Sakata la Kupotea Rajab Omari Mtana na Hukumu ya Kunyongwa kwa Masheikh 10 Tanga

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
SAKATA LA KUPOTEA RAJAB OMARI MTANA KIJIJI CHA LULAGO HANDENI 2013

Waislam 10 wamehukumiwa kunyongwa kwa tuhuma za kuua mlinzi mmoja.

Kufikia hukumu hii kuna mengi na chanzo chake kilianzia katika biashara ya hiliki na malipo ya ushuru kijijini Lulago.

Ninaanza leo kueleza kisa hiki kama nilivyotafiti na kuweka kumbukumbu miaka 10 iliyopita.

Rajab Omar Mtana alikuwa mwanakijiji wa kawaida tu akiishi kijijini Lulago, Handeni kama wanavijiji wengine wanavyoishi na alikuwa na biashara yake ya kuuza hiliki kama mkulima wa zao hilo.

Siku moja akaja mnunuzi mfanyabiashara wa hiliki nyumbani kwake kununua hiliki na akamuuzia.

Yule mfanyabiashara alipokuwa anatoka na gari yake akasimama kwenye kizuizi cha kulipia ushuru.

Alipotakiwa kulipa ushuru akasema kuwa si hiliki yote amenunua katika kijiji hicho kwa hiyo hawezi kulipa ushuru wa hiliki yote.

Hapo palitokea ubishi na mfanyabiashara yule akagonga lile geti na akaondoka.

Hii ikapelekea kwa wakusanya ushuru wa hapo kijijini kwenda nyumbani kwa Rajab Omar Mtana kumkamata na kumweka chini ya ulinzi katika ofisi ya serikali ya kijiji hadi hapo atakapolipa ushuru ambao yule mfanyabiashara alitakiwa alipe.

Ndugu zake Rajab Omar Mtana wakaenda pale ofisini kwa nia ya kumtoa ndugu yao na hapo pakatokea vurugu na mapigano.

Katika mapigano hayo, mgambo ambae ndiye aliyekuwa akishughulika na kudai ushuru akauawa.

Kisa hiki cha ushuru wa hiliki ndicho kilichozua balaa kubwa la mauaji na uchomwaji moto nyumba za Waislam wa kijiji cha jirani cha Madina na kuvunjwa kwa misikiti katika vijiji ambavyo vilikuwa na idadi kubwa ya wakazi wake Waislam.

Baada ya haya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akatoa amri kuwa hapana ruhusa tena ya sehemu hizo kuwa makazi kwa kuwa hizo ni kambi za ugaidi.

Mkuu wa Mkoa alisema mengi ambayo takriban yote yamedhihirika baadae kuwa hayakuwa na ukweli.

Mkuu wa Mkoa alisema kuwa wapo Al Shabab vijijini, kumechimbwa mahandaki ya vita katika vijiji na kuna silaha za kutungulia ndege nk. nk.

Mkuu wa Mkoa alizungumza na Radio Nuur, Tanga inayomilokiwa na Msikiti wa Ibadh.
Nilifunga safari hadi Radio Nuur Tanga kwa nia ya kupata taarifa kamili yalivyorushwa.

Radio Nuur waliogopa kunipa juu wala kuniruhusu kusikiliza kipindi hicho cha Mkuu wa Mkoa ingawa kabla sijahama Tanga nilikuwa mmoja wa Wakurugenzu wa radio hiyo.

Lakini niliwahoji watu waliosikia kipindi hicho.

Katika Waislam waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani Handeni ni huyu kijana Rajab Omari Mtana.

Baada ya kukaa rumande alipata dhamana yeye pamoja na wenzake na akawa nje.
Rajab Omar Mtana alirejea kijijini kwake.

Wakati anakaribia kuingia kijijini alisimamishwa na askari wa kijiji akapekuliwa na akanyang'anywa simu yake na fedha taslimu.

Baada ya mkasa huu walimwachia na yeye akaendelea na safari yake.

Lakini wakati akiwa rumande nyumba yake ilikuwa imevurugwa haifai kuishi mtu kwa hiyo alifikia kwa dada yake.

Akiwa nyumbani kwa dada yake alifatwa na watu wa serikali ya kijiji usiku akatolewa ndani na kuanza kupigwa kwa bakora na kisha kwa mapanga.

Kujitetea kijana huyu alikimbia huku akikimbizwa.
Asubuhi kulipokucha palionekana damu nyingi sana.

Taarifa ilitolewa polisi lakini hakuna kilichofanyika.
Polisi walitoa taarifa (SON/RB346/2014).

Dada yake na mumewe walikamatwa na kushitakiwa katika mahakama ya hapo kijijini na wakapigwa faini ya kila mtu shs. 20.000.

Kosa lao ni kumleta kijiji Rajab Omari Mtana mtu asiyetakiwa.

Miaka 10 imetimia Rajab Omar Mtana hajulikani alipo na inasadikiwa ameuawa na wale waliokuja kumtoa nyumbani kwa dada yake.

Rajab Omar Mtana ametafutwa kote hajapatikana na waliompiga na kumjeruhi wako huru nje hawajaguswa wala kuhojiwa na polisi.

Lakini wale waliotumiwa kwa mauaji ya mlinzi wa kijiji wamehukumiwa kifo.

Hapa kuna mengi sana ya kufikirisha mbali ya yale kuwa kulikuwapo na silaha za kutungua ndege katika vijiji hivi vya Waislam wa Handeni vilivyokuwa na nyumba za nyasi na udongo.

1687702858046.png

Duuuh inafikirisha hii..

naamini si haki kudhulumu haki ya mtu yeyote awe islam au budha..

kula penye neno muislamu hapo nadhani ungefaa kuweka mtanzania..
katika hukumu hiyo ..
Kawele,
Katika kila msikiti lazima utakuta barza ya kahawa.
Baada ya sala watu hukaa khasa Maghrib wakisubiri sala ya Isha.

Katika barza hizi ndipo ziliposikika habari kuwa Handeni kuna operesheni Waislam wanakamatwa katika vizuizi na kushushwa kwenye mabasi.

Yakasikika maneno mengi na siku moja nikajiwa na kijana mmoja nyumbani kwangu simjui wala sijapata kumuona maishani kwangu.

Akaniambia kuwa katumwa na Waislam aje kwangu anieleze yanayotokea Handeni na mimi niandike makala dunia ifahamu.

Niliyosikia sikuwezi kuamini kama kweli ni kweli kama nilivyoelzwa.

Huyu kijana alikataa kunipa jina lake na alikataa kupigwa picha.
Mimi nikampa jina la kupanga, ''Deep Throat.''

Ingia Google mtafute Deep Throat.

NIkamfahamisha kuwa nimekusudia kwenda Handeni nikashuhudie mwenyewe.
Akanionya akasema nithithubutu kwani nitakamatwa.

Picha niliyojenga kutoka kwa Deep Throat ni kuwa Waislam wa Handeni wapo katika dhiki na madhila makubwa.

Hakika hawa ni Watanzania kama ulivyosema lakini haya yaliwatokea Waislam peke yao.
 
Yule mfanyabiashara alipokuwa anatoka na gari yake akasimama kwenye kizuizi cha kulipia ushuru.

Alipotakiwa kulipa ushuru akasema kuwa si hiliki yote amenunua katika kijiji hicho kwa hiyo hawezi kulipa ushuru wa hiliki yote.

Hapo palitokea ubishi na mfanyabiashara yule akagonga lile geti na akaondoka.
Watu wenye mamlaka Tanzania akili zao sijui zikoje yaani mfanyabiashara(mnunuzi) ndie mkosa. Wao wame kwenda kumkamata muuzaji wa hiliki, hivi hio gari haikuwa na namba na kuwa pelekea polisi na kuikamata.
 
Walishikwa ugaidi mwaka 2013 raisi alikuwa Kikwete - Muislamu, wamehukumiwa kunyongwa mwaka 2023 raisi wa sasa ni Samia- Muislamu, hivyo ni Waislamu wamehukumiwa kipindi cha Maraisi Waislamu pia.

Anayebomb kubomoa na kutesa Waislamu na nchi Kiislamu Yemeni ni Saudi Arabia, anaye fund Al Shabaab Somalia na kuharibu na kutesa Waislamu Somalia ni Saudi Arabi pia, anzieni hapo kwanza, …
 
Kawele,
Katika kila msikiti lazima utakuta barza ya kahawa.
Baada ya sala watu hukaa khasa Maghrib wakisubiri sala ya Isha.

Katika barza hizi ndipo ziliposikika habari kuwa Handeni kuna operesheni Waislam wanakamatwa katika vizuizi na kushushwa kwenye mabasi.

Yakasikika maneno mengi na siku moja nikajiwa na kijana mmoja nyumbani kwangu simjui wala sijapata kumuona maishani kwangu.

Akaniambia kuwa katumwa na Waislam aje kwangu anieleze yanayotokea Handeni na mimi niandike makala dunia ifahamu.

Niliyosikia sikuwezi kuamini kama kweli ni kweli kama nilivyoelzwa.

Huyu kijana alikataa kunipa jina lake na alikataa kupigwa picha.
Mimi nikampa jina la kupanga, ''Deep Throat.''

Ingia Google mtafute Deep Throat.

NIkamfahamisha kuwa nimekusudia kwenda Handeni nikashuhudie mwenyewe.
Akanionya akasema nithithubutu kwani nitakamatwa.

Picha niliyojenga kutoka kwa Deep Throat ni kuwa Waislam wa Handeni wapo katika dhiki na madhila makubwa.

Hakika hawa ni Watanzania kama ulivyosema lakini haya yaliwatokea Waislam peke yao.
Umeingiza udini mahali ambapo hapastahili. Kutokana na maelezo yako mwenyewe Rajab alikamatwa kwa mara ya kwanza kwa sababu mtu aliyemuuzia hiliki alikataa kuzilipia ushuru. Ingawa ulikuwa ni uonezi mkubwa hakukamatwa kwa sababu ni muislamu. Umetuambia kuwa ndugu zake walienda kujaribu kumtoa ndio vurugu zikatokea ambapo mtu mmoja aliuawa. Ingawa bila shaka ndugu zake wengi kama sio wote walikuwa waislamu lakini hawakwenda kituoni kumtoa Rajab kwa sababu ni muislamu bali kwa sababu ni ndugu yao. Mkuu wa Mkoa unayemtaja Chiku alikuwa muislamu na sidhani kama alifanya unayomshutumu kwa sababu ya chuki dhidi ya waislamu.

Kugeuziwa kibao na kesi kugeuzwa kuwa ya ugaidi si kwa sababu ya chuki dhidi ya waislamu bali ilikuwa njia ya kuhakikisha kuwa hawachomoki kirahisi. Hata Freeman Mbowe alifunguliwa kesi ya ugaidi na hamna hata mmoja aliwahi kusema kuwa ilikuwa kwa sababu yeye ni mkristu na Rais muislamu.

Kama unayosimulia yana ukweli wowote ni dhahiri kuwa uonevu mkubwa umefanyika dhidi ya Rajab na ndugu zake. Kuingiza udini hakuwatendei haki maana unageuza suala lao kuwa la maonevu dhidi ya waislamu ( yanayofanywa na wakristu na vibaraka wao) wakati ni mfano mwingine wa watu kutumia nafasi zao kuwaonea na kuwafanyia ukatili binadamu wenzao. Badala ya hili suala kuwa letu wote maana watu wa imani zote wamewahi kufanyiwa ukatili (mfano Mdude Nyangali) nyie mnaligeuza kuni ya kuchochea chuki kati ya waislamu na wakristu. Sio vizuri mnavyofanya.

Amandla....
 
Walishikwa ugaidi mwaka 2013 raisi alikuwa Kikwete - Muislamu, wamehukumiwa kunyongwa mwaka 2023 raisi wa sasa ni Samia- Muislamu, hivyo ni Waislamu wamehukumiwa kipindi cha Maraisi Waislamu pia.

Anayebomb kubomoa na kutesa Waislamu na nchi Kiislamu Yemeni ni Saudi Arabia, anaye fund Al Shabaab Somalia na kuharibu na kutesa Waislamu Somalia ni Saudi Arabi pia, anzieni hapo kwanza, …
R.C Chiku Galawa nae alikuwa ni Muislamu. Mohammed hana nia njema.

Amandla...
 
Umeingiza udini mahali ambapo hapastahili. Kutokana na maelezo yako mwenyewe Rajab alikamatwa kwa mara ya kwanza kwa sababu mtu aliyemuuzia hiliki alikataa kuzilipia ushuru. Ingawa ulikuwa ni uonezi mkubwa hakukamatwa kwa sababu ni muislamu. Umetuambia kuwa ndugu zake walienda kujaribu kumtoa ndio vurugu zikatokea ambapo mtu mmoja aliuawa. Ingawa bila shaka ndugu zake wengi kama sio wote walikuwa waislamu lakini hawakwenda kituoni kumtoa Rajab kwa sababu ni muislamu bali kwa sababu ni ndugu yao. Mkuu wa Mkoa unayemtaja Chiku alikuwa muislamu na sidhani kama alifanya unayomshutumu kwa sababu ya chuki dhidi ya waislamu.

Kugeuziwa kibao na kuwa ya ugaidi si kwa sababu ya chuki dhidi ya waislamu bali ilikuwa njia ya kuhakikisha kuwa hawachomoki kirahisi. Hata Freeman Mbowe alifunguliwa kesi ya ugaidi na hamna hata mmoja aliwahi kusema kuwa ilikuwa kwa sababu yeye ni mkristu na Rais muislamu.

Kama unayosimulia yana ukweli wowote ni dhahiri kuwa uonevu mkubwa umefanyika dhidi ya Rajab na ndugu zake. Kuingiza udini hakuwatendei haki maana unageuza suala lao kuwa la maonevu dhidi ya waislamu ( yanayofanywa na wakristu na vibaraka wao) wakati ni mfano mwingine wa watu kutumia nafasi zao kuwaonea na kuwafanyia ukatili binadamu wenzao. Badala ya hili suala kuwa letu wote maana watu wa imani zote wamewahi kufanyiwa ukatili (mfano Mdude Nyangali) nyie mnaligeuza kuni ya kuchochea chuki kati ya waislamu na wakristu. Sio vizuri mnavyofanya.

Amandla....
Fundi....
Kuwa na subira yapo mengi nitaeleza hapa.
 
Anaitendea Vibaya sana Nchi yake kuingiza dini.

Mzee MS, katika utafiti wako sungusungu hao walikuwa Dini gani?
 
Mzee Mohamed Said ni miongoni mwa watu wanaotumia vibaya vipaji vyao kueneza chuki. Ni mjuzi sana wa kusimulia jambo kwa ufasaha, tatizo lake kubwa ni kuongeza chumvi, uongo na uchonganishi. Hapa katika suala analosimulia hapa anataja kuwa ni waislamu wameonewa!
Tundu Lisu alipigwa risasi Dodoma, sikumsikia Mohamed Said akiripoti kuwa mkristo amepigwa risasi!
Freeman Mbowe alipobambikiwa kesi ya ugaidi sikumsikia Mohamed Said akisema mkristo kabambikiwa
Yule binti Akwilina alipopigwa risasi Kinondoni sikusikia Mohamed akisema mkristo kauawa!

Kwake tatizo likimpata muislamu basi moja kwa moja anahusisha na dini yake! Mzee, haya matatizo yanawakumba wote bila kujali dini! Unapoleta udini unaupunguzia umma ile nguvu ya kusimama pamoja dhidi ya dhuluma. Sote tunapaswa kupinga dhuluma inayompata mtu yeyote bila kujali dini yake. Unaposema waislamu wamefanyiwa ubaya huu au ule, unataka kuaminisha umma kuwa ni nani kafanya ubaya huo? Halafu iweje? Chunga kauli zako mzee. Madhara yake ni makubwa.
 
Nafikiri anafanya kusudi, Watu wanaofanyiwa madhila ni wengi na katika Dini na kabila mbalimbali.

Labda anadhani wengine wasio Waislam watapata utetezi kwa wengine! Hii si sawa.

Mara nyingi nimemuasa hapa JF juu ya hilo. Yeye anaona madhila kwa wale wa Dini yake tu. Hili linaweza kukupa sifa na heshima ya muda flani, halafu baada ya hapo? Kwamba duniani tutaishi milele, kwamba spinning hazitatuhukumu!
 
Ralph...
Tundu Lissu hanihitaji mimi kumsemea halikadhalika Freeman Mbowe.
Hawa wana watu wa kutosha kuwasimamia.

Nakuwekea hapo chini kisa kingine ambacho hakuna chombo cha habari kiliripoti ingawa walikuwa na taarifa zote:

Mauaji ya Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir wa Kijiji cha Madina

Tarehe 25 Oktoba 2013 siku ya Ijumaa Waislam katika kujiji cha Madina walishambuliwa na askari na Waislam wawili waliuawa kwa kupigwa risasi.

Waislam hao ni Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir.
Hamisi Ramadhani amezikwa Handeni katika makaburi ya hospitali maiti ilipokuwa imehifadiwa.

Abu Zubeir maiti yake ilihamishwa kutoka Handeni kwa kuwa hospitali haikuwa na chumba cha barafu cha kuhifadhi maiti ikapelekwa Korogwe.

Ndugu zake Abu Zubeir waliogopa kujitokeza kuchukua maiti yake kwa kuwa askari walikuwa wakimkamata kila aliyefika hospitali kuuliza taarifa za maiti hao.

Haijulikani nani wamemzika Abu Zubeir na hadi sasa ndugu zake hawajajitokeza kujua ndugu yao kazikwa wapi kwa hofu ya kukamatwa.

Sheikh Waziri anasema yeye na wenzake walikabidhiwa maiti ya Hamisi Ramadhani siku ya Jumapili na siku hiyo hiyo walimzika katika makaburi ya hospitali sanda yake ikiwa shuka ile iliyofunika maiti yake.

Sheikh Waziri anasema juu ya kuwa maiti zile zilikuwa hazikuhifadhiwa katika baridi hali ya maiti ilikuwa nzuri kabisa.

Mashuhuda wa kifo cha Hamisi Ramadhani wanasema alipopigwa risasi Hamisi Ramadhani alishahadia kwa sauti na kila mtu alisikia shahada ile.

Allah awalaze mahali pema peponi.
Amin.

Maelezo Mafupi ya Sheikh Waziri Shuza

Siku ile ya mashambulizi tarehe 25 Oktoba 2013 Sheikh Waziri akiwa kama kiongozi wa Waislam alipigiwa simu yeye akiwa Mkata katika shughuli za biashara kujulishwa kuwa kuna watu wameuawa kwa hiyo akaombwa aende Hospitali ya Wilaya Handeni akaagalie waliouawa na majeruhi.

Taarifa zilizomfikia alipofika Handeni jioni ile zilikuwa taarifa za kuogofya.

Hali pale hospitali ilikuwa ya kutia hofu palikuwa na ulinzi mkali hospitali nzima imezungukwa na maaskari. Kwa ajili hii Sheikh Waziri hakuweza kwenda hospitali siku hiyo na hata siku ya pili yaani Jumamosi hakuweza kwenda.

Waislam walibakia majumbani kwao wakisubiri na kuomba dua.

Sheikh Waziri akiwa kiongozi alipiga marufuku shura ya aina yoyote msikitini kuhusu mauaji yale kutafuta salama.

Waislam walikuwa wanakuja kuswali na wakimaliza wanaondoka kurudi majumbani kwao.

Lakini Sheikh Waziri akawa na wasiwasi kuwa ikiwa hatafanya jambo kuna hatari ya wale marehemu kutozikwa Kiislam.

Sheikh Waziri ilipofika Jumapili ikamjia fikra ya kumpigia diwani Mushashi. Alimweleza diwani huyu kuwa Waislam wangeshukuru kama serikali wangeruhusu maiti zile wapewe ili wazizike.

Haukupita muda diwani akamfahamisha Sheikh Zuberi kuwa anaweza kwenda hospitali na kuonana na Mganga Mkuu kwa ajili ya kupewa zile maiti mbili.

Lakini Mganga Mkuu akasema kuwa amri aliyopewa na Mkuu wa Mkoa Bi. Chiku Galawa ni kuwa maiti zile zipelekwe Tanga kwa mazishi ikiwa ndugu zao hawajajitokeza na huko maiti hizo zitachangwanywa na maiti nyingine za wasio na ndugu na zitazikwa na serikali.

Ikawa sasa lazima Mkuu wa Mkoa asubiriwe ili abatilishe amri yake ya awali na endapo ruksa itatoka Waislam wa Handeni watazizika maiti hizo.

Sheikh Hamisi akaondoka kusubiri amri ya Mkuu wa Mkoa.

Mwishowe maiti ilitolewa kwa Sheikh Waziri baada ya mazungumzo marefu kati ya Mganga Mkuu na Sheikh Waziri ikizingatiwa kuwa kwa siku tatu hakuna ndugu wa marehemu aliyejitokeza kuchukua maiti.

Sheikh Waziri alifunuliwa maiti ya Hamisi Ramadhani na Mganga Mkuu mbele ya askari.akaonyeshwa jeraha la mguuni alipopigwa risasi.

Shuka haikufunuliwa kuoneshwa majeraha mengine...
Sheikh Waziri hakuwa na haja ya kutaka mengi lililomshughulisha ilikuwa ni kupata maiti ili waisiitiri.

Sheikh Waziri anasema ilikuwa wazi kuwa Polisi na Mganga Mkuu walikuwa wameshakubaliana nini cha kufanya wakati watakapoonyesha maiti kwa ndugu zao.

Mganga Mkuu alionyesha jeraha la risasi mguuni akisema kuwa hapo ndipo zilipotoka damu nyingi kusababisha kifo cha Hamisi Ramadhani.

Lakini wao walikuwa na habari kamili kutoka kwa mke wa marehemu na jamaa wengine kuwa ndugu yao alikuwa amepigwa risasi katika kibofu cha mkojo na kwa hakika sehemu ile ingawa ilikuwa imefunikwa na shuka palikuwa na uvimbe mkubwa.

Sheikh Waziri na Waislam wachache walimzika ndugu yao usiku katika makaburi hapo hospitalini.
 
Yakasikika maneno mengi na siku moja nikajiwa na kijana mmoja nyumbani kwangu simjui wala sijapata kumuona maishani kwangu.

Akaniambia kuwa katumwa na Waislam aje kwangu anieleze yanayotokea Handeni na mimi niandike makala dunia ifahamu.

Niliyosikia sikuwezi kuamini kama kweli ni kweli kama nilivyoelzwa.

Huyu kijana alikataa kunipa jina lake na alikataa kupigwa picha.
Mimi nikampa jina la kupanga, ''Deep Throat.''

Ingia Google mtafute Deep Throat.
Authenticity ya habari kama hizi at most ni Tetesi sasa ukiweka kama uhalisia huoni hujitendei haki wewe kama mwandishi wala msomaji sababu huenda unamlisha matango pori au exaggerations ?
 
Nafikiri anafanya kusudi, Watu wanaofanyiwa madhila ni wengi na katika Dini na kabila mbalimbali.

Labda anadhani wengine wasio Waislam watapata utetezi kwa wengine! Hii si sawa.

Mara nyingi nimemuasa hapa JF juu ya hilo. Yeye anaona madhila kwa wale wa Dini yake tu. Hili linaweza kukupa sifa na heshima ya muda flani, halafu baada ya hapo? Kwamba duniani tutaishi milele, kwamba spinning hazitatuhukumu!
Plato...
Unaniasa mimi badala ya kumuasa dhalim aache kudhuumu?
Usiwe na haraka kuwa na subira nina mengi nitaweka hapa na mtasoma.

Subiri hadi tamati ndipo utajua ni nani wa kunasihiwa.
Hakika haiwezi kuwa mimi.
 
SAKATA LA KUPOTEA RAJAB OMARI MTANA KIJIJI CHA LULAGO HANDENI 2013

Waislam 10 wamehukumiwa kunyongwa kwa tuhuma za kuua mlinzi mmoja.

Kufikia hukumu hii kuna mengi na chanzo chake kilianzia katika biashara ya hiliki na malipo ya ushuru kijijini Lulago.

Ninaanza leo kueleza kisa hiki kama nilivyotafiti na kuweka kumbukumbu miaka 10 iliyopita.

Rajab Omar Mtana alikuwa mwanakijiji wa kawaida tu akiishi kijijini Lulago, Handeni kama wanavijiji wengine wanavyoishi na alikuwa na biashara yake ya kuuza hiliki kama mkulima wa zao hilo.

Siku moja akaja mnunuzi mfanyabiashara wa hiliki nyumbani kwake kununua hiliki na akamuuzia.

Yule mfanyabiashara alipokuwa anatoka na gari yake akasimama kwenye kizuizi cha kulipia ushuru.

Alipotakiwa kulipa ushuru akasema kuwa si hiliki yote amenunua katika kijiji hicho kwa hiyo hawezi kulipa ushuru wa hiliki yote.

Hapo palitokea ubishi na mfanyabiashara yule akagonga lile geti na akaondoka.

Hii ikapelekea kwa wakusanya ushuru wa hapo kijijini kwenda nyumbani kwa Rajab Omar Mtana kumkamata na kumweka chini ya ulinzi katika ofisi ya serikali ya kijiji hadi hapo atakapolipa ushuru ambao yule mfanyabiashara alitakiwa alipe.

Ndugu zake Rajab Omar Mtana wakaenda pale ofisini kwa nia ya kumtoa ndugu yao na hapo pakatokea vurugu na mapigano.

Katika mapigano hayo, mgambo ambae ndiye aliyekuwa akishughulika na kudai ushuru akauawa.

Kisa hiki cha ushuru wa hiliki ndicho kilichozua balaa kubwa la mauaji na uchomwaji moto nyumba za Waislam wa kijiji cha jirani cha Madina na kuvunjwa kwa misikiti katika vijiji ambavyo vilikuwa na idadi kubwa ya wakazi wake Waislam.

Baada ya haya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akatoa amri kuwa hapana ruhusa tena ya sehemu hizo kuwa makazi kwa kuwa hizo ni kambi za ugaidi.

Mkuu wa Mkoa alisema mengi ambayo takriban yote yamedhihirika baadae kuwa hayakuwa na ukweli.

Mkuu wa Mkoa alisema kuwa wapo Al Shabab vijijini, kumechimbwa mahandaki ya vita katika vijiji na kuna silaha za kutungulia ndege nk. nk.

Mkuu wa Mkoa alizungumza na Radio Nuur, Tanga inayomilokiwa na Msikiti wa Ibadh.
Nilifunga safari hadi Radio Nuur Tanga kwa nia ya kupata taarifa kamili yalivyorushwa.

Radio Nuur waliogopa kunipa juu wala kuniruhusu kusikiliza kipindi hicho cha Mkuu wa Mkoa ingawa kabla sijahama Tanga nilikuwa mmoja wa Wakurugenzu wa radio hiyo.

Lakini niliwahoji watu waliosikia kipindi hicho.

Katika Waislam waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani Handeni ni huyu kijana Rajab Omari Mtana.

Baada ya kukaa rumande alipata dhamana yeye pamoja na wenzake na akawa nje.
Rajab Omar Mtana alirejea kijijini kwake.

Wakati anakaribia kuingia kijijini alisimamishwa na askari wa kijiji akapekuliwa na akanyang'anywa simu yake na fedha taslimu.

Baada ya mkasa huu walimwachia na yeye akaendelea na safari yake.

Lakini wakati akiwa rumande nyumba yake ilikuwa imevurugwa haifai kuishi mtu kwa hiyo alifikia kwa dada yake.

Akiwa nyumbani kwa dada yake alifatwa na watu wa serikali ya kijiji usiku akatolewa ndani na kuanza kupigwa kwa bakora na kisha kwa mapanga.

Kujitetea kijana huyu alikimbia huku akikimbizwa.
Asubuhi kulipokucha palionekana damu nyingi sana.

Taarifa ilitolewa polisi lakini hakuna kilichofanyika.
Polisi walitoa taarifa (SON/RB346/2014).

Dada yake na mumewe walikamatwa na kushitakiwa katika mahakama ya hapo kijijini na wakapigwa faini ya kila mtu shs. 20.000.

Kosa lao ni kumleta kijiji Rajab Omari Mtana mtu asiyetakiwa.

Miaka 10 imetimia Rajab Omar Mtana hajulikani alipo na inasadikiwa ameuawa na wale waliokuja kumtoa nyumbani kwa dada yake.

Rajab Omar Mtana ametafutwa kote hajapatikana na waliompiga na kumjeruhi wako huru nje hawajaguswa wala kuhojiwa na polisi.

Lakini wale waliotumiwa kwa mauaji ya mlinzi wa kijiji wamehukumiwa kifo.

Hapa kuna mengi sana ya kufikirisha mbali ya yale kuwa kulikuwapo na silaha za kutungua ndege katika vijiji hivi vya Waislam wa Handeni vilivyokuwa na nyumba za nyasi na udongo.

View attachment 2668468
Shida ya Mohamed Said ni kuamini ukweli ni kile ajuacho yeye kwa kisingizio cha kwamba amefanya tafiti. Umekwepa kabisa kusimulia kile kilichotokea wakati wa mauaji. Bahati mbaya kwako, jaji aliyewahukumu ni Mwislamu, na pia Chiku naye alikuwa mtu wa dini yako.
 
Authenticity ya habari kama hizi at most ni Tetesi sasa ukiweka kama uhalisia huoni hujitendei haki wewe kama mwandishi wala msomaji sababu huenda unamlisha matango pori au exaggerations ?
Log...
Kuwa na stahamala utajua kama ni uongo au kweli.
Usifanye haraka tulia na soma.
 
Back
Top Bottom