Sakata la IPTL na ESCROW: Kafulila aanza kuumbuka, sasa kusambaza umeme MW 2000 Kenya

KAFULILA AUMBUKA KWA KUSEMA SETH HATAKIWI KENYA
View attachment 186998
mmililki wa IPTL na mwakandege mwanasheria wa IPTL

KAMPUNI ya kufua umeme ya Pan African Power Solution inayoimiliki kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imezidi kung’aa katika nchi za jumuia ya Afrika Mashariki katika kusambaza nishati ya umeme.

Hatua hiyo inasababishwa na serikali ya Kenya kuipatia barua kampuni hiyo ya kufanya nao kazi ya usambazaji umeme katika mradi unaohusisha nchi mbili za jumuia hiyo, ambazo ni Tanzania na Kenya.

Barua ya Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli, Injinia Joseph .K. Njoroge ya tarehe 19, Agosti 2014 kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sing Sethi.

Taarifa zaidi kuhusiana na barua hiyo, yenye kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A iliyokuwa na kichwa cha habari Expression of interest for IPP for 2000MV power generations and supply to Kenya and Tanzania.

Barua hiyo, ilieleza kuwa inazitaka pande tatu hizo ikiwemo PAP, Tanzania na Kenya kukutana haraka kuona ni namna gani uzalishaji huo utaanza haraka iwezekanavyo.
Akithibitisha barua hiyo, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema kampuni yao inaendelea kuchapa kazi na haitishiki na kauli za wanasiasa kwa kuwa wao si wanasiasa.

‘’Tunafurahi kuwa tunazidi kuaminiwa na serikali mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hii inadhirisha ufanisi na ueledi wetu katika tasnia nzima ya nishati,’’alisema.

Hivyo, alisema anaamini maneno yote yanayoenezwa juu yao kuwa yanatawaliwa na chuki na wivu wa kibiashara kutoka kampuni zingine za usambazaji wa umeme.

Kutolewa kwa barua hiyo kwa IPTL kutaweza kuondoa sintofahamu iliokuwepo, baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR- Mageuzi) kudai kuwa Seth anayeongoza kampuni hiyo amepigwa marufuku kufanya biashara ya aina yoyote Kenya.

Kafulila alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini hapa, kuwa Seth ni fisadi na kwamba Kamati ya Bunge ya nchini Kenya imempiga marufuku kufanya biashara nchini humo.
===================================

Chanzo: habarileo

tumbiri kuumbuka sana leo kwa kusambaza uongo dhidi ya kampuni za watu binafsi
 
KAFULILA AUMBUKA KWA KUSEMA SETH HATAKIWI KENYA
View attachment 186998
mmililki wa IPTL na mwakandege mwanasheria wa IPTL

KAMPUNI ya kufua umeme ya Pan African Power Solution inayoimiliki kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imezidi kung'aa katika nchi za jumuia ya Afrika Mashariki katika kusambaza nishati ya umeme.

Hatua hiyo inasababishwa na serikali ya Kenya kuipatia barua kampuni hiyo ya kufanya nao kazi ya usambazaji umeme katika mradi unaohusisha nchi mbili za jumuia hiyo, ambazo ni Tanzania na Kenya.

Barua ya Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli, Injinia Joseph .K. Njoroge ya tarehe 19, Agosti 2014 kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sing Sethi.

Taarifa zaidi kuhusiana na barua hiyo, yenye kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A iliyokuwa na kichwa cha habari Expression of interest for IPP for 2000MV power generations and supply to Kenya and Tanzania.

Barua hiyo, ilieleza kuwa inazitaka pande tatu hizo ikiwemo PAP, Tanzania na Kenya kukutana haraka kuona ni namna gani uzalishaji huo utaanza haraka iwezekanavyo.
Akithibitisha barua hiyo, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema kampuni yao inaendelea kuchapa kazi na haitishiki na kauli za wanasiasa kwa kuwa wao si wanasiasa.

''Tunafurahi kuwa tunazidi kuaminiwa na serikali mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hii inadhirisha ufanisi na ueledi wetu katika tasnia nzima ya nishati,''alisema.

Hivyo, alisema anaamini maneno yote yanayoenezwa juu yao kuwa yanatawaliwa na chuki na wivu wa kibiashara kutoka kampuni zingine za usambazaji wa umeme.

Kutolewa kwa barua hiyo kwa IPTL kutaweza kuondoa sintofahamu iliokuwepo, baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR- Mageuzi) kudai kuwa Seth anayeongoza kampuni hiyo amepigwa marufuku kufanya biashara ya aina yoyote Kenya.

Kafulila alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini hapa, kuwa Seth ni fisadi na kwamba Kamati ya Bunge ya nchini Kenya imempiga marufuku kufanya biashara nchini humo.
===================================

Chanzo: habarileo

katika hili la escrow Zitto na Kafulila lazima waumbuke kwa upigaji
 
uwezo wako ndio umefikia mwisho kufikiri?,kweli kila mpumbavu ni mjinga lakini si kila mjinga ni mpumbavu,haya endelea kuquote mdogo wangu

wewe ndio mjinga na huna uwezo wa kufikiri, hivi shadow recruit ni ID yako pia?, maana unawashwa kama vile ndiye uliyeanzisha hii thread
 
huo ni uongo mnaosambaza ninyi wenyewe, hakuna anayezuia isisomwe

Njaa mbaya. Unaendekeza njaa kwa Singasinga hadi masiko na macho yanaziba na kushindwa na kuskia na kuona agizo la 'majaji wa PAP'!

Mod kwanini mnaruhusu uhuni wa mtu mmoja kutumia IDs mbalimbali ili kutetea utumbo alioposti hapa?
 
Ripoti ishasomwa una la kuchangia mtani wangu

Wapi Pendolymo?
Siwezi kusahau tarehe ya leo 26/11/2014. Ripoti ishasomwa. Nina swali moja tu kwako, FEDHA YA ESCROW ilikuwa ya umma au ya IPTL.
Sitegemei kama utakaa kimya ktk hili.
 
Wapi Pendolymo?
Siwezi kusahau tarehe ya leo 26/11/2014. Ripoti ishasomwa. Nina swali moja tu kwako, FEDHA YA ESCROW ilikuwa ya umma au ya IPTL.
Sitegemei kama utakaa kimya ktk hili.

Mkuu hawezi kuja hapa mie pia namsubiri kwa hamu
 
Toka mwanzo nilijua kuwa hii filimbi inayopulizwa na kaka yangu Kafulila ni ya udongo wa kinyesi. Ahh! Kafulila chimba shimo la kujifukia mapema maana huko mbele tuendako wananchi watakutambua kwa true colour yako, sisimizi/Tumbili.

Baada ya bunge kujadili ripoti ya CAG na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kwa wahusika wa hili sakata la Escrow bado una ujasiri wa kuyasema tena haya maneno?
 
Mkuu hawezi kuja hapa mie pia namsubiri kwa hamu

Mshenzi sana huyu mwanamke na wenzake wengine wengi humu, mijitu ina mawazo mgando kabisa, viongozi wetu hawa ni wezi alafu inakuja mijitu humu inawatetea kwa nguvu zote. Inakera sana.
Shukurani na pongezi zimwendee SPIKA wa Bunge kwa kazi kubwa aloifanya leo. Kajijengea heshima kubwa yeye, kiti chake na Bunge kwa ujumla.
Sasa serikali ya Jakaya inaanguka kwa mara nyingine. Ni aibu kwa Taifa na kwa WATANZANIA kwa ujumla wetu.
Shame on ccm.
 
Waungwana mlio anzisha uzi huu tafadhali rejeeni tena hapa kutupa mrejesho. Ripoti imesomwa. Kwa uwazi isema yale mabilioni ni ya umma. Walioumbuka na kuibuka mashujaa tushawajua. Ni vyema mje mkiri ni nini misimamo yenu. Tafadhalini nyie "team IPTL" mkiongozwa na pendolyimo njooni mseme kitu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom