benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Wakati wa kuwasilishwa na kujadiliwa kwa hoja ya Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, moja kati ya mambo yaliyochangiwa na wabunge wengi hasa wanaotoka maeneo ya wafugaji ni suala la HERENI ZA KIELEKTRONIKI KWA MIFUGO HASA NG'OMBE
Katika hotuba iliyowasilishwa ilielezwa kuwa hadi kufikia Oktoba 30, 2022, jumla ya mifugo 5,292,738 ambao ni ng'ombe 4,460,354, punda 66,863, mbuzi 513,729 na kondoo 251,792 wametambuliwa na kusajiliwa kwenye mfumo wa utambuzi. Ingawa pia ilielezwa kuwa , tarehe 3 Novemba, 2022 Serikali ilisitisha zoezi la Utambuzi wa mifugo kwa muda ili kurekebisha kasoro
Baada ya mjadala mrefu mimi, nimevutiwa na sehemu ya mchango wa Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma ambaye mara kadhaa wakati akichangia amemtaja Mbunge wa Kibaha (Akimtaja kwa jimbo lake bila jina) kuwa "ana-lobby" wabunge wengine wakubali suala la ng'ombe kuwekewa hereni kwani yeye ni "mnufaika" wa zoezi hilo.
Mara kadhaa "Msukuma" amemtaka Mbunge huyo wa Kibaha aacahane na suala la "Ku-lobby" wabunge ili wakubali suala la kuwekea ng'ombe hereni akisisitiza kuwa Jimboni kwake Kibaha kuna Kuku wengi sana kama anaona suala hilo ni la muhimu basi ni vyema akawekee hereni kuku katika jimbo lake.
Hoja yangu ni kama kweli Mbunge wa Kibaha anawahadaa wabunge waunge mkono huduma ambayo inamnufaisha yeye binafsi (KUWEKEA HERENI KWENYE MIFUGO) je hili sio suala linaloleta MGONGANO WA KIMASLAHI, NA LINALOPASWA KUTOLEWA MAJIBU NA WAHUSIKA.
Video iko hapa unaweza kutazama: