasa hapa TZ) huwa tunalipia unafungua kesi na unapopeleka utetezi.

Kwa kawaida mdaiwa asipopeleka utetezi wake na kulipia, kesi inasikilizwa upande mmoja kwa kumsikiliza yule aliyeleta kesi, mwishowe hukumu hutolewa. Hiyo hukumu inawabana/ wahusu pande zote mbili.

Hiyo ni kwa utaratibu wa mahakama zinazomilikiwa na serikali.

Sasa kuna mahakama ambazo haziundwi na serikali, hizo gharama za malipo huwa kubwa zaidi. Mfano ni kama hizo mahakama za usuluhishi-Arbitration, na zile zilizopo chini ya Umoja wa Mataifa au jumuiya za kikanda kama EAC COURT
 
yangu macho!! yanga hili shauri hamshindi na hamtashinda! viongozi wenu walipeleka hili shauri huko CAS kama kuwaridhisha mashabiki lakini imekuwa kama zali tu CAS wamewaita kulisikiliza. ngoja tusubiri mtanambia.
Mkuu huwa hakuna zali kwenye maswala ya kisheria,labda kama ni Tff na bodi zake ndo kuna zali na wala Yanga haifanyi kitu kwa kuwaridhisha mashabiki,naomba nkuulize jamba- hivi Simba walivyoomba maelezo ya faini waliyopigwa na FIFA juu ya Kichuya kwa ni kuwaridhisha mashabiki au ni kufuata taratibu za kiofisi au sheria?

Ushabiki wa mpira hauwez kutawala my brain.
 
Mwakalebela amelikomalia sana hili swala,na watu wanamchukulia poa na kumkebehi kwa umbo la mwili wake ,labda atapata majibu sahihi ya kile anachokiamini soon,pamoja na hayo Simba nao walijichanganya kwa huyu mchezaji ata mienendo yako si mizuri.
Watu wanamchukulia poa lakin soon wataona matokeo yake
 
Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa taarifa kuhusu maendeleo ya kesi waliyofungua dhidi ya winga wao wa zamani Bernard Morrison.

Akizungumza mapema leo kutoka jijini Mbeya, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kesi hiyo itasikilizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) na tayari imepangiwa Jaji

Mwakalebela amesema baada ya Yanga kuwasilisha malalamiko yao CAS, Morrison alitakiwa kujibu malalamiko hayo na juzi Yanga imepokea barua kutoka CAS ikiwataarifu kuwa majibu aliyotoa Morrison hayana mashiko na hivyo wanapaswa kulipia pesa za Kifaransa franc 12,000 ili kesi hiyo inze kusikilizwa

Malipo hayo yanapaswa kufanyika kabla ya Januari 12 2021 ambapo pande zote zimetakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha

"Yanga tulipeleka malalamiko Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) kupinga maamuzi ya kubatilisha mkataba wa Bernard Morisson na Yanga yaliyotolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF"

"Morrison alitakiwa kujibu malalamiko yetu na juzi tumepokea barua kutoka CAS iliyotutaarifu kuwa majibu yaliyotolewa na Morrison hayana mashiko na kwamba shauri letu litapangiwa Jaji wa kuendelea kulisikiliza"

"Hadi kufikia Leo hii, Jaji ameshapatikana, Morrison na Yanga sote kila mmoja tunapaswa kulipa Franc 12,000 tayari shauri hilo kuanza kusikilizwa"

"Tarehe ya mwisho ya fedha hizo kulipwa ni Januari 12 2021, sisi kama walalamikaji tutalipa fedha hizo ili shauri lisikilizwe", alisema Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga.
Is it worth it?
 
Wanaosema utetezi hauna mashiko ni kina Nani? Kwa hiyo ungekua na mashiko asingetafutwa Jaji? Kwanin wasifanye uamuzi Kama utetezi hauna mashiko?
Mpaka kasimamishwa yule Morrison kucheza na kuambiwa utetezi wake hauna mashiko anakesi ya kujibu,unadhani anaenda kwenye kamati ya msomali?
 
Mwakalebela amelikomalia sana hili swala,na watu wanamchukulia poa na kumkebehi kwa umbo la mwili wake ,labda atapata majibu sahihi ya kile anachokiamini soon,pamoja na hayo Simba nao walijichanganya kwa huyu mchezaji ata mienendo yako si mizuri.
Kwenye masuala ya kipumbavu ,ya kushindwa na ya kuonesha mashabiki wa Yanga hatuna akili huwa anatumika kubwa jinga Mwakalebela. Hata Msolla huwa hataki ku deal nayo. Anaangalia hili jamaa bozo ndo likaongelee. Hamna kitu kwa suala la Morrison. Ndo imeshatoka hiyo. Ni kukumbushana machungu tu
 
Kwenye masuala ya kipumbavu ,ya kushindwa na ya kuonesha mashabiki wa Yanga hatuna akili huwa anatumika kubwa jinga Mwakalebela. Hata Msolla huwa hataki ku deal nayo. Anaangalia hili jamaa bozo ndo likaongelee. Hamna kitu kwa suala la Morrison. Ndo imeshatoka hiyo. Ni kukumbushana machungu tu
Ok.
 
Rudisheni hilo kima kwao,mpira gani anaocheza juzi tu kawatia kidole maana mnahangaika sana
 
Back
Top Bottom