omujubi
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 4,325
- 2,498
asante kwa kuandika vizuri na kuonyesha uchungu ulionao kwa nchi yako. Tusipoteze muda mwingi kufikiri juu ya utatuzi wa haya matatizo na mengine kama hatujaanzia hapo kwenye kiini cha tatizo. Hapo kwenye red asiyepaelewa na aende akalale, asilalamike!Source: Mwananchi
Maoni yangu
Kwa maelezo ya Mkuchika inaonesha dhahiri kuwa ameshaandaa majibu ya hatma ya hili sakata ila sasa hivi anatafuta njia tu ya kumfikisha kwenye majibu yake. Hivi serikali gan inafanya uchunguziwa suala zito kwa kuwaita watu barabaran wapeleke taarifa za uhalifu?? hivi vyombo vyote vya usalama hawawezi kweli kufanya kazi hiyo???Hapa mwisho wa siku anataka kusema tuliwaomba wenye majina ya waloficha fedha Uswiss hawakujitokeza, hivyo km serikali tuliona habar hizo ni majungu tukaamua kuachana na hilo suala mana tulishindwa timiza kigezo vya serikali ya Uswiss.
Na je hata km majina hayo yatapelekwa kwake, je! tutakuwa na uhakuka gan kama atayafikisha Uswiss?? Najaribu kuimagine kwenye hayo majina kwa mfano katajwa JK na Pinda, hivi kweli Mkuchika atayapeleka Uswiss?? au anataka kutueleza nn hasa hapa??? Hapa suluhisho ni Tume maalum ya wabunge, tukimtegemea Mkuchika apeleke jina la aliyemteua Uswiss au mtoto wa aliyemteua Uswiss tutakuwa WENDAWAZIMU. CCM ni genge linaloongozwa na wezi hivyo tusitegemee km wanaweza wakakaangana mana wote ni wachafu. Hii kesi naona mtuhumiwa ni ngedele na hakimu ni Nyani.